Nazizi, rapper toka Kenya wa crew ya Necessary Noise amemwanika mtoto wake wa kiume anaitwa Tafari huko Nai! Nonini ameonekana akiwa na Tafari muda mwingi na hasa hivi majuzi alipokuwa na katika breakfast show, OneFm.
Mwaka huu Tafari anatimiza miaka 3 na anaoneka he is just like his mother kwa swaga zake.
Baada ya kufulia kimuziki achilia mbali maisha, star wa 'Kikulacho' toka nchini Tanzania aliamua kuhamishia shughuli zake za kimuziki nchini Kenya. Na huko Kenya alidaka dili la kusaini mkataba na GrandPa records na kufanikiwa kurekodi ngoma kadhaa. Miezi miwili sasa imeshapita toka alambe mchongo huo lakini hii leo the CEO wa kampuni GrandPa records, Refigah aliitisha press conference na kutangaza kumtema Mr. Nice.
Refigah alieleza sababu za kumwaga Mr. Nice ni pamoja na uzembe wa msanii, kutokuwa mshindani kimuziki na msanii mwenewe kutoheshimu mkataba huku ikisemekana kuwa kumbe Mr. Nice alikuwa na mkataba na record label nyingine huku Tanzania angali amesaini na GrandPa records.