Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Sunday, 3 February 2013

"MUHAMMAD ALI WA LEO AU KESHO"


“Bondia mkongwe duniani Muhammad Ali, 71,  atakufa wakati wowote ule”. Ni maneno ya kaka yake bondia huyo kutokana na hali aliyokuwa nayo. Inasemekana, Ali yu zofle hali, mahtuti kitandani! Rahman Ali ameongeza kuwa Ali haongei na hawezi kumtambua mtu yeyote. “Kama si miezi basi siku, Ali anaweza kututoka, tumwachie Mungu”, alisema Rahman.
Muhammad Ali
Rahman Ali
Muhammad Ali alipatikana  na ugonjwa wa Pakinson (kutetemeka mwili) mwaka 1984. Alionekana katika Olimpiki mwaka 1996 na mara ya mwisho 2012 huko London na alikuwa dhaifu mno kiasi cha kusaidiwa na mkewe kutembea. 
Rahman Ali anamtuhumu shemejie, mke wa Ali kwa kutoruhusu ndugu wa Ali kumtembelea. “Mara ya mwisho ilikuwa July ndipo niliongea na Ali, tena kupitia simu”, alifunguka Rahman.
Muhammad Ali na mkewe Lonnie
Mke wa Muhammad Ali, Lonnie amekataa kuzungumza lolote juu ya hali ya mumewe na tuhuma za Rahman.

Saturday, 2 February 2013

BRAND NEW ALICIA KEYS


Mama wa Egypt, 2, Alicia Keys yupo busy hivi sasa akitengeneza mtoko wake mpya, ‘Brand New Me 2’. Alicia, 32, amewashirikisha mme wake Swizz Beats na shosti wake Jada Pinkett Smith, mke wa Will Smith.
Keys, Beats na Pinket
Si mara ya kwanza kwa Pinket kushirika katika video ya Alicia, alifanya hivyo mwaka 2008 katika video ya ‘Superwoman’ akiwa na Jaden, mtoto wake!
Pinket on set
 Weka mziki pembeni, Jumatano iliyopita Alicia Keys alikuwa zake Ufaransa aki-promote movie yake mpya, ‘The Inevitable Defeat of Mister and Pete’ ambayo ameitengeneza mwenyewe na kuitengenezea wimbo. Pia Keys alihudhuria uzinduzi wa simu mpya ya Blackberry yeye akiwa kama balozi wake. Stay tuned for the video!
Pinket & Alicia

JUSTIN BIEBER MVUTA BANGI


‘Baby singer’, Justin Bieber amedakwa tena anavuta sigara haramu, bangi! Picha kadhaa za JB inasemekana zimeshasambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikimwonyesha Bieber, demu wake na mshkaji wake Lil Ze wapasiana vipisi vya bangi huko Los Angeles, juzi Alhamis! 
Bieber na kijiti mkononi
Mwezi uliopita JB alipigwa picha akivuta ganja akiwa na rapper Lil Twist katika hotel party huko Newport Beach. 

HUYU NI NANI?


REAL LIL WAYNE!

Ulikuwa na urongo mtupu kwamba Lil Weezy kanyoa dreadlocks zake. Kumbe memba mwenzake wa YMCMB Mack Maine alizi-edit nywele za Wayne kwa kutumia social networks! Oh my Gush!!
Real Lil Wayne