Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday 7 February 2013

RIHANNA KAFA KAOZA KWA CHRIS BROWN!

Hicho ndicho unachoweza kusema kama tafsiri ya yale anayoyafanya ‘The Umbrella singer’ Rihanna kwa Chris Brown. Kwani licha ya kuchezea kipigo mwaka 2009 pamoja na mavurugu mengine kibao ya mapenzi lakini mtoto Rihanna hakomi hachoki hahemi kwa The Bad boy Brizzy!
Chiss Brown & Rihanna, 2009
Pamoja na kichapo na huku kesi ikiwa kwa pilato lakini bado Riri alimsindikiza Brown mahakamani Los Angeles, jana Jumatano. Kabla ya Brown kuzama mahakamani Rihanna alimuaga Brown kwa mabusu na maneno yakumtia moyo. Brown bado yuko na tuhuma za kutomaliza muda aliopewa na mahakama kwa ajili ya kuhudumia jamii!
Brown akiingia kortini akisindikizwa na Rihanna
Mama yake Brown, Joyce Hawkins, Brown na Rihannawakiingia kortini
Chris Brown na wakili wake
Chris Brown akihudumia jamii kwa kufanya usafi wa mazingira
Kesi imeahirishwa mpaka tarehe 5 April. Brown 23 na Rihanna, 24 waliondoka mahakamani pamoja wakiwa wameshikana mikono.

Cheki video ya mahakamani:


No comments:

Post a Comment