Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday, 4 April 2013

EXCLUSIVE: KANYE WEST & KIM KARDASHIAN WAMWAGANA!

Rapper Kanye West na The reality Tv show star Kim Kardashian wameripotiwa kuachana. Ingawa hakuna taarifa rasmi kutoka kwao lakini gigs has it kuwa mastaa hawa ambao kila kukicha hushika vichwa vya habari duniani si wapenzi tena.
Inasemekana mastaa hawa wanashindwa kutangaza kuachana wakihofia vyombo vya habari pia kuachana kwao kutaonekana kumetokea muda mfupi sana tangu waamshe penzi lao. Pia sababu nyingine inayowafunga mdomo ni mtoto wanayetarajia kumpata hivi karibuni! Sababu ya tatu Kanye anasubiri mpaka ali-release album yake mpya.
 
 

Tuesday, 2 April 2013

KWANZA FM YA LADY JAY DEE IPO NJIANI!

Nani kakwambia mtu mzima anatishiwa nyau? Maisha mipango. Huyu ndie ‘Anakonda’! Lady Jay Dee a.k.a Judith Habash mwenyewe ame-break tena the pieces of news kwamba kituo chake cha redio kipo karibu kufunguliwa! Oh my God!

“Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee
— Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013

Huwezi kuanza mapambano km hujajizatiti, si utapigwa ufe? Vita ni pale tu unapokuwa tayari. Sikuwa tayari huko nyuma ndio maana sikuongea — Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013


Tweets hizi zimekuja baada ya kuishutumu The Super Brand Radio Station Clouds Fm kwa kile alichokiita ni kumbania kwa kupiga nyimbo za wasanii ambazo watu ama mashabiki hawazikubali ilihali bado kituo hicho kinajiita redio ya watu!

Anaconda

Monday, 1 April 2013

MAMBO 7 MWANAUME HUTAKIWI KUYATAMKA UKIWA NA MPENZI WAKO KITANDANI!

1. Kumzungumzia mpenzi wako aliyepita:
Kuzungumzia mapenzi yako yaliyopita juuya kitanda uiwa na menzi wako ni sumu kali. Mademu wote hawataki kusikia maongezi haya kwa vile tu atajiskia vibaya na wivu zaidi.

2. Kulitaja jina la mwanamke mwingine:
Kikawaida demu yoyote anajua kwamba ulikuwa na wakati mzuri na mademu zako waliopita lakini kila mwanamke anapenda kujisikia she is the only one in your heart. Hivyo kama ukijifanya kulitaja jina la demu mwingine on bed basi kuwa tayari kwa lolote hasa kuomba msamaha na kufanya lolote atakalokuamrisha ili mradi tu uthibitishe kuwa she is the most beautiful, sexiest and intelligent!

3. Kumnyamazisha:
“Shssss kaa kimya basii jamaniii” Unahitaji mchuchu akae kimya wakati umempeleka mwenyewe kileleni!? Acha zako. You have blown her mind already so mwache mtoto a-enjoy!

4. Kumlinganisha na demu wako aliyepita:
Mademu wote huhisi wako saw asana kitandani. So ukisema, “Wewe ni mtamu kama ex-girlfriend wangu”, mara moja utampotezea appetite ya ku-do na kumtengenezea mwaswali kadhaa likiwemo hili, “Unamfikiria yeye tu wakati una-do na mimi?”. Na“Ungependa kuwa naye muda huu badala yangu?”

5. Kujifanya una haraka:
Kumtonya mwanadada kuwa huna muda mwingi wa kukaa naye hivyo muda si mrefu utasepa, hii itamkata mood kabisa. So ni vizuri kama unataka kukaa na kuspend na mpenzi wako basi utenge muda wa kutosha naye.

6. Kwenda chooni hovyo:
Ni balaa. Kidogo tu mtoto wa kiume unafungua mlango wa chooni. Ni vyema kujipanga kwa kuhakikisha uko vizuri kimwili kwa offload haja zote kabla hamjaanza mambo yenu!

7. Kupokea simu kila wakati:
Kumbuka huu ni wakati wa faragha kati yako na mpenzi wako. Kama unahisi simu yako huita kila mara basi vyema ukaweka ‘silent’ ili mkishafanya yenu then uwacheki waliokuwa wakikutafuta na sio simu kuiacha ikilia na hivyo kukata stimu kabisa za mapenzi!
 

SASA NI BIFU RASMI KATI YA LADY JAY DEE NA CLOUDS FM!

Unalikumbukua bifu la Kalapina na Clouds Fm? Na la Mheshimiwa Sugu na hawahawa jamaa je? Sasa ni zamu ya Malkia wa mziki wa Bongoflava Lady Jay Dee. Judith Wambura Habash amefunguka rasmi na kulianika wazi bifu lake na Clouds Fm ‘The Superbrand Radio Station’! Bado chanzo halisi cha bifu hilo halijafahamika rasmi lakini kupitia tweets zake Jay Dee unaweza kujua ni nini mke wa Gadner G. Habash alichokuwa anakimaanisha!

Baadhi ya tweets zake zinazungumzia kana kwamba kwa sasa Clouds Fm wameamua kumbania kugonga ngoma zake na kuzipigia promo zaidi ngoma zingine hasa bendi mpya inayosemekana kuja kwa kasi zaidi, ‘Skylite Band’. Band hii inaundwa na baadhi ya wasanii waliondoka Machozi Band akiwemo Jonnical Flower!
Tweets za Lady Jay Dee anayetamba na ngoma yake mpya ‘Joto Hasira’ akilalamikia ukandamizaji kama sio unyanyasaji huo zinakwenda kama hivi:-
JD: Radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu.
#JotoHasira
JD:Kill me if u can. Am on fire. Siogopi ng’ooooooo. Jipangeni.
JD: Ni kweli nimelamba sumu lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily. I will survive.
*****Lady Jay Dee
Hee! Kuna wajinga wanadhani nilitweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka-hack ac yangu nooo it’s me.
*****Mnalishwa chungu na tamu na vyote mnakula. #JotoHasira
*****Anaedai kuianzisha Bongoflava aliapa kuiua bongoflava. Sasa hata wasiojua Hiphop nao wana beef na bongoflava! Damn!!
*****Kama tweets zangu zinakukwaza pls unfollow taratibu na kwa amani. Happy Easter.
*****Vinyoka nyamazeni achene Anaconda aongee #JotoHasira
*****My name is Judith Wambura Habash. Hii imeandikwa kwenye passport. Gmorning!








Wednesday, 27 March 2013

D' BANJ AMTWANGA MAKOFI MANAGER WAKE, AMTIMUA KAZI!

Wiki chache zilizopita, aliyekuwa manager wa Koko Master, Dapo Oyebanjo a.k.a D'banj, Abisagboola Oluseun John aka Bankuli alifukuzwa kazi na kichapo juu! Chanzo cha data hii kinasema kuwa mnamo December mwaka jana baada ya show, 'Koko concert', Bankuli alipaa zake kwenda Paris Ufaransa kuipigia promo album mpya ya Kanye West bila kumpa taarifa D'Banj. Koko Master akampa vitasa/makofi na kumtimua kazi right away!
Bankuli alivunja ukimya na alikuwa ana yake ya kusema,"D’Banj hakunifukuza ila ni uamuzi wangu mwenyewe" Bankuli pia alikana kufanya kazi na Kanye West bila ruhusa ya D' Banj!
Inasemekana D'Banj ni msanii mgumu kum-manage. Anaamua atakacho na ni mgumu kufuata ushauri vile kila mtu anayefanya kazi naye, Baba (D’Banj) mwisho wa siku aliamua kusepa zake!
 
D'Banj na Bankuli