Tanzania top model audition
Tanzania top model audition
Wednesday, 29 August 2012
JESUS KUNOGESHA TAMASHA LA USIKU WA SAUTI NA MARAFIKI WA KWELI
Mwezi ujao kiongozi wa zamani wa Diamond Musica aitwaye Kibinda Nkoi aka Ibonga Katumbi 'Jesus' na baadhi ya wanamuziki wengine wa kundi wataungana kwa ajili ya kupagawisha mashabiki watakaojitokeza kwenye onesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa Kweli litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
Akizungumza Dar es Salaam jana mratibu wa tamasha hilo Martin Kadinda ambaye anatamba na brand zake mpya ya ‘Single Button’na 'Vibunduki' alisema onesho hilo linawahusisha wanamuziki wakongwe ambao wataungana na Jesus pamoja na hao wa Diamond, “Kila kitu kinakwenda sawa aliyekuwa amealikwa kwenye onesho hili ni Jesus,lakini kwenye onesho hilo atatakiwa kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo alitamba nazo akiwa Diamond na Beta Musica kwa hali hiyo alishauriwa awaite wenzake ili wamsindikize”
“Kutokana na heshima waliyojengana na wenzake walikubali kumsindikiza kwa hiyo mashabiki wa Kibinda Nkoi baada ya miaka 12 wataweza kuwaona tena Ibonga Katumbi, Richard Mangustino, Wayne Zola Ndonga, na Alain Mulumba Kashama wakisimamia pamoja na kuimba tena nyimbo zao kali” alisema Kadinda
Aliongezea kuwa lengo kubwa la onesho hilo ni kuthamini muziki wa zamani na kufundisha matumizi ya vyombo vya muziki, katika onyesho hilo pia watakuwepo wapiga magita kama Elly Chinyama, Adolph Mbinga, Marcis Mengina na mpiga drum wa mwisho kuipigia Diamond Sound kwa jina la Kata Nyama Serikali.
Tuesday, 28 August 2012
USAILI WA MAISHA PLUS SEASON MPYA WAANZA
Zoezi la kwasaka watu watakaoweza kuingia kwenye shindano la Maisha Plus, imeanza jana (Agosti 27) huko Bagamoyo mkoani Pwani...
Baada ya hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo;
Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu
Usaili utafanyika katika mji wa Bomang’ombe
Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro
Usaili utafanyika Karatu
Agosti 31 – Singida
Usaili utafanyika Singida Mjini
Septemba 1- Iramba
Usaili utafanyika Iramba Mjini
Septemba 2- Dodoma
Usaili utafanyika Kondoa Mjini
Baada ya hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo;
Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu
Usaili utafanyika katika mji wa Bomang’ombe
Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro
Usaili utafanyika Karatu
Agosti 31 – Singida
Usaili utafanyika Singida Mjini
Septemba 1- Iramba
Usaili utafanyika Iramba Mjini
Septemba 2- Dodoma
Usaili utafanyika Kondoa Mjini
Subscribe to:
Posts (Atom)


