Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Sunday, 23 June 2013

KIM KARDASHIAN AFURAHIA KUMNYONYESHA MTOTO WAKE.

Kim Kardashian AFURAHIA KUMNYONYESHA NORTH WEST

Mwana dada Kim au Mbabs wa Kanye west anasema anafurahia zaidi anavyo mnyonyosha mtoto wake North West hadharani na hii ni tofauti kabisa na kile alicho kisema hapo nyuma katika mwaka wa 2010 kuwa hakufurahishwa na mama mmoja aliyekua akimnyonyesha mwanae Restaurant na kumbadilisha nepi chafu. lakini kwa sasa Kim huyo huyo alikua akipinga  ndio anafanya maswala ya kunyonyesha hadharani kwa ukamilifu.


Friday, 14 June 2013

WILL SMITH AMLA DENDA MWANAE JADEN!

Katika hali ya kawaida lazima ishangaze lakini lengo lilikuwa ni kuonyesha tu ni jinsi gani baba yaani Will Smith anampenda na yuko karibu mno na mwanae Jaden Smith mpaka kufikia hatua ya kumla denda mbele ya kioo cha Thai Television walipokwenda kui-promote movie yao ya 'After Earth'! 

Woody Milintachinda ndiye mwanzilishi wa tukio hilo katika kipindi chake cha The Woody Talk huko Thailand pale alipouliza kama Will na Jaden wana ukaribu wowote kama baba na mwana katika maisha yao ya kawaida (maisha halisi) kwasababu kwenye movie yao walioitoa hivi karibuni ya 'After Earth' hakuna ukaribu wowote baina yao. Katika kutaka kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye na mwanae wako karibu kuliko watu wanavyofikiri basi akaamua kumpiga kiss mwanae Jaden




Hii ndio trailer la 'After Earth':-


:

Wednesday, 12 June 2013

ASHANTI KUTOKA UPYA NA JA RULE

Unazikumbuka hits "Always On Time" and "Mesmerize". Ni ngoma zilizowatakatisha vizuri Ja Rule na Ashanti na kuwafanya waoenekane moja kati ya collaboraters wakati huo. Sasa baada ya Ja Rule kutoka jela, Ashanti amesema kuwa yupo mbioni kufanya tena ngoma kadhaa na rapper Ja Rule. 


Wakati huo huo Ashanti yupo katika harakati za kutoa albam yake mpya "BraveHeart" itakayotoka tarehe 30 July akiwashirikisha wasanii kama Meek Mill, french Montana na singer Keyshia Cole.


Tuesday, 11 June 2013

MARIO BALOTELLI AMVISHA PETE DEMU WAKE!

Kupitia akaunti yake ya Instagram, mpenzi wake 'Super' Mario Balotelli, Fanny Negeusha amepost picha ya pete yake ya uchumba aliyovishwa na Balotelli. Pete hiyo inagharimu kiasi cha £100,000/=.


Fanny Negeusha, Belgian model aliandika chini ya picha hiyo kuwa 'It's official!'. Miezi 6 imepita toka uhusiano wao uanze na inasemekana kuwa Balotelli na Fanny wako katika maandalizi ya harusi yao!