Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday, 26 January 2013

TIMBERLAKE NA JAY-Z NDANI YA SUIT NA TIE

He is the mastermind behind Rihanna’s 2007 comeback track Umbrella. This time around anamrudisha tena the former ‘N Sync star, Justin Timberlake. He is Shawn Carter a.k.a Jay-Z katika mtoko mpya wa Timberlake, "Suit and Tie"! 

Ijumaa (jana), Jay and Timber walikuwa very busy wakitengeneza video ya ngoma hiyo mpya na one of the very interesting part of that video ni pale Timber anapoonekana ameshikilia mwamvuli mweupe wakati Jay akiitupia mikono yake mifukoni, kama hana habari vile!

Ni matayarisho ya albam mpya ya Timberlake iitwayo 20/20 Experience ambayo rasmi itakuwa sokoni March 19. Stay Tuned!


Timberlake & Jay-Z

Justin Timberlake




Thursday, 24 January 2013

EDEN HAZARD APAMSUA MBAVU MWOKOTA MIPIRA

Ni dakika ya 80 katika mchezo wa marudiano, nusu fainali ya kombe la ligi Capital One, kati ya Swansea na Chelsea. Winga wa Chelsea Eden Hazard,22, anafanya tukio la aibu hasa katika mpira wa miguu kwa kumbutua mwokota mipira na kumsababishia maumivu mbavuni na kuoneshwa kadi nyekundu. Dogo huyo aitwaye Charlie Morgan, 17, ni mtoto wa bosi wa Swansea, Martin Morgan. 

Hazard akiongea na Chelsea Tv baada ya mchezo alisema, "Dogo alilalia mpira na nilitaka kuuchukua mpira na haikuwa dhamira yangu kumdhuru, Niliupiga mpira na sio yeye. Naomba radhi. Dogo alikuja vyumba vya kubadilishia nguo na niliongea naye, aliniomba msamaha nami pia nilimtaka radhi" 

Swansea captain Ashley Williams, aliyekuwa karibu na tukio alisema, ‘Demba Ba alisema alimwona Hazard akimpiga dogo mbavuni. Huwezi fanya vile kwa dogo kama yule"

Chelsea manager Rafael Benitez, amesema kuwa suala hilo litashughulikiwa na klabu na tayari Hazard na dogo walikutana dressing room na kuombana msamaha. Police wa South Wales wanachunguza tukio hilo kwa umakini.


Japo Swansea walilazimishwa suluhu ya 0-0 lakini wamefuzu kwa faida ya magoli 2 ya mchezo wa awali na kuingia fainali Wembley baada ya miaka 100!


Eden Hazard katika purukushani na dogo
Demba Ba akimpoza dogo
Patashika: Captain wa Swansea Ashley Williams (katikati) aliyeshikiliwa akitaka kumzingua Eden Hazard
Red card: Eden Hazard nje
Dogo akiugulia
Dogo akipelekwa hospitali







PETER WA P-SQUARE APATA MTOTO WA PILI!

Hivi majuzi katika hospitali moja huko US of A, Peter Okoye, pacha katika kundi la P-Square alipata mtoto wa kike toka kwa girlfriend wake wa muda mrefu, Lola Omotoya. Peter aliandika katika ukurasa wake wa twitter na kutangaza mtoto wake huyo wa kike ataitwa Aliona.

Peter na Lola sasa wana watoto wawili, wa kwanza wa kiume aitwaye Cameron, 4, na wa pili wa kike Aliona! The family is now 'complete"!

Peter's girlfriend Lola Omotoya na bintiye Aliona

Peter Okoye


Peter na madaktari


Wednesday, 23 January 2013

KUAPISHWA KWA OBAMA PLUS ALL THE FASHION!

Juzi, Barack Hussein Obama aliapishwa kuwa raisi na kuingoza tena USA kwa muhula wa pili na kufuatiwa na tafrija fupi huko Washington DC. Kikubwa ni mitokelezeo ya siku hiyo ambapo The 1st lady herself alionekana kinara kwa kutupia gauni refu jekundu designed by Jason Wu velvet & chiffon halter, miguuni akatupia heels za Jimmy Choo na kidoleni pete ya diamond by Kimberly McDonald.

1st lady Michelle Obama
Obama na mkewe Michelle

Watoto wa Obama, Sasha & Maliah. Malia alitupia amethyst J Crew coat na kuongezea na  tights, ballerina flats, na navy gloves wakati Sasha alivaa lavender coat & dress by Kate Spade. 
Mrs Beyonce Carter aliimba wimbo wa taifa, akiwasili ndani ya Emilio Pucci gown & bright green earrings by jeweler Lorraine Schwartz ndani ya Christian Dior coat  akiwa na mumewe Jay-Z
Obama na Michelle, Jennifer Hudson na Alicia Keys(chini kulia)
Beyonce akiimba National Anthem
Jennifer Hudson
Mke wa makamu wa raisi Joe Biden Jill alitokea bomba pia katika blue silk dress by Vera Wang




Monday, 21 January 2013

LADY GAGA AMSHIKA DANCER WAKE KALIO STEJINI!!

Kabla ya siku ya kuapishwa kwa Rais Barack Obama, kama ilivyokuwa mwaka 2009, wasanii kadha wa kadha wataperform siku hiyo! Mmojawapo ni Lady Gaga, wengine ni Beyonce atayeimba wimbo wa taifa, Stevie Wonder, Alicia Keys, Usher, pamoja na Smokey Robinson!

Macho na masikio ya wengi huko USA yapo kwa this controversial singer anayeonekana kama atarudia madudu yaleyale aliyoyafanya katika show ya tour yake jana Jumapili iitwayo "BornThis Way" ukumbini Staples Center. Gaga wakati akiwa stejini alionekana akimshika dancer wake kalio. Pamoja na tukio hilo vipo vituko vingine kibao. Check these pictures!