Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday, 16 February 2013

EXCLUSIVE: MUME WA GOLDIE AIBUKA, AMPIGA BITI PREZZO!


Nobody knew bout this! Kumbe Goldie Harvey, mshiriki wa BBA stargame alikuwa ameolewa kabla hajafa! Andrew Harvey, raia wa Uingereza ameibuka na picha zote za harusi yao waliofunga kwa siri nyingine kibao wakati wakila bata pamoja.

Andrew na Goldie Harvey
Andrew na Goldie Harvey batani.
Andrew Harvey ameongeza kuwa yeye na Goldie walikuwa bado katika mahusiano na mawasiliano mazuri mpaka umauti ulipomfika. Andrew alikutana na Goldie katika party ya rafiki yake huko Lagos. Ndipo mfanyabiashara huyo wa mafuta akafunga ndoa na Goldie, December, 2005. Pia Andrew amekana marehemu Goldie kuhusishwa na matumizi yaliopitiliza ya madawa ya kulevya kuwa ndio moja ya sababu za kifo chake!


Upande mwingine pia Andrew Harvey alimpiga biti Prezzo na kumtaka kutojihusisha kabisa na maswala yoyote ya Goldie. Prezzo na Goldie walikuwa wakutane Lagos tarehe 15 February kwa ajili ya kusherehekea Valentine’s. 

Prezzo na Goldie mjengoni BBA



AKON MADENI TUPU!


Akiwa na idea ya kuanzisha website kwa ajili ya artistes mbalimbali ku-interact na fans wao, matokeo yake ni kusimama kizimbani! Akon, ‘Lonely’ singer, amefunguliwa mashtaka na kampuni ya Atlanta Business Video huko Georgia wakilalamika kuwa Akon aliwaajiri mwaka 2011 kwa kazi ya kuitengeneza site yake lakini hawajaambulia chochote.

Atlanta Business Video waliajiriwa na Akon kuiboresha “Fantrace” na kuifanya kuwa website rasmi. Kwa taarifa yako tu, “Fantrace” ilikuwa facebook forum iliyokutanisha wasanii na raia, idea ya Akon na kutengenezwa na makampuni mawili.

Atlanta Business Video waliitwa baadae na Akon ili kuiboresha na kuifanya sasa iwe website. Hapo ndipo ABV wakaingia mzigoni na kufanya kazi kwa masaa 1,023 ambapo Akon alitakiwa awalipe dola 127,875, ambazo mpaka leo Akon hajawalipa hata sumni! 

Akon

Friday, 15 February 2013

OSCAR PISTORIUS AFIKISHWA MAHAKAMANI!



Sakata la mauaji ya aliyekuwa girlfriend wa Oscar Pistorius Reeva Steenkamp limechukua sura mpya baada ya mtuhumiwa, Oscar Pistorius kufikishwa kwa pilato na kusomewa mashtaka. 

Oscar, mkimbiaji wa mbio za miguu ya bandia, alionekana akifuta machozi pale pilato alipokuwa anasoma mashtaka dhidi yake. Mahakama imeahirisha masikizano ya dhamana mpaka Jumanne ijayo na mshtakiwa Oscar amerudishwa rumande.

Oscar Pistorius anakabiliwa na mashtaka ya kumuua mpenzi wake  Reeva Steenkamp, model, kwa bastola siku ya Valentine’s. 
Oscar Pistorius akimwaga machozi mahakamani

Thursday, 14 February 2013

CHRIS BROWN NA DRAKE USO KWA USO MAHAKAMANI!


Unalikimbuka vizuri lile varangati lililotokea club moja ya usiku huko New York City kati ya Drake na Chris Brown? Lile soo sasa lipo mezani kwa pilato! Model mmoja, Romain Julien, ambaye alikuwepo usiku ule amelianzisha kwa kwenda mahakamani na kuwashtaki kuanzia Chris Brown, Drake mpaka club yenyewe, kwa majeraha aliyoyapata usiku ule kwa kile kinachoelezwa kuwa fujo hizo zilihusha kurushiana vyupa. 

Sasa kusikia hivyo Brown na Drake kwa nyakati tofauti leo hii wameenda mahakamani kila mmoja akimshtaki mwenzake kwamba anahusika na fujo pamoja na uharibifu wote uliotokea usiku ule.

Drake na Brown kwa nyakati tofauti huko nyuma walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rihanna, hicho ndio chanzo cha vurumai yenyewe!