Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday, 17 April 2013

MR. NICE AZALIWA UPYA!

Alikuwa moto kwelikweli at his times, Afrika Mashariki na Kati. Mr. Nice, mwimbaji wa ngoma kama ‘Kikulacho’ iliyomfanya avute mkwanja mrefu pengine kuliko msanii mwingine yeyote kwa wakati wote hapa Tanzania. Baada ya kupiga shows lukuki nje na ndani ya Tanzania Mr. Nice alianza kudrop taratibu na katika press conference yake leo hii alisema sababu yeye kushuka ilikuwa ni management yake.


Mr. Nice pia alikanusha kuwahi kuwa na bifu na Jose Chameleone wa Uganda. Zaidi ya hapo Mr. Nice alizungumzia kuhusu wimbo wa “Mac Muga” wa Ali Kiba kuwa haukuwa ukimuhusu yeye na maisha yake ya kimuziki, yaani kupanda na kuporomoka kwake! Mr. Nice alikana kuwa alikwenda Afrika Kusini, hali ya kimisha ikawa mbaya mpaka kurudishwa nyumbani Tanzania. Mr. Nice alikana kwenda Afrika Kusini na kusema kuwa Ali kIba hajawahi hata siku moja kusema kuwa ngoma hiyo inamuhusu yeye Mr. Nice!


The King is back. Mr. Nice amerudi upya katika game na this time amemshirikisha DNA toka Kenya, ngoma inaitwa ‘Tafuta’. Mr. Nice ame-sign label deal na Grandpa production ya Kenya na tarehe 26 April ataanza mfululizo wa kugonga shows hukohuko KE. 

Angalia video ya Mr. Nice feat. DNA:

BI. KIDUDE AFARIKI DUNIA!

Gwiji la muziki nchini Tanzania hususan taarab asilia, Fatuma Binti Baraka "Bi Kidude" hatunaye tena. Taarifa kutoka katika familia yake zinasema Bi Kidude alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal amefariki leo. Bi Kidude atakumbukwa kama mwanamuziki mkongwe zaidi nchini ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 10 tu na aliwahi kupokea tuzo mbalimbali kutokana na mchango wake katika muziki wa mahadhi ya mwambao. Hakika sanaa nchini imepoteza moja ya nguzo kubwa.

Pumzika kwa amani Fatuma Binti Baraka.
 

Tuesday, 16 April 2013

MRS. CARTER TOUR YAANZA!

Kama kuhitaji ku-make headlines tu, basi the wife of Mr. Carter, Jay Z anao uwezo huo na katika show yake ya kwanza kabisa amefanya hivyo. Tour imeanza rasmi huko Belgrade, Serbia  Jumatatu usiku na Beyonce, 31, alipanda on stage ni kivazi cha rangi ya gold, transparent kilichoonyesha maungo yake yote ya ndani kama nipples!

BeyoncĂ© ana shows 64 na atazunguka mabara ya Europe, North America mpaka South America.
 




Monday, 15 April 2013

2013 MTV MOVIE AWARDS RED CARPET FASHION

The 2013 MTV Movie awards ilifanyika usiku wa kuamkia leo huko Los Angeles, California. Na hii ndio red carpet fashion ya A-list stars waliohudhuria utoaji wa tuzo hizi.

Serena Gomes

Hana Mae Lee

Jamie Foxx na binti yake Corrine Bishop

Kerry Washington

Kim Kardashin

RuPaul

Snoop Dogg Lion

Zoe Saldana

Saturday, 13 April 2013

PAUL WA P-SQUARE APATA MTOTO!

Baada ya pacha wake Peter kupata mtoto wa pili wa kike sasa ni zamu ya Paul. Jana Paul Okoye na mchumba wake wa muda mrefu Anita, walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume. Mtoto huyo aliyepewa jina la Andre alizaliwa Atlanta, USA.

Peter tayari ana watoto wawili, toka kwa demu wake wa muda mrefu Lola Omotayo. Welcome to the world Andre Okoye.