Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday 23 February 2013

OSCAR PISTORIUS APATA DHAMANA


Oscar Pistorius yupo huru! Mkimbiaji mbio kwa miguu ya bandia ameachiwa na yupo nje kwa dhamana kufuatia kesi inayomkabili ya kutuhumiwa kumuuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp  siku ya Valentine, February, 14. Dhamana inakaribia randi ya Afrika Kusini 1,000,000 ambayo ni dola 113,000 za Kimarekani.

Pistorius aliyekuwa rumande kwa siku 8 amepewa masharti kadhaa ya dhamana yakiwemo kusalimisha pass yake ya kusafiria na silaha zote anazomiliki. Pistorius pia haruhusiwi kutoka nje ya mji wa Pistorius na la mwisho haruhusiwi kutumia kinywaji chochote chenye kilevi!

Kesi ya Pistorius imeahirishwa mpaka June 4.

Oscar Pistorius


No comments:

Post a Comment