Pamoja na Diva Loveness Love kutangaza kumpiga chini Mheshimiwa mbunge Zitto Kabwe na kuendelea kumsakama kwa maswali kadhaa na jumbe mbalimbali kupitia akaunti yake ya Instagram na mitandao mingine, lakini mheshiwa ameonyesha ustaarabu kwa kuamua kujikalia kimya bila kumjibu lolote bi-dada huyo.
Haya yote yamejitokeza hasa wakati huu ambapo The Romantic voice Clouds Fm presenter wa 'Ala za Roho' Diva amemdondokea msanii mwenye mkwanja mrefu toka area code 254, 'Kerewa' hitmaker Prezzo na kwa mujibu wa Diva ni kuwa penzi lao liko moto bati!
Tanzania top model audition
Tanzania top model audition
Thursday, 23 May 2013
Tuesday, 21 May 2013
WASANII HAWA WATAPAFOMU UFUNGUZI WA BIG BROTHER AFRICA JUMAPILI HII!
Moja kati ya Tv reality shows kubwa Africa itaanza kuruka hewani Jumapili hii. Hii ni Big brother Africa 'The Chase'. Kama ulivyo utmaduni wa BBA ni lazima shamra shamra za ufunguzi wa shindano hili uambatane na show kali toka kwa sanii wakali hapa africa au nje. na wasanii watafungua shindano hili kwa mwaka 2013 tayari wameshatajwa.

Kutoka Afrika Mashariki, Kisima award winning star STL amebahatika ku-grace the stage pamoja na wasanii toka Afrika Kusini kama Mafikizolo. Toka Naija Don Jazzy B atafanya yake siku hiyo bila kumsahau Wande coal! Show itaanza saa 1:00 kwa midaya afrika ya Kati na kurushwa live na channels za DSTV!

Kutoka Afrika Mashariki, Kisima award winning star STL amebahatika ku-grace the stage pamoja na wasanii toka Afrika Kusini kama Mafikizolo. Toka Naija Don Jazzy B atafanya yake siku hiyo bila kumsahau Wande coal! Show itaanza saa 1:00 kwa midaya afrika ya Kati na kurushwa live na channels za DSTV!
![]() |
| STL |
D' BANJ APIGA SHOW NA VIATU TOFAUTI!
The koko master himself D’banj ametokelezea na kituko cha kipeke
yake on stage. This time arround, D' Banj alipanda na ku-perfom katika stage ya
MTV All Stars concert huko Durban, South Africa akiwa na raba (sneakers) mbili
tofauti miguuni mwake. Moja ikiwa ni nyeupe na nyingine ni nyeusi lakini zote
ni aina ya Guiseppe Zanotti.
Hata hapa Bongo kamchezo haka kalishawahi fanywa na rapa controversial Ney wa Mitego kwa kutupia viatu tofauti
katika videos kadhaa na katika shows mbalimbali pia.
![]() |
| D’banj |
PROFFESOR JAY AJIUNGA NA CHADEMA.
Mambo sasa yamebadilika. Msanii nguli wa Hip-hop na bongo flava Joseph Haule a.k.a Proffesor Jay, leo hii amejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na tayari amekabidhiwa kadi yake ya uanachama. Swali linalobaki vichwani mwa watu na mashabiki wa muziki Tanzania ni kuwa Je, Prof. Jay atagombea ubunge kupitia chama hicho kama ilivyokuwa kwa swahiba wake walioanza nae muziki kitambo hicho, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu?
Prof. Jay anaongeza idadi ya wanamuziki walioamua kuingia rasmi katika siasa akitanguliwa na wasanii kama Kalapina (CUF), Mwana-FA (CCM), Sugu (Mb. Mbeya-CHADEMA)
![]() |
| Prof. Jay na Sugu |
Monday, 20 May 2013
JCB AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA MZUNGU!
Mwanahip-hop toka A-Town, 'Ukiskia paah' hitmaker single, JCB ameachana na ukapera this week-end kwa kufunga ndoa. Na hizi ni baadhi ya picha za harusi hiyo iliyofanyika Arusha Jumamosi hii!
Subscribe to:
Posts (Atom)








