Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday, 11 February 2013

ASHLEY COLE ADAKA MTOTO KUPITIA TWITTER

Alilalama kuwa lonely baada ya kuachana na Cheryl Cole mwaka 2010. Lakini inaonekana wazi kuwa sasa Ashley Cole, 32, amekaa sawa baada ya kuopoa mtoto, MTV reality star na model Anna Kelle. tena kupitia mtandao wa kijamii wa twitter!
Ashley Cole
Umbea ulipo ni kuwa Ashley na Anna wana wiki mbili toka waanze uhusiano na walikuwa pamoja jijini London, Chelsea wakila bata katika shisha bar kabla ya kuelekea zao May Fair Hotel ili kuliendeleza bata!
Ashley na Anna batani!
Katika ulaji wao wa bata Ashley na Anna walijitenga na watu wengine huku wakidendeka na kushikana viuno muda wote. Baadhi ya watu waliotaka kwenda kuwapa 'hi' walizuiwa na mabaunsa! Baadae kidogo, Jumapili usiku, Anna alipost picha yake na Ashley na kuandika hivi, 'Lush night at #mayfairclub with ash #amazingclub (sic)'

Baada ya kuachana na Ashley, Cheryl Cole sasa anatoka na Tre Holloway ambaye ni dancer!

Cherl Cole na Tre Holloway




PAPA BENEDICT XVI KUSTAAFU FEBRUARY


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedict wa XVI ametangaza  kustaafu nafasi hiyo February 28. Papa huyo aliyechukua wadhifa huo toka mwaka 2005 alikutana na makardinali huko Vatican leo hii na kutangaza uamuzi huo. Katika taarifu yake Papa alisema kuwa hali ya afya yake ndio inayomfanya afikie uamuzi huo. Papa Ben XVI alionekana Ijumaa iliyopita kushindwa kutembea japo alipata usaidizi wa fimbo.

Taarifa ya Papa Ben XVI umepokelewa kwa mshtuko kwani ameutoa bila hata kushirikisha watu wake wa karibu. Na hii ni tofauti na Papa aliyemrithi, Papa John Paulo II ambaye hakuachia nafasi hiyo mpaka pale alipofariki licha ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa kipindi kirefu. 


Sunday, 10 February 2013

CHRIS BROWN APATA AJALI MBAYA


Jana, saa 6:03 mchana, Chris Brown alipata ajali mbaya na gari lake aina ya Porsche nyeusi kuharibika vibaya. Katika ajali hiyo Chris Brown aliparamia ukuta na kuuvunja kabisa. Mwakilishi wa Chis brown alitoa tamko na kusema chanzo cha ajali ya Brown ni mapaparazi. Inasemekana wapigapicha wawili walikuwa wakimkimbiza Brown. 



Porsche ya Chris Brown
Ukuta aiovunja Chris Brown
Ingawa mmiliki na bosi wa wapiga picha hao alipinga ajali hiyo kusababishwa na mapaparazi wake na kumtaka Brown kuwa makini na kauli zake.

Baada ya ajali hiyo ambayo Brown hakuumia, aliekea zake katika shule ya vipaji ya Allen Dance Academy ambapo Chris Brown kupitia kituo chake cha Symphonic Love Foundation, hutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kituo hicho.



Saturday, 9 February 2013

DIDDY AJA NA MAAJABU

Haijawahi kutokea! Kuchorwa tatuu na huku unanyolewa nywele! Lakini P Diddy amefanya hivyo. Juzi kati Sean Combs alitupia picha zake katika twitter  zikimwonyesha akinyolewa na kuchorwa tatuu kwa pamoja!
Nyoa nywele na chora tatuu
Diddy aliyekuwa anachora tatuu yenye neno ‘NEW YORK’ katika mkono wake wa kushoto na kuandika pia katika ukurasa wake wa twitter, ‘Gettin a Tat and Cut at the same damn time!! These n***** can't multitask...ha.’

Ijumaa, P Diddy aliweka historia pale alipopiga fashion show kupitia Instagram baada ya kushindwa kuhudhuria New York fashion week. Diddy aliandika, “Kupitia technologia ya instagram tunawaletea Sean John mpaka walipo watea wetu!”
Sean Combs

TIGER WOODS AMTUMIA DEMU WAKE NDEGE


Mcheza golf maarufu duniani Tiger Woods, 38, amemtumia ndege yake binafsi demu wake Lindsey Vonn aliyeko Austria ili arudi USA kwa matibabu. Vonn alipata majeraha mara mbili katika goti lake katika mashindano ya kuteleza katika barafu, Alpine Ski World Championships. 

Lindsey Vonn
Lindsey Vonn na Woods walianza uhusiano wao baada ya Woods kuachana na mkewe Elin Nordegre mwaka 2010 na Vonn kuzinguana na boyfriend wake wa muda mrefu, Thomas Vonn.
Lindsey Vonn
Tiger aliachana na mkewe Elin baada ya kukaa pamoja ndoani kwa miaka mitano na kupata watoto wawili, Samantha, 5, na Charlie, 3. Tiger ameonekana kujifunza kutokana na ,makosa yake na ameamua kuangusha moyo wake kwa Lindsey Vonn.

Tiger Woods na Elin Nordegre enzi za penzi lao