Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday, 17 August 2012

KEKO KUKINUKISHA JIJINI MWANZA WEEKEND HII

 
 
Rapper wa kike toka nchini Uganda, Keko anatarajiwa kupiga show weekend hii jijini Mwanza.
 
Taarifa hiyo ameitoa mwenyewe kupitia Twitter account yake.

“TANZANIA ARE YOU READY!!! #KEKONIANS IN MWANZA #MAKEYOUDANCE COMING TO YOU THIS WEEKEND tell every & anyone KEKO Coming!!”

Hata hivyo mpaka sasa haijawa wazi ni nani anayempeleka jijini humo ama show itafanyika wapi kwakuwa hakuna matangazo yaliyotolewa.

THE MAKING OF BAADAE-OMMY DIMPOZ

KOFFI OLOMIDE ATUPWA JELA MIAKA MITATU


Stori kutoka Kinshasa Congo DRC zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki maarufu ambae jina lake lina uzito ndani na nje ya Afrika, Koffi Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu au kulipa faini.
Kilichomfanya star huyu wa rhumba mwenye miaka 56 apigwe nyundo hizo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake kwa jina la Diego Lubaki.
Nimemsikia mwandishi wa DW kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi ya mawakili 15 ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani kusikiliza kitatokea nini kwenye kesi yake August 16, 2012.Kabla ya kufikishwa Mahakamani Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni muda mfupi tu baada ya kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya mahakama ndogo Kinshasa kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni pamoja na kumpiga meneja wake ambae amekua akiishi Ulaya.
Mwandishi wa DW amesema ugomvi huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro elfu sita ambapo mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi alimpiga ngumi meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.
Hata hivyo meneja huyo aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka yake dhidi ya Koffi na kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao lakini majaji walilipiga chini hilo ombi lake.
Baadhi ya wananchi waliotoa maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono adhabu hiyo na kusema amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye, mwingine amesema ni safi kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye kutenda kosa.
Kutokana na adhabu hiyo kiongozi wa mawakili wanaomtetea Koffi amesema wamepanga kukata rufaa lakini wanasubiri maoni ya Koffi mwenyewe.…

Thursday, 16 August 2012

ALLY REHMTULLAH KUZINDUA DESIGNS ZAKE TAREHE 8 SEPTEMBER 2012

 
 
MWANAMITINDO  maarufu nchini, Ally Rehmtullah pichani juu atazindua onyesho rasmi la kazi zake mpya  za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanawake na wanaume ‘Ally Rehmtullah 2013 Collection’lililopangwa kufanyika Hoteli ya Serena,  jijini Dar es Salaam, Septemba 8 2012.
  Rehmtullah alisema dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati za kuinua kiwango cha kazi za mitindo kwa Tanzania.
“Nimepania kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini,  ili kazi za wanamtindo na wabunifu ziweze kupenya kwenye soko la ndani na la Afrika Mashariki na ya kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki,’ alisema.
Pia aliongeza kuwa, kwenye uzinduzi huo mavazi na onyesho litapambwa kwa rangi nyeupe, ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa mwafrika.
Aidha, Rehmtullah alisema licha ya kuonesha mavazi pia kutakua na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nyota, ambapo pia aliwataja wadhamini wakuu wa onyesho hilo kuwa, Mercedez Benz, Mo Blog, Belvedere Vodka, Dulux, Raha, Hugo Domingo,The Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Missie Popular Blog, Quality Furniture na Mx Carter.
Katika onesho hilo, linatarajia kudhuriwa na watu 400, wakiwemo viongozi wa serikali, wafanyabiashara na wageni mbalimbali  ambapo watashuhudia wanamitindo wengine mahili na chipukizi watakaoonesha mitindo siku hiyo.

WAREMBO WA REDDS MISS ILALA WATAMBULISHWA LEO





Mratibu wa Shindano la Redd's Miss Ilala 2012, Gadner G. Habash akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge mchana huu wakati wa kutambulisha warembo watakaoshiriki kwenye fainali ya Redd's Miss Ilala 2012. Washindi watafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012.Wengine Pichani toka Kulia ni Mratibu Mwenza wa Shindano hilo,Juma Mabakila, Cylivia Mashuda na Neema Mbula ambao ni walimu wa warembo hao.







Baadhi ya warembo watakaoshiriki Shindano la Redd's Miss Ilala wakiwa kwenye kikao hicho.