Tanzania top model audition
Tanzania top model audition
Monday, 4 February 2013
THE MULTI-MILLION SHOW YA BEYONCE, SUPER BOWL, HII HAPA!
Sunday, 3 February 2013
"MUHAMMAD ALI WA LEO AU KESHO"
“Bondia mkongwe duniani Muhammad Ali, 71, atakufa wakati wowote ule”. Ni maneno ya kaka
yake bondia huyo kutokana na hali aliyokuwa nayo. Inasemekana, Ali yu zofle
hali, mahtuti kitandani! Rahman Ali ameongeza kuwa Ali haongei na hawezi kumtambua
mtu yeyote. “Kama si miezi basi siku, Ali anaweza kututoka, tumwachie Mungu”,
alisema Rahman.
![]() |
| Muhammad Ali |
![]() |
| Rahman Ali |
Muhammad Ali alipatikana na ugonjwa wa Pakinson (kutetemeka mwili) mwaka
1984. Alionekana katika Olimpiki mwaka 1996 na mara ya mwisho 2012 huko London na
alikuwa dhaifu mno kiasi cha kusaidiwa na mkewe kutembea.
Rahman Ali anamtuhumu shemejie, mke wa Ali kwa
kutoruhusu ndugu wa Ali kumtembelea. “Mara ya mwisho ilikuwa July ndipo
niliongea na Ali, tena kupitia simu”, alifunguka Rahman.
![]() |
| Muhammad Ali na mkewe Lonnie |
Mke wa Muhammad Ali, Lonnie
amekataa kuzungumza lolote juu ya hali ya mumewe na tuhuma za Rahman.
Saturday, 2 February 2013
BRAND NEW ALICIA KEYS
Mama wa Egypt, 2, Alicia Keys yupo busy hivi sasa akitengeneza
mtoko wake mpya, ‘Brand New Me 2’. Alicia, 32, amewashirikisha mme wake Swizz
Beats na shosti wake Jada Pinkett Smith, mke wa Will Smith.
![]() |
| Keys, Beats na Pinket |
Si mara ya kwanza kwa Pinket
kushirika katika video ya Alicia, alifanya hivyo mwaka 2008 katika video ya ‘Superwoman’
akiwa na Jaden, mtoto wake!
![]() |
| Pinket on set |
Weka mziki pembeni, Jumatano iliyopita Alicia Keys
alikuwa zake Ufaransa aki-promote movie yake mpya, ‘The Inevitable Defeat of
Mister and Pete’ ambayo ameitengeneza mwenyewe na kuitengenezea wimbo. Pia Keys
alihudhuria uzinduzi wa simu mpya ya Blackberry yeye akiwa kama balozi wake. Stay tuned for the video!
![]() |
| Pinket & Alicia |
JUSTIN BIEBER MVUTA BANGI
‘Baby singer’, Justin Bieber
amedakwa tena anavuta sigara haramu, bangi! Picha kadhaa za JB inasemekana zimeshasambazwa
katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikimwonyesha Bieber, demu wake na
mshkaji wake Lil Ze wapasiana vipisi vya bangi huko Los Angeles, juzi Alhamis!
![]() |
| Bieber na kijiti mkononi |
Mwezi uliopita JB alipigwa picha
akivuta ganja akiwa na rapper Lil Twist katika hotel party huko Newport Beach.
Subscribe to:
Posts (Atom)



















