Tanzania top model audition
Tanzania top model audition
Thursday, 23 August 2012
MAISHA PLUS IZ BACK
Maisha Plus is back na shughuli ya kusaka washiriki wa kuingia kijijini mwezi October utaanza rasmi siku ya Jumatatu ijayo kwa ajil.
Tofauti na usaili wa mashindano yaliyopita, vijana hao 26 watatafutwa katika vijiji ambavyo Mama Shujaa wa chakula wapatao 15 walipatikana kutokana na mchakato uliofanywa na shirika la chakula na kilimo la Uingereza la Oxfam ambalo msimu huu litashirikiana na waratibu wa shindano hilo.
“Vijana wa Maisha Plus wataingia kijijini, watakwenda kuchanganyika na hao kinamama, watakaa kwa siku tatu jumla kwa maana ya kwamba watakaa siku 12, 13 na siku 14. Katika hizi siku tatu vijana watakapochanganyika na hawa akinamama mle ndani tutatengeneza makundi ambapo kila mama mmoja mzalishaji wa chakula atakuwa na timu ya vijana tuseme watatu, wanne, sita kulingana na idadi ya washiriki wa Maisha Plus ambayo mwaka huu imeongezeka kutoka 18 hadi 26", Masoud Kipanya ambaye ndiye mratibu wa shindano hilo.
Mshindi wa mwaka huu atakamata kitika cha shilingi milioni 20.
PREZZO IN NAIJA - ATANGAZA NIA YAKE YA KUTAKA KUMUOA GOLDIE
The Big Brother Africa star game second runner up Prezzo anataka kumuoa Goldie kama atalikubali ombi lake..
Mkenya huyu mwenye miaka 32 ambaye kwa sasa yuko Nigeria, amesema safari yake ya kutoka Kenya 'haikuwa ya kwenda kucheza nchini humo' bali ameenda ku-express hisia zake za mapenzi kwa Goldie.
Prezzo, ambaye aliwaomba Wanigeria msamaha kwa jinsi alivyom-treat Goldie kwenye mjengo wa BBA, amesema anatangaza nia yake hadharani ya kutaka kumuoa Goldie kwani hata kukutana kwao kulikuwa hadharani akiongeza kuwa yuko tayari kwa lolote ambalo litamfanya kumfanye bibie huyu kuwa Mrs Prezzo.
"Sikuwa na uwezo wa kuonyesha feelings zangu zote kwa Goldie pindi tukiwa kwenye jumba la BBA kutokana na paranoia lakini kwa sasa niko tayari kupambana ili kuishinda zawadi hii itakayo nifanya niwe mshindi halisi....
Will Goldie say YES I DO kwa Prezzo...., lets wait.
THE RETURN OF J LO YA SINTA TAYARI
![]() |
| Cover ya movie ya Sinta |
Mwezi ujao kuna movie mpya inaingia sokoni. Inaitwa The Return
of JLO.
Kwenye filamu hiyo Sintah ndo main character ambapo wengine
watakaonekana ni Chalz Baba, Beny Kinyaiya, Monalisa, Nyoshi
El-sadat na wengine.
TUKINAO NDIYE BIBI BOMBA 2012
Fainali ya lile shindano la kumsaka BIBI BOMBA lililokuwa likirushwa na Clouds TV ilifanyika jana mjengoni ambapo bibi Veronica Mpangala aka Tukinao aliibuka kidedea na kuondoka na zawadi ya shilingi milioni tano toka kwa wadhamini wa shindano hilo.
| Bibi Veronica akiwashukuru wapiga kura wake kwa kumpigia kura hadi kuibuka kidedea |
| Anold (kulia) toka Zantel akimkabidhi bibi bomba mfano wa check.Katikati ni host wa show hiyo Babuu wa Kitaa. |
| Anna Said mshindi wa pili |
| Nasra Mohamed mshindi wa tatu |
| Finalists wa shindano hilo |
| Ruge akiwapongeza bibi bomba |
Subscribe to:
Posts (Atom)


