Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday, 25 July 2013

GENEVIVIE ANA MIAKA 10 HAJA-DO!

Hii imechukuliwa kama gia ama kick ya kumlegeza bwana wake ili aharakishe ndoa yao kwa mwanamama mahiri katika tasnia ya uguzaji, Genevivie Nnaji kusema kuutangazia umma kuwa, ana miaka kumi toka alipofanya ngono kwa mara mwisho. 



Hivi ndivyo Nnaji anavyofunguka,

      "Nimekuwa single na mpweke kwa muda mrefu.                         Hata nilipokuwa na D'banj, mahusiano yetu                               yalikuwa ya muda mfupi sana kinyume na matarajio                 yangu. Namshukuru Mungu sasahivi nimempata                       mwanaume ambaye nitamaliza naye maisha yangu yote"

Wednesday, 24 July 2013

NYAKATI MBILI MBAYA ZA BEYONCE!

Hii ilikuwa ni tour yake iitwayo 'B-Day tour' akiperform 'Ring the Alarm'. Hapa alidondoka mzima mzima wakati akipanda ngazi za steji.


Katikati ya show yake ya mwezi March mwaka huu, Beyonce alimpa microphone shabiki wake aliyekuwa na midadi kwelikweli, ili nae aimbe kidogo japo mistari miwili mitatu. Kumbe jamaa hajui lolote. Shabiki huyo,  Princess Eugenie alipopewa mic aligeuka bubu ghafla. Whoops!


WASANII WATANO WASIOJUA KUIMBA JAPO MASHABIKI WANAWAKUBALI!

1.KEYSHIA COLE
Inatakiwa atafutwe mtu amwambie binti huyu wa Frankie kuwa sauti yake haijakaa sawa. Ni lazima atafute mwalimu wa sauti ili amuweke sawa.


2.ALICIA KEYS
Baada ya kuzaa, Alicia amerudi tena kuwa mzuri ajabu kimuonekano. Lakini kiumbaji hasa vocally, wataalam wa mziki wanasema ameshuka sana. Na hii ni baada ya kuambatana na mumewe Swizz Beatz. Sauti yake haijarudi na kuwa tamu tena.

3.JUSTIN BIEBER
Ana uwezo mzuri wa kulimiliki jukwaa lakini linapokuja suala la sauti, Bieber hamgusi Usher hata Maxwell. Kwa mwendo huu miaka kumi toka sasa anaweza kuwa amesahaulika.


4. MICHELLE WILLIAMS
Michelle anaboa sana. Sauti yake bado haijawa ile ya kuweza kumuweka katika list ya waimbaji bora USA kutokana na vile ana pata shida sana kufikia nota za juu katika uimbaji wake. Alikuwa memba wa Destiny child. Pengine hii ndio sababu iliyomfanya asionekana kung'aa katika kundi hilo lililovunjika na hata kupotea kabisa tofauti na Beyonce na Kelly Rowland. 


5. ROBIN THICKE
Robin anaonekana mlazimishaji kwelikweli. Anataka kwenda high notes lakini hafiki inavyotakiwa kimuziki. Tafura performace yake ya BET 2013.


Thursday, 18 July 2013

NUKUU YA LEO

DIAMOND ASHIKA NAMBA MOJA AFRIKA MASHARIKI!

Kubali au kataa, mpende au mchukie lakini ukweli utabaki palepale kuwa kwasasa msanii toka Tanzania, Diamond Platnumz a.k.a Naseeb Abdul ndio mwenye nguvu kubwa zaidi katika majukwaa yote ya Afrika Mashariki.



Kwa mujibu wa website moja huko Kenya anayemfuata kwa ni nguli Dk. Jose Chameleone ambaye kwa kipindi kirefu sana ameweza kukusanya raia wengi popote pale anapopiga show hasa East Africa. Achana na Chameleone, Diamond hivi sasa ameonekana kung'arisha zaidi huku makampuni makubwa hasa ya Kitanzania kila leo yakibisha hodi nyumbani kwa Diamond ili kuingia naye mikataba (endorsements).

Moja kati ya vipimo sahihi vya Diamond kuwa juu kwasasa ni ile show ya Congo iliyosababisha foleni ambayo haijawahi tokea huko Congo kutokana na umati uliopitiliza kumwagika barabarani! Pia kuna hii tour ya Burundi. Nyomi la hatari lilimwagika kupita mategeo ya waandaaji.