Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday, 27 March 2013

D' BANJ AMTWANGA MAKOFI MANAGER WAKE, AMTIMUA KAZI!

Wiki chache zilizopita, aliyekuwa manager wa Koko Master, Dapo Oyebanjo a.k.a D'banj, Abisagboola Oluseun John aka Bankuli alifukuzwa kazi na kichapo juu! Chanzo cha data hii kinasema kuwa mnamo December mwaka jana baada ya show, 'Koko concert', Bankuli alipaa zake kwenda Paris Ufaransa kuipigia promo album mpya ya Kanye West bila kumpa taarifa D'Banj. Koko Master akampa vitasa/makofi na kumtimua kazi right away!
Bankuli alivunja ukimya na alikuwa ana yake ya kusema,"D’Banj hakunifukuza ila ni uamuzi wangu mwenyewe" Bankuli pia alikana kufanya kazi na Kanye West bila ruhusa ya D' Banj!
Inasemekana D'Banj ni msanii mgumu kum-manage. Anaamua atakacho na ni mgumu kufuata ushauri vile kila mtu anayefanya kazi naye, Baba (D’Banj) mwisho wa siku aliamua kusepa zake!
 
D'Banj na Bankuli
 

GAUNI GHALI ZAIDI DUNIANI!

The saying diamonds are a girl’s best friend has been taken to a whole new level as the world's most expensive dress has been unveiled.




 
Bei yake: £11.7m
Designer: Debbie Wingham
 

Monday, 25 March 2013

MWANAMKE MWENYE MIGUU MIREFU ZAIDI DUNIANI!

Ni Svetlana Pankratova. Ni mcheza basketball wa zamani  raia wa Urusi mwenye kimo cha futi 6 na nchi 5 (1.96 m). Miguu yake ina urefu wa futi 4 na nchi 4 (1.32 m)




MTOTO WA MIAKA 8 AOA KIBIBI CHA MIAKA 61!

Dogo wa miaka 8, Sanele Masilela, amefunga ndoa na kibibi cha miaka 61. Dogo huyo ambaye ni mwanafunzi wa Primary school ameushangaza Ulimengu kwa kumuoa ajuza  Helen Shabangu huko Tshwane, South Africa.

Ingawa ndoa hiyo haitambuliki kisheria lakini dogo amekomaa kwa kusema kuwa sasa anajihisi ni mme kamili na ana wajibu kwa ndoa yake akiwa kama mme!

Dogo alifunguka haya katika siku ya ndoa yake na kuwaacha wahudhuriaji wa ndo hiyo vinywa wazi, "Leo ni siku kubwa kwetu (mimi na mke wangu) kama vile nilivyoitarajia. Marafiki zangu walifikiri na wanaona ni vichekesho nilipofunga ndoa hii lakini mimi najiona ni mwenye furaha na kujihisi kama mme kamili sasa"

Bwana Sanele Masilela na Bi. Harusi Helen Shabangu

Bwana na Bi Harusi wakipata chakula cha usiku!













HAIHUU!!

Mwanamuziki wa Marekani Nicki Minaj alinaswa na kamera akiwa nyuma ya gari lake aina ya Maybach akiwa ameuchapa 'fofofo' huku mguu mmoja ukiwa Magharibi na mwingine Mashariki ya mbali!