Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Sunday, 24 November 2013

MFANYAKAZI WA GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL ASHEREKEA BIRTHDAY NA WASHIRIKI WA TANZANIA TOP MODEL 2013

 Mfanyakazi wa Hotel ya Giraffe Ocean View jioni ya jana alisherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa kazini kwake,wafanyakazi wenzake na washiriki wa shindano la Tanzania Top model 2013 walijumuika kuila keki ya Birthday,Glady anasherekea kufikisha miaka 40.
(Rose akimlisha keki Gladys Msia kama picha inavyozungumza).
 Gladys akilishwa keki na Bi. Hellen.
 Gladys akiwa na wafanyakazi wenzake Hellen,Martha Mkololo na Gladys kwenye picha ya pamoja.
Mambo ya ku-pop campaign yaliendelea.Thomas Fusi akifungua campaign kimadaha.
 Hapa wimbo wa Hapy birthay to you ukiimbwa....
 Washiriki wa Tanzania Top Model wakishiriki birthday ya Gladys.

MAZOEZI YA WASHIRIKI TANZANIA TOP MODEL YAZIDI KUNOGA

Thursday, 21 November 2013

PETER P-SQUARE AMTETEA MKEWE!

Baada ya kutohudhuria kwa Jude Okoye katika harusi ya mdogo wake Peter P-Square, kumetokea maneno mengi kuwa mke huyo wa Peter hajatulia(kicheche). Lakini baada ya kufunga ndoa hiyo ya kimila siku ya Jumapili tarehe 17, Oktoba, Peter mwenyewe ameibuka na kumtete mkewe, Lola Omotoya!
 
Lola Omotoya


"Nina furaha sana leo kwasababu ninaungana na kuwa mwili mmoja na mwanamke ninayempenda. Ni mwanamke mkakamavu/shupavu na yupo na mimi nyakati zote. Ninaamini ataniletea furaha", Peter P-Square.

Peter, Lola, Genevive Nnaji na mastaa wengine


Wednesday, 20 November 2013

WASHIRIKI WA TANZANIA TOP MODEL KUPIGA KAMBI GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL

 Mkurugenzi Tanzania Top model Ysufu George akiongea na wanahabari kuhusu ujio wa kuweka kambi ya siku 17 ya wanamitindo hao katika Hoteli ya Giraffe ocean view iliyomo Frikana jijini Dar.
 Wanamitindo wakiwasili leo mapema Giraffe Ocean View Hotel wakitokea Tamar Hotel walikokuwa wameweka kambi ya siku mbili baada ya kutokea hotel ja Jb Bekmont.
Giraffe ocean View Hotel ,hoteli yenye hadhi ya nyota nne,karibu Giraffe upate huduma zilizo sawa na thamani ya pesa zako,inasifika kwa ukarimu uliopita kiwango.

TANZANIA TOP MODEL WAFUNGUA RASMI ZOEZI LA UPIGAJI KURA KWA WASHIRIKI

  Mkurugenzi wa shindano la Tanzania Top Model 2013 Bw. Jackson Kalikumtima akitangaza rasmi namba ya kupiga kura ili kumchagua mshiriki umpendae kushinda taji la Princess of Tanzania.
  Bwana Kalikumtima aliyasema hayo keo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanika katika hoteli ya Tamar iliyopo mwenge jijini Dar.
Namba iliyotangazwa ni 15564 ikiwa ni namba maalumu unatuma ujumbe mfupi wa maneno Mfano :  TM Nyanjige kwenda 15564 hapo utakuwa umemwezesha mshiriki umpendae kushinda taji. hilo.
 Baadhi ya vionjo vya vipindi vya televisheni vitakavyoruka Clouds Tv kila siku kuanzia leo usiku saa tatu hadi siku ya fainali vilioneshwa kwa waandishi wa habari hii leo
 Huu ndiyo mfumo mpya wa kumchagua mshiriki umpendae.
 Washiriki wa Tanzania Top model wakiwa katika mkutano na waandishi wa Habari hii leo.