Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday, 15 February 2013

OSCAR PISTORIUS AFIKISHWA MAHAKAMANI!



Sakata la mauaji ya aliyekuwa girlfriend wa Oscar Pistorius Reeva Steenkamp limechukua sura mpya baada ya mtuhumiwa, Oscar Pistorius kufikishwa kwa pilato na kusomewa mashtaka. 

Oscar, mkimbiaji wa mbio za miguu ya bandia, alionekana akifuta machozi pale pilato alipokuwa anasoma mashtaka dhidi yake. Mahakama imeahirisha masikizano ya dhamana mpaka Jumanne ijayo na mshtakiwa Oscar amerudishwa rumande.

Oscar Pistorius anakabiliwa na mashtaka ya kumuua mpenzi wake  Reeva Steenkamp, model, kwa bastola siku ya Valentine’s. 
Oscar Pistorius akimwaga machozi mahakamani

Thursday, 14 February 2013

CHRIS BROWN NA DRAKE USO KWA USO MAHAKAMANI!


Unalikimbuka vizuri lile varangati lililotokea club moja ya usiku huko New York City kati ya Drake na Chris Brown? Lile soo sasa lipo mezani kwa pilato! Model mmoja, Romain Julien, ambaye alikuwepo usiku ule amelianzisha kwa kwenda mahakamani na kuwashtaki kuanzia Chris Brown, Drake mpaka club yenyewe, kwa majeraha aliyoyapata usiku ule kwa kile kinachoelezwa kuwa fujo hizo zilihusha kurushiana vyupa. 

Sasa kusikia hivyo Brown na Drake kwa nyakati tofauti leo hii wameenda mahakamani kila mmoja akimshtaki mwenzake kwamba anahusika na fujo pamoja na uharibifu wote uliotokea usiku ule.

Drake na Brown kwa nyakati tofauti huko nyuma walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rihanna, hicho ndio chanzo cha vurumai yenyewe!





Wednesday, 13 February 2013

DMX AKAMATWA NA POLISI!

Leo hii asubuhi rapper DMX alitiwa mbaroni kwa masaa kadhaa baada ya kudakwa na polisi kwa kosa la kuendesha gari bila leseni, huko South Carolina! DMX alipigwa pingu na kupelekwa kituo cha polisi ambako alikaa masaa kadhaa kabla ya kuachiwa huru.

Baada ya kuachiwa DMX alikiri kutokuwa na leseni, hivyo kukamatwa na polisi, kulipa pesa huku akilalamikia muda wake uliopotezwa bure. "No, I didn't have a license ... put the cuffs on me. Brought me here. I paid the money. Basically, just 5 hours wasted for nothing."

Kituko ni kuwa, kwa muda wote huo wa tukio binti yake wa miaka 5 alikuwa kiti cha nyuma cha gari la DMX!
DMX





MANCHESTER UNITED WALITEKA JIJI LA MADRID

Zaidi ya mashabiki 4,000 wa Red Devils a.k.a Manchester United wapo jijini Madrid kuisapoti timu yao ambayo leo hii itakutana uso kwa uso na Los Blancos a.k.a Real Madrid, Santiago Bernabeu. Leo hii mchana baadhi ya wachezaji wa Man U walijumuika na mashabiki wao kabla ya mtangane wenyewe utakao vurumishwa usiku huu majira saa 4:45 usiku!












Santiago Bernabeu




Tuesday, 12 February 2013

AFISA POLISI WA KESI YA CHRIS BROWN AJIUZULU


Kamanda wa polisi aliyeratibu na kusimamia adhabu ya Chris Brown ya kuhudumia jamii, amejiuzulu cheo chake. Pamoja na mahakama na kitengo cha Polisi cha Los Angeles kusema kuwa Chris Brown hakukamiisha muda aliotakiwa kuifanya kazi jamii lakini Bryan Norwood amekuwa upande wa Brown mpaka kufikia hatua ya kuandika barua akimtetea Chris kuwa alimaliza muda huo vile inavyotakiwa.

Tetesi zinasema kuwa Bryan Norwood ameacha kazi ili akafanye kazi kama hiyo ya upolisi huko Raleigh, North Carolina, lakini scandal ya Brown ndio inachukuliwa kama sababu kuu na halisi!
Kamanda Bryan Norwood & Brown
Hakimu katika kesi ya Chris Brown kumchapa Rihanna amemhitaji Brown kuithibitishia mahakama kwamba kweli alimaliza muda wote aliotakiwa kuihudumia jamii, kinyume chake Brizzy atakuwa katika wakati mgumu!
                                                                                                                   Wakati huohuo baada ya utolewaji wa tuzo za grammy, Chris Brown na Rihanna wakiwa pamoja batani walionekana wakivuta sigara tena kwa kupokezana, inasemekana kuwa ni bangi!

Brown & Riri na bangi yao