Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Sunday, 17 March 2013

PETER MSECHU KUZALIWA UPYA KESHO!

Peter Msechu kesho atasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka kadhaa. Peter Msechu ambaye ni Bongo Star Search na Tusker Project Fame Star anatarajia pia ku-release his new hit single hiyo kesho. 

Ngoma hiyo inaitwa 'Kumbe' amemshirikisha 'Mwamba wa Kaskazini', Joh Makin!   

Happy Birthday Peter Msechu.




Saturday, 16 March 2013

ALINGO Vs AZONTO

Kumeibuka ghasia na kutupiana kwa maneno katika mitandao ya jamii baina ya Wanigeria na Waghana kuhusiana na styles hizi mbili za Alingo na Azonto. Na sokomoko hili limekuja hasa baada ya artiste wa dancehall toka Ghana, Samini kutoa ngoma kwa kutumia biti ya Alingo kuwadis P-Squae kwa kukopi dance ya Azonto na kuitumia katika Alingo!

 Wewe unafikiri style ipi ya ku-dance ni kali kati ya ile ya Azonto na Alingo? Na je, ni kweli styles hizi zinafanana?















































LIL WAYNE BADO YUPO HOI HOSPITALI!

Young Money Cash Money brother, Lil Wayne alikimbizwa hospitali hivi majuzi baada ya kuzidiwa. Hali yake ilikuwa mbaya sana kiasi cha kukutwa akiwa sakafuni chumbani kwake hajitambui. Mpaka sasa hali ya Wayne si nzuri sana licha ya ku-tweet kuwa yupo poa!


Ndugu, jamaa, marafiki na rap artistes kadhaa walimiminika hospitalini siku ya Jumatano kumjulia hali Wayne. Hali hii ya Lil Wayne inatokana na ubwiaji unga aina ya codeine uliopitiliza. Inasemekana madaktari walikuta kiasi kikubwa cha madawa hayo mwilini mwa Wayne hivyo kupelekea madaktari kuamua kuusafisha mwili wa Wayne mara tatu.

Pamoja na hayo yote jana Ijumaa Lil wayne aliibuka na ku-tweet kuwa yupo fresh na kuwashukuru fans wake kwa sala zao na upendo kwake!











Thursday, 14 March 2013

CHRIS BROWN DOING FINE IN CHINA!

Still he makes the heads of lines. 'Turn Up the Music' star Chris Brown is back in business! Jana Jumatano alikuwa zake location, huko Los Angeles California aki-shoot video ya single yake mpya,  ‘Fine China’.

Mcheck Brown na co-star wake katika video hiyo wakifanya yao while getting ready for the audio and video single! 

Are you there Rihanna?










Wednesday, 13 March 2013

MICHAEL JACKSON ALIPOIMBA KISWAHILI!

Ni ngoma ya 'Liberian Girl'. Ndani ya ngoma hii iliyorekodiwa na kutolewa mwaka 1987 toka katika albam ya 'Bad' ndio ina maneno yasemayo, 'Nakutaka pia, Nakupenda pia, Mpenzi wangu'! Sio kwamba Michael Jackson alisema moja kwa moja maneno haya kwa Kiswahili bali yeye alitafsiri maneno hayo kutoka kwa SouthAfrican singer, Letta Mbulu. Alichofanya MJ ni kutafsiri kutoka Kiswahili moja kwa moja kwenda Kiingereza.

Wataalamu wa mambo wanasema kuwa hii ni heshima kubwa kwa jamii ya Afika Mashariki na Kati pia.