Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday, 23 February 2013

KANYE WEST AMTOSA KIM KARDASHIAN!

Alilaumiwa sana kwa kutokea mara kadhaa katika reality shows za demu wake Kim Kardashian mwenye ujauzito wa miezi minne! Na sasa inaonekana Kanye West amelitilia maanani suala hili na sasa hataki tena!

Kanye West ametangaza rasmi kumtosa Kim K katika maana ya kutoonekana kabisa katika shows hizo katika kile alichosema kuwa kuonekana mara nyingi on tv kitampunguzia umaarufu mbele ya hadhira!


Moja kati ya sababu za kuachana na boyfriend wake wa zamani, NFL football player Reggie Bush ni kukataa kutokea katika reality shows za Kim, sasa itakuaje kwa KW baada ya kumtosa KK ku-appear katika shows zake?

KW & KK


PREZZO AND FRIENDS PAYING LAST RESPECT TO GOLDIE



OSCAR PISTORIUS APATA DHAMANA


Oscar Pistorius yupo huru! Mkimbiaji mbio kwa miguu ya bandia ameachiwa na yupo nje kwa dhamana kufuatia kesi inayomkabili ya kutuhumiwa kumuuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp  siku ya Valentine, February, 14. Dhamana inakaribia randi ya Afrika Kusini 1,000,000 ambayo ni dola 113,000 za Kimarekani.

Pistorius aliyekuwa rumande kwa siku 8 amepewa masharti kadhaa ya dhamana yakiwemo kusalimisha pass yake ya kusafiria na silaha zote anazomiliki. Pistorius pia haruhusiwi kutoka nje ya mji wa Pistorius na la mwisho haruhusiwi kutumia kinywaji chochote chenye kilevi!

Kesi ya Pistorius imeahirishwa mpaka June 4.

Oscar Pistorius


Friday, 22 February 2013

WIZ KHALIFA + AMBER ROSE = SEBASTIAN 'THE BASH' TAYLOR THOMAZ

Hatimaye penzi limejibu. Habari njema kwa whole world of entertainment kwamba rapper Wiz Khalifa na supa model Amber Rose wamepata mtoto wa kiume na kupewa jina la Sebastian 'The Bash' Taylor Thomaz na Wiz Khalifa. Asubuhi ya Ijumaa Amber, 29, ali-break the news yote kuwa the new baby born is in town!


Cameron Jibril Thomaz a.k.a Wiz, 25,  alionekana akiwa so emotional huku akiwa amembeba mwanae mikononi. Later Wiz alitweet kitu cha kushangaza. Eti baada ya Amber kujifungua kitu cha kwanza kuhitaji ni 'whiskey na sigara'!
 

Kwa nyakati tofauti wazazi wote, Wiz na Amber walijipongeza kwa kumpata mtoto, pia Rihanna alitweet pongezi za kutosha kwa Amber kwa kumleta duniani Sebastian ‘The Bash’



Thursday, 21 February 2013

KIM KARDASHIAN SI LOLOTE

Ni maneno ya mwigizaji filamu Ghana, Juliet Ibrahim. Juliet amechukizwa na mkwanja wa dola 500,000 aliovuta Kim Kardashian kwa kutokea on stage tu, tena chini ya dakika moja katika concert ya ‘Love Like A Movie’. Kupitia istagram yake, Julie aliandika, 

“Sijajua kwanini alilipwa kiasi kile cha pesa plus gharama ya kumsafirisha. Huku akiperform for oonly sekunde 45 tu! Ni wakati sasa wa ku-appreciate vipaji vyetu vya Africa. Uzuri wangu ni wa asili na sio wakufanya upasuaji”

Pamoja na hayo aliyoyasema Julie lakini bado kuna sababu kuu za Kim K kudondoshwa Nigeria. Moja ikielezwa kuwa ni sababu ya kibiashara zaidi. KK akifahamika zaidi duniani kwa kuwa na wafuasi milioni 15 katika twitter na ‘likes’  milioni 12 katika facebook. Endorsements kadhaa plus super producer boyfriend. Je kama Julie angehost show ile angeweza kuvutia watu locally na internationally? Obviously ‘no’!