Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday, 29 August 2012

KAT DELUNA NEW VIDEO - WANNA SEE U DANCE (LA LA LA)

JESUS KUNOGESHA TAMASHA LA USIKU WA SAUTI NA MARAFIKI WA KWELI


Mwezi ujao kiongozi wa zamani wa Diamond Musica aitwaye Kibinda Nkoi aka Ibonga Katumbi 'Jesus' na  baadhi ya wanamuziki wengine wa kundi wataungana kwa ajili ya kupagawisha mashabiki watakaojitokeza kwenye onesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa Kweli litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.

Akizungumza Dar es Salaam jana mratibu wa tamasha hilo Martin Kadinda ambaye anatamba na brand zake mpya ya ‘Single Button’na 'Vibunduki' alisema onesho hilo linawahusisha wanamuziki wakongwe ambao wataungana na Jesus pamoja na hao wa Diamond, “Kila kitu kinakwenda sawa aliyekuwa amealikwa kwenye onesho hili ni Jesus,lakini kwenye onesho hilo atatakiwa kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo alitamba nazo akiwa Diamond na Beta Musica kwa hali hiyo alishauriwa awaite wenzake ili wamsindikize”

“Kutokana na heshima waliyojengana na wenzake walikubali kumsindikiza kwa hiyo mashabiki wa Kibinda Nkoi baada ya miaka 12 wataweza kuwaona tena Ibonga Katumbi, Richard Mangustino, Wayne Zola Ndonga, na Alain Mulumba Kashama wakisimamia pamoja na kuimba tena nyimbo zao kali” alisema Kadinda


Aliongezea kuwa lengo kubwa la onesho hilo ni kuthamini muziki wa zamani na kufundisha matumizi ya vyombo vya muziki, katika onyesho hilo pia watakuwepo wapiga magita kama Elly Chinyama, Adolph Mbinga, Marcis Mengina na  mpiga drum wa mwisho kuipigia Diamond Sound kwa jina la Kata Nyama Serikali.

   

Tuesday, 28 August 2012

USAILI WA MAISHA PLUS SEASON MPYA WAANZA

Zoezi la kwasaka watu watakaoweza kuingia kwenye shindano la Maisha Plus, imeanza jana (Agosti 27) huko Bagamoyo mkoani Pwani...

Baada ya hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo;
Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu
Usaili utafanyika katika mji wa Bomang’ombe

Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro
Usaili utafanyika Karatu

Agosti 31 – Singida
Usaili utafanyika Singida Mjini

Septemba 1- Iramba
Usaili utafanyika Iramba Mjini

Septemba 2- Dodoma
Usaili utafanyika Kondoa Mjini

Monday, 27 August 2012

P SQUARE WAKIWA NA RICK ROSS UK KWENYE AFROBEAT FESTIVAL

KANYE AMFANYA KIM K KUBADILI NGUO ZAKE ZOTE


Kanye West anamtaka mpenzi wake Kim Kardashian avae mavazi ya heshima na ya kuvutia.


Katika kipindi cha jana cha Keeping Up With the Kardashians, rapper na mbunifu huyo wa mavazi, 35 – ameweka deal na mpenzi wake huyo wa miezi mitano kuwa kama atazitupa nguo zake zote atamnunulia zingine.