Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday, 10 June 2013

KANYE WEST ASHEREHEKEA BIRTHDAY BILA KIM KARDASHIAN

Kanye West ametimiza miaka 36 na kuangusha bonge la party la kimya kimya. Party hili liliwahusisha watu wake karibu tu wakiwemo Beyonce na Jay Z. Nas pia alikuwepo mjengoni. Ila kilichowashangaza watu wengi ni kutoonekana kwa mama kijacho wake, Kim Kardashin. 


Lakini wataalam wa mambo wanasema kuwa Kim K alishindwa kupaa mpaka New York kwavile yupo katika nyakati za majeruhi akikaribia kabisa siku zake za kumleta duniani mtoto wake wa kwanza ambaye tayari madaktari wameshasema kuwa atakuwa mwenye jinsia ya kike! 


Friday, 7 June 2013

NAZIZI AMWANIKA MTOTO WAKE!

Nazizi, rapper toka Kenya wa crew ya Necessary Noise amemwanika mtoto wake wa kiume anaitwa Tafari  huko Nai! Nonini ameonekana akiwa na Tafari muda mwingi na hasa hivi majuzi alipokuwa na katika breakfast show, OneFm. 


Mwaka huu Tafari anatimiza miaka 3 na anaoneka he is just like his mother kwa swaga zake.



Wednesday, 5 June 2013

MR NICE ATEMWA GRANDPA RECORDS, KENYA.

Baada ya kufulia kimuziki achilia mbali maisha, star wa 'Kikulacho' toka nchini Tanzania aliamua kuhamishia shughuli zake za kimuziki nchini Kenya. Na huko Kenya alidaka dili la kusaini mkataba na GrandPa records na kufanikiwa kurekodi ngoma kadhaa. Miezi miwili sasa imeshapita toka alambe mchongo huo lakini hii leo the CEO wa kampuni GrandPa records, Refigah aliitisha press conference na kutangaza kumtema Mr. Nice.


Refigah alieleza sababu za kumwaga Mr. Nice ni pamoja na uzembe wa msanii, kutokuwa mshindani kimuziki na msanii mwenewe kutoheshimu mkataba huku ikisemekana kuwa kumbe Mr. Nice alikuwa na mkataba na record label nyingine huku Tanzania angali amesaini na GrandPa records.





PREZZO AANGUKA AKIPAFOMU STEJINI