Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday, 23 February 2013

ARSENAL KUMSAJILI FALCAO NA NANI!

Jijini London, Klabu ya Arsenal imemkabidhi manager wake Arsene Wenger pauni milioni 80 kwa ajili ya kukitengeneza kama sio kukiimarisha kikosi chake. Arsenal imekuwa katika wakati mgumu sana kipindi hiki hasa baada ya kutolewa katika michuano ya FA na Blackburn na hivi majuzi kukandamizwa 3 tena palepale Emirates Stadium! Mipango ya Arsenal Wenger ni hii;- Kwanza kumsajili straika wa Athletico Madrid anayezitoa udenda klabu nyingi duniani kwa sasa, Radamel Falcao. Dau la Falcao ni pauni milioni 40. Pili upo mpango wa kumsajili Luis Nani kutoka klabu ya Manchester United kwa dau la pauni milioni 20.

Radamel Falcao
Luis Nani
Arsenal mkononi wana pauni milioni 150 zakutumia zitokanazo na mauzo ya jezi katika mkataba wao wa miaka mitano na kampuni ya Fly Emirates. 

Jack Wilshere
Wenger mwenye mkataba na Arsenal mpaka 2014 amesema kuwa atatangaza uamuzi wake kama atabaki au kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa mkataba wake 2014, japo Alhamisi ya juzi alipewa nafasi ya kusaini mkataba mpya na bodi ya Arsenal.

Mario Mandzukic (kushoto) akitupia la tatu (Arsenal Vs B. Munich)
Arsene Wenger

CASH MONEY WAIBA NGOMA.

Music label Cash Money Records inayomilikiwa na Lil Wayne na Birdman wameingia matatizoni na watatakiwa kusimama mbele ya pilato kujibu shtaka la ku-sample wimbo wa "Love Gonna Pack Up (and Walk Out)" wa bendi ya The Persuaders.

Robert Poindexter, producer wa bendi hiyo ya miaka ya 1970 alisema kuwa ngoma hiyo iliyorekodiwa mwaka 1972 ndio imezalisha ngoma ya "Still Ballin” ya Bow Wow ikiwa imetengenezwa na Cash Money Records. Poindexter alisema si Cash Money wala Bow Wow walipata ruhusa ya ku-sample wimbo huo. Ilipotoka "Love Gonna Pack Up (and Walk Out)" ilifanikiwa kutop charts mbalimbali huko US of A.

Poindexter amesema kuwa aliwafuata Cash Money kwa ajili ya kuzungumzia ishu hii lakini Cash Money wakamwambia awasiliane na Bow Wow. Alipowasiliana na Bow Wow huko pia akarudishwa kwa Cash Money na ndio maana akaamua kuwashtaki Cash Money. Poindexter anahitaji zaidi ya dola 600,000 katika kesi hii. 