Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday, 30 August 2012

MSINIITE MZEE MAGARI.


Nyota kwenye tasnia ya filamu nchini Charles Magari amekataa kuitwa mzee while age yake imeshasogea.
Hali hiyo ilitokea hivi karibuni baada ya wasanii chipukizi kumpa jina la 'mzee' kutokana na ushauri wake anaowapa wasanii hao kwenye tasnia hiyo.

"Mimi sitaki kabisa kusikia mtu ananiita mzee wakati ni kijana, nashangaa kila nikipita mitaani naitwa mzee waambieni na wengine silitaki jina hilo”, Mzee Kijana Magari.

Pia mzee Magari alisema kuwa yupo mbioni kuzindua filamu yake inayoitwa "Zig Zag" iliyoandaliwa na Pilipili Entertainment, mbapo ndani yake kutakuwepo na vichwa kama Haji Adam na Mohamed Fungafunga.

MWAKA WA SHETANI KWA MAY D, YOU TUBE ACCOUNT YAKE YAFUTWA


We all know that May D hivi sasa hayupo tena chini ya label ya Square Records, leboiliyokuwa isimamia kazi zake hadi hivi majuzi alipotimuliwa.
Kwa upande mwingine inashtusha kusikia kuwa official YouTube channel ya singer huyu liyokuwa ikisimamiwa na Iroko Partners imefutwa siku mbili zilizopita pamoja na video zake za "Soundtrack" na "Ile Ijo".
Pamoja na videos za nyimbo hizo, page nyingine zilizotolewa ni pamoja na  streams za still clips.
Square Records’ Youtube accounts pia zinasimamiwa na Iroko Partners.
Hadi sasa haijawekwa wazi iwapo ni  Square Records, Iroko au hata  May D mwenyewe aliyeamua kuifuta account hiyo.
Infoz za kuaminika zinadai kuwa hadi sasa hakuna e-mail hata moja iliyotumwa kwa Iroko na pia Square records kuulizia issue imeibiwa.
Kwenye recent interviews Psquare waliweka wazi kuwa kuondoka kwa May D kwenye label hiyo kutamfanya kuwa na ya kujibu kiuongozi zaidi.

GADNER HUYO TIMES FM ATAKUWA AKITANGAZA SHOW IITWAYO MASKANI




Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM katika kipindi cha Jahazi, Garder G Habash aka Captein anatarajia kuanza kutangaza tena Jumatatu ijayo kupitia kituo cha radio cha Times FM 100.5 cha Dar es Salaam kwenye kipindi cha .
"Maskani" kitakachokuwa kikiruka from Jumatatu to Ijumaa saa 10 jioni hadi saa 1 usiku.


Gadner akiongea machache baada ya kutambulishwa Times FM
  Rumors dong the rounds ni kuwa mtangazaji huyo atakuwa akilipwa shilingi milioni 5 kwa mwezi na kama tetesi hizi zitakuwa ni za kweli basi Gadner atakuwa the most paid radio personality in Tezee.





Kipindi chake kinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na kipindi chake cha zamani,  Jahazi cha Clouds FM ambacho kwa sasa huendeshwa na Arnord Kayanda, Wasiwasi Mwabulambo na Ephraim Kibonde.

Hata hivyo Clouds FM watakuwa na advantage katika mikoa mingine ambayo Times FM haisikiki.

Picha ya pamoja ya baadhi ya watangazaji wa Times FM. Kutoka kushoto ni: Gadner, Schola, Natasha, Ndimbo, Dida na Joet.
Kwa upande wa Dar es Salaam, Maskani ina nafasi kubwa ya kuchukua wasikilizaji wengi wa Jahazi hasa wanaosikiliza radio wakiwa majumbani.

Times FM wana disadvantage ya frequency walinayo ya 100.5 ambayo gari nyingi haizifikii na hii ni kwa sababu kuna wasikilizaji wengi jijini Dar es Salaam wanaosikiliza radio kwenye magari.

ITAZAME OFFICIAL REMIX YA WIMBO WA MATAPELI WA JAGUAR