Friday, 31 August 2012
Thursday, 30 August 2012
MSINIITE MZEE MAGARI.
Nyota kwenye tasnia ya filamu nchini Charles Magari amekataa kuitwa
mzee while age yake imeshasogea.
Hali hiyo ilitokea hivi karibuni baada ya wasanii chipukizi kumpa
jina la 'mzee' kutokana na ushauri wake anaowapa wasanii hao kwenye tasnia hiyo.
"Mimi sitaki kabisa kusikia mtu ananiita mzee wakati ni kijana, nashangaa kila nikipita mitaani naitwa mzee waambieni na wengine silitaki jina hilo”, Mzee
Pia mzee Magari alisema kuwa yupo mbioni kuzindua filamu yake inayoitwa "Zig Zag" iliyoandaliwa na Pilipili Entertainment, mbapo ndani yake kutakuwepo na vichwa kama Haji Adam na Mohamed Fungafunga.
MWAKA WA SHETANI KWA MAY D, YOU TUBE ACCOUNT YAKE YAFUTWA
We all know that May D hivi sasa hayupo tena chini ya label ya Square Records, leboiliyokuwa isimamia kazi zake hadi hivi majuzi alipotimuliwa.
Kwa upande mwingine inashtusha kusikia kuwa official YouTube channel ya singer huyu liyokuwa ikisimamiwa na Iroko Partners imefutwa siku mbili zilizopita pamoja na video zake za "Soundtrack" na "Ile Ijo".
Pamoja na videos za nyimbo hizo, page nyingine zilizotolewa ni pamoja na streams za still clips.
Square
Records’ Youtube accounts pia zinasimamiwa na Iroko Partners.
Hadi sasa haijawekwa wazi iwapo ni Square Records, Iroko au hata
May D mwenyewe aliyeamua kuifuta account hiyo.
Infoz za kuaminika zinadai kuwa hadi sasa hakuna e-mail hata moja iliyotumwa kwa Iroko na pia Square records kuulizia issue imeibiwa.
Kwenye recent interviews Psquare waliweka wazi kuwa kuondoka kwa May D kwenye label hiyo kutamfanya kuwa na ya kujibu kiuongozi zaidi.
GADNER HUYO TIMES FM ATAKUWA AKITANGAZA SHOW IITWAYO MASKANI
Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM katika kipindi cha
Jahazi, Garder G Habash aka Captein anatarajia kuanza kutangaza tena Jumatatu
ijayo kupitia kituo cha radio cha Times FM 100.5 cha Dar es Salaam kwenye kipindi cha .
"Maskani" kitakachokuwa kikiruka from Jumatatu to Ijumaa saa 10
jioni hadi saa 1 usiku.
Rumors dong the rounds ni kuwa mtangazaji huyo atakuwa akilipwa shilingi milioni 5 kwa mwezi na kama tetesi hizi zitakuwa ni za kweli basi Gadner atakuwa the most paid radio personality in Tezee.
Gadner akiongea machache baada ya kutambulishwa Times FM |
Kipindi chake kinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na
kipindi chake cha zamani, Jahazi cha
Clouds FM ambacho kwa sasa huendeshwa na Arnord Kayanda, Wasiwasi Mwabulambo na
Ephraim Kibonde.
Hata hivyo Clouds FM watakuwa na advantage katika mikoa
mingine ambayo Times FM haisikiki.
Picha ya pamoja ya baadhi ya watangazaji wa Times FM.
Kutoka kushoto ni: Gadner, Schola, Natasha, Ndimbo, Dida na Joet.
|
MAANDALIZI YA SEND OFF YA AUNTY EZEKIEL UTATA MTUPU
Zimepita week kadhaa toka kikao cha Aunty Ezekiel kifanyike nyumbani kwake pamoja na Wajumbe wenzake wa tasnia ya filamu hapa nchini inayofahamika kama Bongowood.
Kikao hiki cha Aunty Ezekiel kimezua utata baada ya kila mjumbe kutoa ahadi katika kikao cha kwanza na kutokufika katika kikao cha pili hii iliwashangaza watu wengi sana hasa ndugu na marafiki mbalimbali waliofika katika kikao hicho.
Asilimia nyingi ambao waliotoa ahadi ni wasanii wenzake na inasemekana kwamba muhusika wa maandalizi haya ya send off yuko ziarani. Je huu si utata?.
MJENGO MPYA WA MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATARE
Muonekano wa mbele wa hekalu la Mchungaji Rwakatare
MC na mchungaji Haris Kapiga wa Clouds FM
Mc Harris Kapiga akiwa kazini.
Watu wakijiachia
Kabati la vyombo
Akiwa katika ofisi yake ya nyumbani, kuna sehemu ya kufanyia mikutano, Salon, Studio, na sehemu ya mazoezi.
Wadau wakijiachia kwenye moja wapo ya kochi la kifahari mjengoni humo
Wakati wa msosi
Mambo ya dressing table
Kitanda chake cha kulalia
---
Mchungaji Getrude Rwakatare amehamia rasmi katika nyumba yake mpya iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pembezoni mwa bahari ya Hindi. Inaripotiwa kuwa waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika mahali hapo kwa kushuhudia nyumba yake hiyo ya kifahari.
Kabla ya kuhamia kwenye hekalu lake jipya Mch. Mh. Getrude Pangalile Rwakatare alikuwa akiishi Mikocheni B katika nyumba nyingine ya kifahari pia.
Images via Ruma Africa
Wednesday, 29 August 2012
MARTIN KADINDA KWENDA KU-SHOWCASE DESIGNS ZAKE MAREKANI KWENYE AFRICA NEW YORK FASHION WEEK
Hard work pays.
Baada ya kufanikiwa kuwateka fashionistas wa Bongo kwa designs zake za Single Button na Vibunduki now Martin Kadinda is going to places baada ya kupata mwaliko wa kwenda kuonyesha brand zake huko New York kwenye Africa New York Fashion Week itakayofanyika August 31 mwaka huu.
"Kwa
mara ya Kwanza Maishani mwangu nitakanyaga Ardhi ya Marekani Ijumaa
hii, nitakuwa the only Designer Mwalikwa katika Africa New York
fashion...... Kivumbi collection itaonekana tena ndani ya New York..
kivumbi collection Hiyoooo.. single button hizooo and Ofcourse Vibunduki
teheheteetehehehhe"-said Martin Kadinda.
JESUS KUNOGESHA TAMASHA LA USIKU WA SAUTI NA MARAFIKI WA KWELI
Mwezi ujao kiongozi wa zamani wa Diamond Musica aitwaye Kibinda Nkoi aka Ibonga Katumbi 'Jesus' na baadhi ya wanamuziki wengine wa kundi wataungana kwa ajili ya kupagawisha mashabiki watakaojitokeza kwenye onesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa Kweli litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
Akizungumza Dar es Salaam jana mratibu wa tamasha hilo Martin Kadinda ambaye anatamba na brand zake mpya ya ‘Single Button’na 'Vibunduki' alisema onesho hilo linawahusisha wanamuziki wakongwe ambao wataungana na Jesus pamoja na hao wa Diamond, “Kila kitu kinakwenda sawa aliyekuwa amealikwa kwenye onesho hili ni Jesus,lakini kwenye onesho hilo atatakiwa kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo alitamba nazo akiwa Diamond na Beta Musica kwa hali hiyo alishauriwa awaite wenzake ili wamsindikize”
“Kutokana na heshima waliyojengana na wenzake walikubali kumsindikiza kwa hiyo mashabiki wa Kibinda Nkoi baada ya miaka 12 wataweza kuwaona tena Ibonga Katumbi, Richard Mangustino, Wayne Zola Ndonga, na Alain Mulumba Kashama wakisimamia pamoja na kuimba tena nyimbo zao kali” alisema Kadinda
Aliongezea kuwa lengo kubwa la onesho hilo ni kuthamini muziki wa zamani na kufundisha matumizi ya vyombo vya muziki, katika onyesho hilo pia watakuwepo wapiga magita kama Elly Chinyama, Adolph Mbinga, Marcis Mengina na mpiga drum wa mwisho kuipigia Diamond Sound kwa jina la Kata Nyama Serikali.
Tuesday, 28 August 2012
USAILI WA MAISHA PLUS SEASON MPYA WAANZA
Zoezi la kwasaka watu watakaoweza kuingia kwenye shindano la Maisha Plus, imeanza jana (Agosti 27) huko Bagamoyo mkoani Pwani...
Baada ya hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo;
Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu
Usaili utafanyika katika mji wa Bomang’ombe
Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro
Usaili utafanyika Karatu
Agosti 31 – Singida
Usaili utafanyika Singida Mjini
Septemba 1- Iramba
Usaili utafanyika Iramba Mjini
Septemba 2- Dodoma
Usaili utafanyika Kondoa Mjini
Baada ya hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo;
Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu
Usaili utafanyika katika mji wa Bomang’ombe
Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro
Usaili utafanyika Karatu
Agosti 31 – Singida
Usaili utafanyika Singida Mjini
Septemba 1- Iramba
Usaili utafanyika Iramba Mjini
Septemba 2- Dodoma
Usaili utafanyika Kondoa Mjini
Monday, 27 August 2012
KANYE AMFANYA KIM K KUBADILI NGUO ZAKE ZOTE
Kanye West anamtaka mpenzi wake Kim Kardashian avae mavazi ya heshima na ya kuvutia.
Katika kipindi cha jana cha Keeping Up With the Kardashians,
rapper na mbunifu huyo wa mavazi, 35 – ameweka deal na mpenzi wake huyo wa
miezi mitano kuwa kama atazitupa nguo zake zote atamnunulia zingine.
BBC DIRA YA DUNIA KURUKA LIVE LEO KWENYE TV
Saleem Kikeke |
Matangazo ya televisheni ya Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili
ya BBC leo yanaanza kuruka rasmi kupitia Star TV ya Tanzania na Qtv ya Kenya.
Wiki iliyopita kulifanyika uzinduzi wa matangazo hayo jijini Dar es Salaam.
Matangazo hayo ya Dira ya Dunia kwa upande wa radio ni maarufu
zaidi pengine kuliko matangazo yote ya radio za kimataifa zinazotangaza
Kiswahili duniani.
Kuingia kwenye matangazo ya runinga kwa BBC Swahili kunafungua
ukurasa mpya wa matangazo ya aina hiyo ya Kiswahili nchini.
BBC Dira ya Dunia siku za usoni itakuwa ikishindana na matangazo mengine
ya Kiswahili ya Al-Jazeera ambayo yapo kwenye mchakato wa kuanzishwa.
CHIWAWA WA KENYA AZINDUA MAJI YAKE
Rapper wa Kenya aliyewahi kutamba na ngoma kali iitwayo ‘Mnafeel
aje’, Chiwawa amezindua maji yake ya kunywa.
Maji hayo yanaitwa Minerva jina la kigiriki la mungu wa
busara aliyekuwa akihusishwa na maji katika sehemu ya story zake.
Kwa upande wa Tanzania, Lady Jaydee aliwahi kujaribu
kuanzisha maji yake lakini hata hivyo hayakuendelea kutolewa kutokana na sababu
ambazo hazikuwekwa wazi.
SINTA APIMA NGOMA
"zoom ,,,,, tena zoom halafu hii ndio habari ya blue monday"
"Sisemi nao eeh,sisemi nao wanao comment mbofu mbofu kuhusu
jlo,,
Waganda hapa wangesema nakowaaaaa, maana mtoto wa watu sili
silali sihemi
sina la kusema zaidi, mimi huwa ninafanya vitendo tu,, Je
wewe umepima? au kazi kushadadia ya watu,,, haya zueni balaa lengine hili naona
mmeloana na macho yamewatoka kama fundi saa akiangalia mishale kama iko sawa.
Kama nawaona mlivyokuwa na hasira n comment lolest."
MDOGO WAKE KANUMBA ARITHI MIKOBA YA KAKA YAKE
Ni miezi kadhaa imepita sasa tangu kifo cha one of the best actor ever in Tzee film industry kwa jina la Steven Kanumba kitokee. Na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kusema kampuni ya Kanumba The Great itakuwa inafanya kazi chini ya usimamizi wa Seth Bosco na Abela au Mrs Bile ambae ni dada yake na Marehemu Steven Kanumba ambae Kanumba ndio alikua anamfata kwa kuzaliwa.
Latest infoz nikuwa company hiyo imeshakamilisha movie mpya kwa jina la “Malaika” ikiwa imeshirikisha wasanii km Rose Ndauka, Abdalah Mkumbila, Seth Bosco na Kijana Rammy Galis ambaye anatarajiwa kuwa Kanumba part 2 kutokana na muonekano wake kufanana na The late Steven Kanumba.
Filamu hii inatarajiwa kuwaburudisha mashabiki wa Kanumba na itasambazwa na Steps Entertainment LTD , kaa mkao wa kula kijipatia Copy yako pindi itapokuwa madukani.
Friday, 24 August 2012
R.I.P MATONYA
Yule ombamba maarufu kuliko wote nchini , Matonya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
“Namtaarifu Komredi Yusufu Makamba, kuwa yule kiboko yake
'MATONYA' amefariki usiku wa kuamkia leo kijijini kwakwe Mpamantwa wilaya ya
Bahi, mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni kijijini hapo. Habari ziwafikie,
Mkuu wa Wilaya Betty Mkwasa, Familia ya Mzee Makamba popote walipo, wakazi wa
Dar na Moro pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote. Bila ya kusahau wale wa
eneo la Darajani Mjini Morogoro", ameandika mwandishi wa habari Habel Chidawali
ambaye amewahi kumfanyia mahojiano ombamba huyo.
Matonya amefariki akiwa anaishi kwenye nyumba ya tembe
ambayo ni mali ya mtoto wake wa kike
aitwaye Elizabeth Matonya.
Nyumba hiyo ya asili ya watu wa Dodoma ipo kwenye Kijiji cha
Bahi Sokoni katika Kitongoji cha Nghungugu, umbali wa kilomita 3 kutoka yalipo
makao makuu ya wilaya ya Bahi.
Katika mahojiano aliyofanya na Habel, Matonya enzi za uhai wake
alisema kuwa hana mali yoyote kama wengi walivyokuwa wanadhani.
“Watu wanasema kuwa nina mali, lakini ni ‘walambi’
(akimaanisha kwamba ni waongo). Mimi sina kabisa mali; hata mbuzi; hata kuku
sina na wala sina mpango wa kununua tena hata kama nina pesa kwa kuwa
walishazoea kuniibia, hivyo sitaki tena kuwa na mali.”
Nilikuwa na ng’ombe wengi sana. Kila wakati walikuwa
wakiwaiba wakati ninaishi Kilimatinde na ng’ombe hao nilinunua kwa pesa yangu
ya kuomba huko Dar es Salaam. Walikuwa wengi lakini waliibwa wote na ndugu
zangu.
Kuhusu kuacha kuomba
Jibu: Labla serikali inijengee nyumba nzuri hapa na inipe
mtu wa kunitunza au hata wakijenga nyumba nzuri kwa mtoto wangu halafu
wanisaidie na chakula pamoja na chai ya kila siku, mimi naweza kustaafu kazi
yangu lakini bila ya kufanya hivyo kazi yangu nitakufa nayo.
Katika mahojiano hayo Matonya alisema alikuwa akipata kati
ya Sh50,000 hadi 100,000 kwa mwezi na mara nyingi alikuwa akirudi kijijini kila
baada ya miezi miwili au mitatu tangu alipoanz`a kazi hiyo mwaka 1961.
Rest in Peace Matonya.
ANA PETER WA EA RADIO AJA NA WIMBO WA " A CALL"
Mtangazaji wa show ya Power Jams ya East Africa Radio, Ana Peter ameachia ngoma mpya yenye mahadhi ya reggae iitwayo "A call".
Ngoma hii imetengenezwa na DX wa Arusha kwa kutumia beat ya riddim ya "heart &
soul riddim".
"Nimeimba kuhusu kufata ndoto zetu katika maisha,kuondokana na
dhana potofu kuwa maisha yana formula fulani.Shule ni muhimu sana katika
kuturahisishia maamuzi maishani,Pasipo uelewa na maarifa,Maisha huonekana
magumu zaidi,Matumizi ya vilevi kupita kipimo ama hata kujihusisha na utumiaji
wa madawa ya kulevya yote ni matokeo ya kupuuza malengo endelevu na kufata
mikumbo, anasema Ana.
BEN POL NEW SINGLE-PETE
Pete ni wimbo wa kwanza
wa Ben Pol tangu aachie albam yake iitwayo Maboma akiwa chini ya MLab.
Kwa maana nyingine ni kuwa huu ndio wimbo mpya aliorekodi akiwa nje ya
label ya MLAB.
"Thank God it's been a great journey and I
personally feel the singles of that album were great. I have now come with a
new production team and heading for my second album. Share it and I hope you
enjoy this record as much as I enjoyed recording it. Peace and much love," ameandika Ben kwenye maelezo yake.
Wimbo huu umendikwa na waandishi watatu akiwemo yeye mwenyewe Ben Pol, Fred
Max na Lady Peace Winnie.. Producer ni Mona
Gangsta wa Classic Sounds.
Mashairi
Verse 1;
Hadithi ya penzi langu umenikata nini mwisho
huthamini huoni pendo lako nalihitaji leo kesho
nishawahi kukosa
,mwenzenu nilisumbuka
mchana na usiku mimi,
nishawahi kukosa
nasema niliteseka mchana na usiku mimi
nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
mchana na usiku mimi,
sitaki tena kosa
najua nitateseka
mwisho sitokuwa nawe tena naulizaa
Chorus;
Kama pete yangu, inakuchomaa kidoleni
ni kama pendo langu , linakuchoma moyonii ,
bora kuitoa aaah aah ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
bora kuitoa aaah aa ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
Verse 2;
sikujali wambea
wanafki walosema
hatutadumu mimi nawe tutajaachana
wakiniona siko nawe si ndo watasema
hata nyumbani watajua tumefarakana
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
kila jema n'tendalo mie ,kwako limekuwa sio
nitakapo kujua ulipo ,wanijibu utakavyo
pete kidoleni mwako ,yanisuta mwenzio
ndo maana nikukosapo ,moyo wanienda mbio
Thursday, 23 August 2012
EXCLUSIVE: K LYNN IS PREGIOUS
Mama kijacho |
List ya baby boom kwenye Miss Tanzania inataongeza siku si nyingi.
Baada ya Hoyce Temu, Nagris Mohammed, Miriam Gerald, Silvia Shally na Nancy Sumari ambao waliwahi kuwa mamiss Tezee kumuongezea Uncle Lundenga cheo cha U-uncle baada ya kujaliwa watoto, latest news ni kwamba Jacquline Ntuyabaliwe better known as K Lynn naye yuko mbioni kuongeza mjomba mwingine coz she's now eating for two.
Habari za uhakiaka zinadai kuwa jamaa mwenye makampuni MEEENGI hapa nchini ndiye aliefanikisha zoezi hilo.
MB DOGG KWENYE MOVIE
Filamu kali na ya kusisimua ya Nankonda wa Mikindani inayotarajia
kuingia sokoni hivi karibuni ndio itakayokuwa filamu ya kwanza
kumtambulisha msanii wa Bongo fleva kwa jina la Mbwana Mohamed
aka ‘Mb Dogg’ kuingia katika tasnia ya filamu.
Filamu hiyo ambayo Mb Dogg amacheza kama mhusika mkuu imetayarishwa na Dr. Cool Production company.
“Uwezo alionyesha Mb Dogg ni wa hali ya juu sana, utafikiri alikuwepo katika tasnia ya uigizaji kwa miaka mingi , msanii amebeba uhusika kulingana na hadithi yenyewe nasema ni msanii anayejua kuigiza na hilo mtalismtalishuhudia katika filamu hiyo,” said Mzee Korongo.
Filamu hiyo ambayo Mb Dogg amacheza kama mhusika mkuu imetayarishwa na Dr. Cool Production company.
“Uwezo alionyesha Mb Dogg ni wa hali ya juu sana, utafikiri alikuwepo katika tasnia ya uigizaji kwa miaka mingi , msanii amebeba uhusika kulingana na hadithi yenyewe nasema ni msanii anayejua kuigiza na hilo mtalismtalishuhudia katika filamu hiyo,” said Mzee Korongo.
NYUMBA MPYA YA CEO WA CASH MONEY
Ronald
Williams Aka Slim ambaye ndio C.E.O Wa Cash Money ndiye amenunua nyumba
ya thamani ya Dollar zaki Marekani Milliom $ 7.15. Ni Nyumba yenye
vyumba 9 vya kulala ,Mabafu 12.
Unuunnuzi wa nyumba hii umekuwa wa siri sana kitu ambacho ni tafauti na wasanii wa kundi hilio la Cash Money huwa wanapenda kutangaza mambo yao yote ya thamani. Ronald ni kaka wa Bryan 'Birdman' Williams na ni mmoja wa wadau matajiri sana kwenye mziki Marekani mwenye Thamani ya Dollar za Kimarekani Million $100
Unuunnuzi wa nyumba hii umekuwa wa siri sana kitu ambacho ni tafauti na wasanii wa kundi hilio la Cash Money huwa wanapenda kutangaza mambo yao yote ya thamani. Ronald ni kaka wa Bryan 'Birdman' Williams na ni mmoja wa wadau matajiri sana kwenye mziki Marekani mwenye Thamani ya Dollar za Kimarekani Million $100
Subscribe to:
Posts (Atom)