Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday 12 February 2013

AFISA POLISI WA KESI YA CHRIS BROWN AJIUZULU


Kamanda wa polisi aliyeratibu na kusimamia adhabu ya Chris Brown ya kuhudumia jamii, amejiuzulu cheo chake. Pamoja na mahakama na kitengo cha Polisi cha Los Angeles kusema kuwa Chris Brown hakukamiisha muda aliotakiwa kuifanya kazi jamii lakini Bryan Norwood amekuwa upande wa Brown mpaka kufikia hatua ya kuandika barua akimtetea Chris kuwa alimaliza muda huo vile inavyotakiwa.

Tetesi zinasema kuwa Bryan Norwood ameacha kazi ili akafanye kazi kama hiyo ya upolisi huko Raleigh, North Carolina, lakini scandal ya Brown ndio inachukuliwa kama sababu kuu na halisi!
Kamanda Bryan Norwood & Brown
Hakimu katika kesi ya Chris Brown kumchapa Rihanna amemhitaji Brown kuithibitishia mahakama kwamba kweli alimaliza muda wote aliotakiwa kuihudumia jamii, kinyume chake Brizzy atakuwa katika wakati mgumu!
                                                                                                                   Wakati huohuo baada ya utolewaji wa tuzo za grammy, Chris Brown na Rihanna wakiwa pamoja batani walionekana wakivuta sigara tena kwa kupokezana, inasemekana kuwa ni bangi!

Brown & Riri na bangi yao






No comments:

Post a Comment