Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday 16 February 2013

AKON MADENI TUPU!


Akiwa na idea ya kuanzisha website kwa ajili ya artistes mbalimbali ku-interact na fans wao, matokeo yake ni kusimama kizimbani! Akon, ‘Lonely’ singer, amefunguliwa mashtaka na kampuni ya Atlanta Business Video huko Georgia wakilalamika kuwa Akon aliwaajiri mwaka 2011 kwa kazi ya kuitengeneza site yake lakini hawajaambulia chochote.

Atlanta Business Video waliajiriwa na Akon kuiboresha “Fantrace” na kuifanya kuwa website rasmi. Kwa taarifa yako tu, “Fantrace” ilikuwa facebook forum iliyokutanisha wasanii na raia, idea ya Akon na kutengenezwa na makampuni mawili.

Atlanta Business Video waliitwa baadae na Akon ili kuiboresha na kuifanya sasa iwe website. Hapo ndipo ABV wakaingia mzigoni na kufanya kazi kwa masaa 1,023 ambapo Akon alitakiwa awalipe dola 127,875, ambazo mpaka leo Akon hajawalipa hata sumni! 

Akon

No comments:

Post a Comment