Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday, 9 April 2013

KANYE WEST AIBA NGOMA!


Roc-A-Fella Records & Good Music Rapper Kanye West, 35, ameingia matatani kwa kuiba baadhi ya mistari na kuitumia katika ngoma yake ‘Gold Digger’. Jana Jumatatu Trena Steward na Lorenzo Pryor, watoto wa David Pryor, ndio waliofungua kesi hii kwa niaba ya baba yao aliyeimba wimbo huo 'Bumpin Bus Stop' kwa kushirikiana na bendi yake, Thunder & Lightening mwaka 1974.
 
Ni sekunde 13 tu za wimbo wa David Pryor  ndio West alikopi mistari pia tune ambayo ni 'Get down' three times’ huku West alisema, 'Get down, girl, go head get down' three times’. Trena Steward na Lorenzo Pryor, watoto wa David Pryor kila mmoja anamiliki robo ya tune katika wimbo huu na wanahitaji fidia ya $ 150,000 pamoja gharama za wakili.

Hii sio mara ya kwanza kwa West kupelekwa mahakamani kwani  mwaka September, 2012, New York record label, TufAmerica ilimfungulia mashtaka West kwa kuchukua mistari ya ngoma ya Eddie Bo,  'My Beautiful Dark Twisted Fantasy' na kutoa ‘Stronger’.







Monday, 8 April 2013

A GAME TWO CAN PLAY! BROWN Vs RIHANNA.

Juzi Chris Brown alionekana anamhofia babyboo wake Rihanna kwamba anaweza kumsaliti wakati akiwa katika tour yake. Lakini inaonekana kama Rihanna ndio wakumhofia  Chris Brown wakati alipoonekana aki-party club na dada duu mmoja usiku wa Jumamosi! Brown alionekana akishikana mikono na mtoto huyo huku akimpa chupa moja ya champagne huko Los Angeles nightclub.


 
Wakati hayo yakitokea kwa Brown, Rihanna ,25, alionekana Jumapili (siku inayofuata) akicheki basketball match kati ya Los Angeles Clippers dhidi ya Los Angeles Lakers na mchizi mwingine kabisa!
 

 
Nani hapa anamdanganya mwenzake? Is it Brown or Riri?

Saturday, 6 April 2013

VIMINI MARUFUKU UGANDA!

Serikali ya Uganda iko mbioni kupeleka muswaada bungeni ili kupitisha sheria itakayo kataza wakina dada na kina mama kuvaa nguo fupi, kama vimini. Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo jirani, Bw. Simon Likodo ametoa tamko hilo akisema kuwa mwanamke yeyote atayevaa nguo itakayoonyesha maeneo yake nyeti atakuwa amevunja sheria na ataadhibiwa.
Waziri huyu ambaye ni Padre wa zamami wa Kanisani aligusia pia suala la picha chafu za ngono na kusema, "Serikali itaweka system itakayotambua raia yupi kaingia kwenye mtandao upi na hivyo kumtambua ni nani kaangalia picha chafu, 'pornographic pictures'.

Hii inamaanisha kuwa hata wasanii kama Beyonce na Madonna watapigwa marufuku kuja Uganda. Pia luninga za Uganda hazitaruhusiwa kuonyesha picha chafu zenye kuonysha maungo ya mwanamke.

Adhabu kwa mwanamke atapatikana na hatia ya kuvaa nguo fupi atapigwa faini ya Shilingi za Kiganda milioni 10 sawa na pauni 2,500. Au miaka 10 jela! Waganda wengi wako kinyume na kupitia mitandao ya facebook na twitter wameendesha kampeni '#SaveMiniSkrt' inayolenga kupinga muswaada huu!


Thursday, 4 April 2013

CHRIS BROWN AJA NA AZONTO, AWAKERA WAGHANA!


Rihanna's boo Chris Brown amelikoroga! Ni baada ya jana kufanya interview moja na BET na kutangaza kuwa katika video yake mpya ya single, 'Fine China' atakayoitoa hivi karibuni itakuwa na dance yenye style ya Azonto. Na akakiri kuwa style hiyo alifundishwa na WizKid msanii toka Nigeria hivyo kuonekana kana kwamba style hiyo ni ya Wanigeria.
Hapo ndipo msala ulipoanza kwani Waghana wanahisi Chris Brown alikosea kwa kusema kuwa asili ya Azonto ni Nigeria. vymbo vya habari huko Ghana havikuwa nyuma katika hili kwani blog moja 'Ghana Celebrities’ aliandika,
"Chris Brown Talks About AZONTO On BET, But He Says The Dance Is A Nigerian Thing". Mtandao huo uliendelea kuandika, "It seems Chris Brown coming to Ghana and introducing Nigerian artiste-Wizkid on stage to do Azonto was not a mere mistake. In fact, Chris Brown thinks Azonto is a Nigerian thing. Probably he is taking the piss out of Ghanaians by failing to credit Ghana with the dance which has gained international recognition"

Kwa upande mwingine Chris Brown pengine hajui lolote kuhusu asili ya Azonto na kwa vile alifundishwa kucheza style hiyo na WizKid msanii toka Nigeria ndio maana Chris Brown anaihusisha Azonto na Nigeria na sio Ghana!

EXCLUSIVE: KANYE WEST & KIM KARDASHIAN WAMWAGANA!

Rapper Kanye West na The reality Tv show star Kim Kardashian wameripotiwa kuachana. Ingawa hakuna taarifa rasmi kutoka kwao lakini gigs has it kuwa mastaa hawa ambao kila kukicha hushika vichwa vya habari duniani si wapenzi tena.
Inasemekana mastaa hawa wanashindwa kutangaza kuachana wakihofia vyombo vya habari pia kuachana kwao kutaonekana kumetokea muda mfupi sana tangu waamshe penzi lao. Pia sababu nyingine inayowafunga mdomo ni mtoto wanayetarajia kumpata hivi karibuni! Sababu ya tatu Kanye anasubiri mpaka ali-release album yake mpya.