Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday 8 August 2012

NONINI AHAMIA KWENYE UTANGAZAJI WA REDIO


Habari ni kwamba Kenyan Rapper/Singer amechukua nafasi ya Tina Kaggia katika kipindi cha asubuhi, yaani 'Breakfast Show' katika kituo cha radio cha 1FM. Nonini sasa atatangaza kipindi hicho na Marcus Olang' ambapo Tina Kaggia amehamia katika kipindi kingine katika radio hiyo.
       Wengine wanaweza kudhani Nonini ni mpya katika utangazaji wa Radio lakini aliwahi kufanya kazi kama Celebrity Radio Presenter katika kituo cha Radio cha YFM, ambayo kwa sasa inafahamika kama HOT 96.
       Nonini ni msanii aliyeshinda tuzo nyingi toka atoke kimuziki mwaka 2000 kutoka studio za Calif (Calif Records). Nonini ni mmoja wa wasanii waliotunga aina ya muziki wa Genge na sasa hivi anatambulika na Jamii ya Haki Miliki ya Muziki nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment