Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday, 7 February 2013

LIL KIM ARUDI UTOTONI


The Lady Marmalade star, Lil Kim alionekana tofauti sana alipotokelezea kwa mara kwanza Hollywood wiki iliyopita. Pia Kim alionekana wa tofauti kabisa alipotokea ku-party huko West Hollywood. Umri wa miaka 38 lakini bado alitoka na sura ya kitoto iliyomfanya kila mtu amshangae!
Lil Kim na Mariah Carey, 1997
Mwonekano wake huo umefanya watu waanze kuhisi kuwa Lil Kim amefanya plastic suggery ili kurudisha mwonekano wake. Lil Kim ali-make headline hivi majuzi kwa kupiga collabo katika video mpya ya Miley Cyrus


Kim na Miley Cyrus


RIHANNA KAFA KAOZA KWA CHRIS BROWN!

Hicho ndicho unachoweza kusema kama tafsiri ya yale anayoyafanya ‘The Umbrella singer’ Rihanna kwa Chris Brown. Kwani licha ya kuchezea kipigo mwaka 2009 pamoja na mavurugu mengine kibao ya mapenzi lakini mtoto Rihanna hakomi hachoki hahemi kwa The Bad boy Brizzy!
Chiss Brown & Rihanna, 2009
Pamoja na kichapo na huku kesi ikiwa kwa pilato lakini bado Riri alimsindikiza Brown mahakamani Los Angeles, jana Jumatano. Kabla ya Brown kuzama mahakamani Rihanna alimuaga Brown kwa mabusu na maneno yakumtia moyo. Brown bado yuko na tuhuma za kutomaliza muda aliopewa na mahakama kwa ajili ya kuhudumia jamii!
Brown akiingia kortini akisindikizwa na Rihanna
Mama yake Brown, Joyce Hawkins, Brown na Rihannawakiingia kortini
Chris Brown na wakili wake
Chris Brown akihudumia jamii kwa kufanya usafi wa mazingira
Kesi imeahirishwa mpaka tarehe 5 April. Brown 23 na Rihanna, 24 waliondoka mahakamani pamoja wakiwa wameshikana mikono.

Cheki video ya mahakamani:


Wednesday, 6 February 2013

MADONNA AMFUNIKA BEYONCE


Bado huko duniani wanajaribu kuangalia nini kilitokea na kilinganisha show ya Beyonce na ya wasanii wengine waliopita, hasa Madonna ambaye ndio mtu wa mwisho kufanya show ya Super Bowl, Feb 05, 2012 kabla ya hii ya Beyonce, Feb 03, 2013.

Madonna
Beyonce
Inaripotiwa kuwa japo show ya Mrs. Carter ilikuwa such an incredible one lakini haikuvutia watazamaji wengi kama ile ya Madonna ambayo ndio show iliyovunja rekodi. 

Pamoja na Beyonce,31, kujiandaa kwa miezi mitano pia kupewa sapoti na her former Destiny’s Child members, Kelly Rowland na Michelle Williams, rekodi zilizotoka jana zinaonyesha Beyonce aliangaliwa na watazamaji milioni 104 wakati Madonna alitazamwa na watu milioni 112.5

Madonna alipewa shavu na artistes kama na CeeLo Green, Nicki Minaj and LMFAO.


MUTHONI THE DRAMMER QUEEN KUPAFOMU FAINALI YA AFRIKA, 2013


Msanii wa Kenya, Muthoni Ndonga a.k.a Muthoni The Drammer Queen ata-grace stage ya fainali ya mataifa ya Afika 2013 alongside well known celebrities! Fainali ya mataifa ya Afrika itafanyika Nelson Mandela Bay Stadium, huko Port Elizabeth mnamo tarehe 10, February.

Muthoni The Drammer Queen
Tunampongeza MDQ ambaye ni mjasiriamali pia rapper na mwandishi wa mashairi for this beautiful achievement!


MDQ


Tuesday, 5 February 2013

DAVID BECKHAM AANZA RASMI BIASHARA, UFARANSA!

Inasemekana kuwa sasa mpira ni kazi ya pili ya Beckham, ya kwanza ni biashara, ziwe zake binafsi au zile zinamhusisha yeye na Paris Saint-Germain, PSG! Ni mtoko mpya wa biashara yake ya boxer kwa wanaume katika picha mbili alizotoa akionyesha samples za bidhaa zenyewe! 

Becks alisajili PSG kwa miezi 5 aliandika katika katika ukurasa wake wa facebook. Hizo picha ni sehemu ya mtoko wangu  (wa bixers) uitwao H&M, kaeni tayari kwa mengi zaidi wiki hii