Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday, 21 November 2013

PETER P-SQUARE AMTETEA MKEWE!

Baada ya kutohudhuria kwa Jude Okoye katika harusi ya mdogo wake Peter P-Square, kumetokea maneno mengi kuwa mke huyo wa Peter hajatulia(kicheche). Lakini baada ya kufunga ndoa hiyo ya kimila siku ya Jumapili tarehe 17, Oktoba, Peter mwenyewe ameibuka na kumtete mkewe, Lola Omotoya!
 
Lola Omotoya


"Nina furaha sana leo kwasababu ninaungana na kuwa mwili mmoja na mwanamke ninayempenda. Ni mwanamke mkakamavu/shupavu na yupo na mimi nyakati zote. Ninaamini ataniletea furaha", Peter P-Square.

Peter, Lola, Genevive Nnaji na mastaa wengine


Wednesday, 20 November 2013

WASHIRIKI WA TANZANIA TOP MODEL KUPIGA KAMBI GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL

 Mkurugenzi Tanzania Top model Ysufu George akiongea na wanahabari kuhusu ujio wa kuweka kambi ya siku 17 ya wanamitindo hao katika Hoteli ya Giraffe ocean view iliyomo Frikana jijini Dar.
 Wanamitindo wakiwasili leo mapema Giraffe Ocean View Hotel wakitokea Tamar Hotel walikokuwa wameweka kambi ya siku mbili baada ya kutokea hotel ja Jb Bekmont.
Giraffe ocean View Hotel ,hoteli yenye hadhi ya nyota nne,karibu Giraffe upate huduma zilizo sawa na thamani ya pesa zako,inasifika kwa ukarimu uliopita kiwango.

TANZANIA TOP MODEL WAFUNGUA RASMI ZOEZI LA UPIGAJI KURA KWA WASHIRIKI

  Mkurugenzi wa shindano la Tanzania Top Model 2013 Bw. Jackson Kalikumtima akitangaza rasmi namba ya kupiga kura ili kumchagua mshiriki umpendae kushinda taji la Princess of Tanzania.
  Bwana Kalikumtima aliyasema hayo keo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanika katika hoteli ya Tamar iliyopo mwenge jijini Dar.
Namba iliyotangazwa ni 15564 ikiwa ni namba maalumu unatuma ujumbe mfupi wa maneno Mfano :  TM Nyanjige kwenda 15564 hapo utakuwa umemwezesha mshiriki umpendae kushinda taji. hilo.
 Baadhi ya vionjo vya vipindi vya televisheni vitakavyoruka Clouds Tv kila siku kuanzia leo usiku saa tatu hadi siku ya fainali vilioneshwa kwa waandishi wa habari hii leo
 Huu ndiyo mfumo mpya wa kumchagua mshiriki umpendae.
 Washiriki wa Tanzania Top model wakiwa katika mkutano na waandishi wa Habari hii leo.

MPIGIE KURA MSIRIKI UMPENDAE: TANZANIA TO MODEL 2013


 Mpigie kura mshiriki umpendae kwenda namba 15564.

Sunday, 17 November 2013

WASHIRIKI WA TANZANIA TOP MODEL WAANZA KUFUNDISHWA DANSI LEO

 Mwalimu wa dansi 'bad spencer' akitoa mafunzo kwa washiriki wa Tanzania Top Model 2013,mazoezi haya yameanza jioni ya leo na yataendelea kwa wiki tatu zijazo,dansi ya ufunguzi ni kitu muhimu kwa mashindano ya mitindo na urembo.
WAshiriki wakijaribu kumfatilia kwa vitendo mwalimu wao ambapo steps zilikuwa ngumu kidogo ila modoz wanajitaidi kumudu japo ilikuwa ni siku ya kwanza.
Ni step kwa step sambamba na mwalimu haina kupoteza point.
   Mwendo sebene sasa....watu weweeeeee..!!
mmmmh usiniguse mie..!!
 
 Mwalimu Bad spencer akitoa maelezo kwa kina washiriki wa Tanzania Top Model 2013 jinsi ya kutumia viungo vya mwili kutengeneza umbile la kitu kingine.
 
 
 
 
 
 
 
 Matroni'Zakia' akiwa amepozi kwa kiti.