Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday 11 February 2013

PAPA BENEDICT XVI KUSTAAFU FEBRUARY


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedict wa XVI ametangaza  kustaafu nafasi hiyo February 28. Papa huyo aliyechukua wadhifa huo toka mwaka 2005 alikutana na makardinali huko Vatican leo hii na kutangaza uamuzi huo. Katika taarifu yake Papa alisema kuwa hali ya afya yake ndio inayomfanya afikie uamuzi huo. Papa Ben XVI alionekana Ijumaa iliyopita kushindwa kutembea japo alipata usaidizi wa fimbo.

Taarifa ya Papa Ben XVI umepokelewa kwa mshtuko kwani ameutoa bila hata kushirikisha watu wake wa karibu. Na hii ni tofauti na Papa aliyemrithi, Papa John Paulo II ambaye hakuachia nafasi hiyo mpaka pale alipofariki licha ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa kipindi kirefu. 


No comments:

Post a Comment