Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday 4 September 2012

NEY AWAVAA KWEUPE WEMA SEPETU NA AUNTY EZEKIEL HUKO MWANZA


Chezea Ney Wa Mitego uone. 
Baada ya kuwachana kina P Funk aka Majani, Zay B, Sister , Dudu Baya na wengine kwenye songi lake la "Itafahamika", now Ney wa Mitego kahamia kwa mademu wa Bongo movie. 
Baada ya wimbo wake wa "Nasema Nao" kuzua utata mwingi kwa kuimba mistari inayowaponda mademu toka kwenye tasnia ya filamu nchini, hivi majuzi  jamaa ameonesha kutomwogopa yeyote baada ya kuwataja live live Wema Sepetu na Aunty Ezekiel kwamba ni makahaba. 
Tukio hilo lilitokea weekend iliyopita kwenye tamasha la Fiesta huko Mwanza ambapo kwenye kipande cha wimbo wake kinachosema makahaba wengi wapo bongo movie, alibadilisha kwa kusema "Makahaba wengi wapo bongo movie kama Wema Sepetu na Aunty Ezekiel", kitendo hicho kilimfanya Wema Sepetu alie sana kiasi cha hata kushindwa kupanda kwenye jukwaa la Fiesta mkoani Mwanza. Kwa upande wa Aunt Ezekiel ilifikia wakati mpaka akataka kumrushia ngumi msanii wa songi hilo. 
Ney alipoulizwa kuhusiana na kitendo hicho cha kutaja majina ya watu kweupe unajua alichojibu, "Sijakosea kusema vile nilimaanisha kabisa kweli hawa watu matendo yao yanaendana na ukahaba". 

Wema (kushoto) akiwa na Aunty Ezekiel (kulia)

No comments:

Post a Comment