Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday, 21 May 2013

PROFFESOR JAY AJIUNGA NA CHADEMA.

Mambo sasa yamebadilika. Msanii nguli wa Hip-hop na bongo flava  Joseph Haule a.k.a Proffesor Jay, leo hii amejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na tayari amekabidhiwa kadi yake ya uanachama. Swali linalobaki vichwani mwa watu na mashabiki wa muziki Tanzania ni kuwa Je, Prof. Jay atagombea ubunge kupitia chama hicho kama ilivyokuwa kwa swahiba wake walioanza nae muziki kitambo hicho, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu?

Prof. Jay anaongeza idadi ya wanamuziki walioamua kuingia rasmi katika siasa akitanguliwa na wasanii kama Kalapina (CUF), Mwana-FA (CCM), Sugu (Mb. Mbeya-CHADEMA)


Prof. Jay na Sugu

 
 
 

Monday, 20 May 2013

JCB AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA MZUNGU!

Mwanahip-hop toka A-Town, 'Ukiskia paah' hitmaker single, JCB ameachana na ukapera this week-end kwa kufunga ndoa. Na hizi ni baadhi ya picha za harusi hiyo iliyofanyika Arusha Jumamosi hii!



 

SIKILIZA HOTUBA YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE KUHAIRISHWA LEO HII!


Friday, 17 May 2013

MNYAMA AMPOTEZEA ANACONDA

TID a.k.a Mnyama amemtema au amemtolea nje Lady Jay Dee a.k.a anaconda kushiriki katika show yake ya kutimiza miaka 13 katika mziki pale Nyumbani Lounge mwishoni mwa mwezi huu. Hii inakuja baada ya Jay Dee kuingia katika mzozo mkubwa na Mkurugenzi utafiti wa redio binafsi, Clouds Fm, Ruge Mutahaba!
 
Katika kuthibitisha kwake kutoshiriki show hiyo, TID aliandika hivi katika ukurasa wake wa facebook:-
“Three reasons why I can’t do Lady Jay Dee Show….. No 1 I have better contract which pays me better than. No 2 I really don’t want to be between anybody’s conflict, ya kwangu yananishinda naona niepushe shari. No3 nataka kuoa muda wangu ndio huu………. Kama nimekukosea captein na madame kazeni but I have been tru the same shit”
 
TID anaungana na wasanii kama Linah, Barnaba na Matonya ambao walishatangaza hapo wali kuwa hawatashiriki kabisa katika show hiyo. Amebaki Professor Jay.