Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday 1 April 2013

SASA NI BIFU RASMI KATI YA LADY JAY DEE NA CLOUDS FM!

Unalikumbukua bifu la Kalapina na Clouds Fm? Na la Mheshimiwa Sugu na hawahawa jamaa je? Sasa ni zamu ya Malkia wa mziki wa Bongoflava Lady Jay Dee. Judith Wambura Habash amefunguka rasmi na kulianika wazi bifu lake na Clouds Fm ‘The Superbrand Radio Station’! Bado chanzo halisi cha bifu hilo halijafahamika rasmi lakini kupitia tweets zake Jay Dee unaweza kujua ni nini mke wa Gadner G. Habash alichokuwa anakimaanisha!

Baadhi ya tweets zake zinazungumzia kana kwamba kwa sasa Clouds Fm wameamua kumbania kugonga ngoma zake na kuzipigia promo zaidi ngoma zingine hasa bendi mpya inayosemekana kuja kwa kasi zaidi, ‘Skylite Band’. Band hii inaundwa na baadhi ya wasanii waliondoka Machozi Band akiwemo Jonnical Flower!
Tweets za Lady Jay Dee anayetamba na ngoma yake mpya ‘Joto Hasira’ akilalamikia ukandamizaji kama sio unyanyasaji huo zinakwenda kama hivi:-
JD: Radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu.
#JotoHasira
JD:Kill me if u can. Am on fire. Siogopi ng’ooooooo. Jipangeni.
JD: Ni kweli nimelamba sumu lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily. I will survive.
*****Lady Jay Dee
Hee! Kuna wajinga wanadhani nilitweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka-hack ac yangu nooo it’s me.
*****Mnalishwa chungu na tamu na vyote mnakula. #JotoHasira
*****Anaedai kuianzisha Bongoflava aliapa kuiua bongoflava. Sasa hata wasiojua Hiphop nao wana beef na bongoflava! Damn!!
*****Kama tweets zangu zinakukwaza pls unfollow taratibu na kwa amani. Happy Easter.
*****Vinyoka nyamazeni achene Anaconda aongee #JotoHasira
*****My name is Judith Wambura Habash. Hii imeandikwa kwenye passport. Gmorning!








No comments:

Post a Comment