Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday, 29 January 2013

RICK ROSS ANUSURIKA KIFO


Alfajiri ya jana Jumatatu, The Miami based rapper William Roberts a.k,a Rick Ross alinusurika kuuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana. Ross alikuwa akitoka kwenye birthday party yake ya 37. Party hiyo ilihusisha list ndefu ya mastaa wakiwemo P Diddy, Fabolous Quincy Combs na Christina Milian just to mention a few.

Ross
Ross na Diddy
Ross, P Diddy, Fabolous Quincy Combs na Christina Milian
Rick Ross akiwa njiani huko Las Olas Boulevard baada ya kula bata usiku mzima, alianza kutupiwa risasi yeye akiwa ndani ya gari lake aina ya Rolls Royce ya silver isiyoingiza risasi! Katika sekeseke hilo dereva wa Ross alijikuta aligonga nyumba ya watu baada ya gari kupoteza mwelekeo.

 Hakuna mtu aliyejeruhiwa kutokana na taarifa ya polisi lakini inasemekana kuwa pengine bifu la muda mrefu lililopo kati yake na 50 Cent inaweza ikawa sababu.



Monday, 28 January 2013

NI WAKATI WA LULU KUTENGENEZA PESA?

Alifariki tarehe 7 April, 2012 na kuzikwa tarehe 10 April,2012. Ni miezi 9 imepita baada ya kifo cha mwigizaji maarufu Steven Charles Kanumba, The Great. Sababu au chanzo cha kifo chake kimekuwa bado kitendawili mpaka sasa huku kila mtu akijaribu kukisia sababu halisi. Baadhi ya media na hata polisi wamekuja na ripoti kuwa pengine unywaji uliopindukia wa kilevi cha whiskey, Jacky Daniels ndio sababu. Kuna waliosema eti Kanumba alikuwa mfuasi wa Freemasons ila alikiuka baadhi ya maagizo ndio ikapelekea kifo chake. Wengine wakasema kusukumwa na mwigizaji mwenzake Elizabeth Michael Kimemeta au Lulu ndio chanzo kufuatia majibizano kati yake na Kanumba wanaosemekana walikuwa wapenzi. Hii ikasababisha Lulu kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ‘kuua’ na baadae ‘kuua bila ya kukusudia’. Lulu akatupwa rumande, tarehe 11 April, 2012.


Dhamana inayofikia milioni 40 imepitishwa na taratibu za kimahakama zimefuatwa hivyo Lulu  ametoka! Kifuatacho ni Lulu kugeuka kuwa lulu mbele ya media kwani vyombo vyote vya habari, ndani na nje vitamtafuta kwa ajili ya interviews. Sababu ni kuwa inaaminika Lulu pekee ndiye anayejua ukweli wa nini kilitokea usiku ule kabla ya umauti wa The Great!

Ni ukweli kuwa Lulu atakuwa bize sana kipindi hiki wakati kila media ikitaka story hiyo ya ndani ‘Exclusive’ ya kifo cha Kanumba. Je, Lulu ataweza kuendana na presha za media hizi? Je, ni wakati wa Lulu kupumzika kiakili na kimwili baada ya sekeseke hili, japo bado halijaisha!
Lulu ni lulu sasa! Ana mpango gani? Ameshafikiria tukio lake kuligeuza na kuwa bidhaa? Au yeye ataishia kulia na kupangusa machozi atakapokuwa anahojiwa na huku wengine wakiingiza pesa? Wakili wake pia ana mchango gani katika hili? Wazazi je?


Wapo waliojigeuza lulu kuendana na matukio na usupastaa wao mbele ya jamii. Mfano harusi ya Jay Dee na Gadner. Bang magazine pekee walipewa haki juu ya picha hizo. Huko South Africa kuna media ambayo tayari imeshanunua haki za kurusha kifo cha Mzee Nelson Mandela. Hayo ni baadhi tu ya matukio ambayo yaligeuzwa na mengine yataweza kugeuzwa kuwa bidhaa na kuingiza hela nyingi!


Sunday, 27 January 2013

TOP 5 FIGURES

1. Kim Kardashian: Reality Star
Familia nzima ya mabinti wa Kardashian wamejaaliwa figure namba 8. Like them or loathe them (kubali au kataa), lazima tukubaliane kwamba Kim amejazia! Swali tunalojiuliza ni kuwa baada ya kujifungua atabaki na curve yake ileile?
Kim Kardashin
 2. Beyonce: Singer
Kabla na baada ya kuzaliwa kwa Blue Ivy, umbo la Beyonce, the queen of pop, limebaki vilevile. Before she was married kila msanii alitamani kuchukua chuma hiki but Jay-Z is the luckiest man. Akilia mtamu, akinuna bado mtamu, akicheka ndio kabisaaa! 
Beyonce
3. Amber Rose: Model
Curves are an understatement when it comes model, X-Kanye West’s girlfriend Amber Rose. It is said kwamba Amber appeared too much for him (Kanye). She’s pregnant too just like Kim. Lets keep an eye on her kama atabaki na umbo lake no. 8!
Amber
 4. Nicki Minaj: Singer
Eti Nicki Minaj’s ba-donka-donk inabidi ipewe its own area code. Inasemekana watoto wanachora umbo lake as they state their perfect women. Nicki is one the curvy celebrity that’s pretty fabulous in the present entertainment industry.
Minaj
5. Christina Aguilera: Singer
So what if she dresses the way she does, don’t judge her. Maybe she gets ready in the dark and doesn’t really know just how much chest and thighs she reveals each and every episode of the Voice. 
Aguilera

Saturday, 26 January 2013

MVUA YAMNYEA DAVID BECKHAM

Jana Ijumaa David Beckham alionekana akirandaranda jijini London. Tofauti na hali ya hewa ya jua huko Los Angeles,London ni baridi na mvua. Akiwa bado matembezini mara mvua ikaanza kunyesha hivyo kumfanya Beckham kuhaha akitafuta sehemu ya kujikinga.

Achana na dhahama iliyomkuta bado Becks alionekana so stylish as usual. Juu alitupia kofia almaarufu baker boy flat cap, viatu vya brown akimechisha na t-shirt yake cheki his narvy valvet jacket.

Beckham ,Vicky na familia yake wamerudi jijini London baada ya kumaliza mkataba na timu ya Los Angeles Galaxy.
Welcome back Becks!
 







Beckham akitoka nduki


TIMBERLAKE NA JAY-Z NDANI YA SUIT NA TIE

He is the mastermind behind Rihanna’s 2007 comeback track Umbrella. This time around anamrudisha tena the former ‘N Sync star, Justin Timberlake. He is Shawn Carter a.k.a Jay-Z katika mtoko mpya wa Timberlake, "Suit and Tie"! 

Ijumaa (jana), Jay and Timber walikuwa very busy wakitengeneza video ya ngoma hiyo mpya na one of the very interesting part of that video ni pale Timber anapoonekana ameshikilia mwamvuli mweupe wakati Jay akiitupia mikono yake mifukoni, kama hana habari vile!

Ni matayarisho ya albam mpya ya Timberlake iitwayo 20/20 Experience ambayo rasmi itakuwa sokoni March 19. Stay Tuned!


Timberlake & Jay-Z

Justin Timberlake