Tanzania top model audition
Tanzania top model audition
Monday, 27 August 2012
MDOGO WAKE KANUMBA ARITHI MIKOBA YA KAKA YAKE

Ni miezi kadhaa imepita sasa tangu kifo cha one of the best actor ever in Tzee film industry kwa jina la Steven Kanumba kitokee. Na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kusema kampuni ya Kanumba The Great itakuwa inafanya kazi chini ya usimamizi wa Seth Bosco na Abela au Mrs Bile ambae ni dada yake na Marehemu Steven Kanumba ambae Kanumba ndio alikua anamfata kwa kuzaliwa.
Latest infoz nikuwa company hiyo imeshakamilisha movie mpya kwa jina la “Malaika” ikiwa imeshirikisha wasanii km Rose Ndauka, Abdalah Mkumbila, Seth Bosco na Kijana Rammy Galis ambaye anatarajiwa kuwa Kanumba part 2 kutokana na muonekano wake kufanana na The late Steven Kanumba.
Filamu hii inatarajiwa kuwaburudisha mashabiki wa Kanumba na itasambazwa na Steps Entertainment LTD , kaa mkao wa kula kijipatia Copy yako pindi itapokuwa madukani.
Friday, 24 August 2012
R.I.P MATONYA
Yule ombamba maarufu kuliko wote nchini , Matonya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
“Namtaarifu Komredi Yusufu Makamba, kuwa yule kiboko yake
'MATONYA' amefariki usiku wa kuamkia leo kijijini kwakwe Mpamantwa wilaya ya
Bahi, mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni kijijini hapo. Habari ziwafikie,
Mkuu wa Wilaya Betty Mkwasa, Familia ya Mzee Makamba popote walipo, wakazi wa
Dar na Moro pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote. Bila ya kusahau wale wa
eneo la Darajani Mjini Morogoro", ameandika mwandishi wa habari Habel Chidawali
ambaye amewahi kumfanyia mahojiano ombamba huyo.
Matonya amefariki akiwa anaishi kwenye nyumba ya tembe
ambayo ni mali ya mtoto wake wa kike
aitwaye Elizabeth Matonya.
Nyumba hiyo ya asili ya watu wa Dodoma ipo kwenye Kijiji cha
Bahi Sokoni katika Kitongoji cha Nghungugu, umbali wa kilomita 3 kutoka yalipo
makao makuu ya wilaya ya Bahi.
Katika mahojiano aliyofanya na Habel, Matonya enzi za uhai wake
alisema kuwa hana mali yoyote kama wengi walivyokuwa wanadhani.
“Watu wanasema kuwa nina mali, lakini ni ‘walambi’
(akimaanisha kwamba ni waongo). Mimi sina kabisa mali; hata mbuzi; hata kuku
sina na wala sina mpango wa kununua tena hata kama nina pesa kwa kuwa
walishazoea kuniibia, hivyo sitaki tena kuwa na mali.”
Nilikuwa na ng’ombe wengi sana. Kila wakati walikuwa
wakiwaiba wakati ninaishi Kilimatinde na ng’ombe hao nilinunua kwa pesa yangu
ya kuomba huko Dar es Salaam. Walikuwa wengi lakini waliibwa wote na ndugu
zangu.
Kuhusu kuacha kuomba
Jibu: Labla serikali inijengee nyumba nzuri hapa na inipe
mtu wa kunitunza au hata wakijenga nyumba nzuri kwa mtoto wangu halafu
wanisaidie na chakula pamoja na chai ya kila siku, mimi naweza kustaafu kazi
yangu lakini bila ya kufanya hivyo kazi yangu nitakufa nayo.
Katika mahojiano hayo Matonya alisema alikuwa akipata kati
ya Sh50,000 hadi 100,000 kwa mwezi na mara nyingi alikuwa akirudi kijijini kila
baada ya miezi miwili au mitatu tangu alipoanz`a kazi hiyo mwaka 1961.
Rest in Peace Matonya.
ANA PETER WA EA RADIO AJA NA WIMBO WA " A CALL"
Mtangazaji wa show ya Power Jams ya East Africa Radio, Ana Peter ameachia ngoma mpya yenye mahadhi ya reggae iitwayo "A call".
Ngoma hii imetengenezwa na DX wa Arusha kwa kutumia beat ya riddim ya "heart &
soul riddim".
"Nimeimba kuhusu kufata ndoto zetu katika maisha,kuondokana na
dhana potofu kuwa maisha yana formula fulani.Shule ni muhimu sana katika
kuturahisishia maamuzi maishani,Pasipo uelewa na maarifa,Maisha huonekana
magumu zaidi,Matumizi ya vilevi kupita kipimo ama hata kujihusisha na utumiaji
wa madawa ya kulevya yote ni matokeo ya kupuuza malengo endelevu na kufata
mikumbo, anasema Ana.
BEN POL NEW SINGLE-PETE
Pete ni wimbo wa kwanza
wa Ben Pol tangu aachie albam yake iitwayo Maboma akiwa chini ya MLab.
Kwa maana nyingine ni kuwa huu ndio wimbo mpya aliorekodi akiwa nje ya
label ya MLAB.
"Thank God it's been a great journey and I
personally feel the singles of that album were great. I have now come with a
new production team and heading for my second album. Share it and I hope you
enjoy this record as much as I enjoyed recording it. Peace and much love," ameandika Ben kwenye maelezo yake.
Wimbo huu umendikwa na waandishi watatu akiwemo yeye mwenyewe Ben Pol, Fred
Max na Lady Peace Winnie.. Producer ni Mona
Gangsta wa Classic Sounds.
Mashairi
Verse 1;
Hadithi ya penzi langu umenikata nini mwisho
huthamini huoni pendo lako nalihitaji leo kesho
nishawahi kukosa
,mwenzenu nilisumbuka
mchana na usiku mimi,
nishawahi kukosa
nasema niliteseka mchana na usiku mimi
nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
mchana na usiku mimi,
sitaki tena kosa
najua nitateseka
mwisho sitokuwa nawe tena naulizaa
Chorus;
Kama pete yangu, inakuchomaa kidoleni
ni kama pendo langu , linakuchoma moyonii ,
bora kuitoa aaah aah ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
bora kuitoa aaah aa ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
Verse 2;
sikujali wambea
wanafki walosema
hatutadumu mimi nawe tutajaachana
wakiniona siko nawe si ndo watasema
hata nyumbani watajua tumefarakana
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
kila jema n'tendalo mie ,kwako limekuwa sio
nitakapo kujua ulipo ,wanijibu utakavyo
pete kidoleni mwako ,yanisuta mwenzio
ndo maana nikukosapo ,moyo wanienda mbio
Subscribe to:
Posts (Atom)



