Yule ombamba maarufu kuliko wote nchini , Matonya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
“Namtaarifu Komredi Yusufu Makamba, kuwa yule kiboko yake
'MATONYA' amefariki usiku wa kuamkia leo kijijini kwakwe Mpamantwa wilaya ya
Bahi, mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni kijijini hapo. Habari ziwafikie,
Mkuu wa Wilaya Betty Mkwasa, Familia ya Mzee Makamba popote walipo, wakazi wa
Dar na Moro pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote. Bila ya kusahau wale wa
eneo la Darajani Mjini Morogoro", ameandika mwandishi wa habari Habel Chidawali
ambaye amewahi kumfanyia mahojiano ombamba huyo.
Matonya amefariki akiwa anaishi kwenye nyumba ya tembe
ambayo ni mali ya mtoto wake wa kike
aitwaye Elizabeth Matonya.
Nyumba hiyo ya asili ya watu wa Dodoma ipo kwenye Kijiji cha
Bahi Sokoni katika Kitongoji cha Nghungugu, umbali wa kilomita 3 kutoka yalipo
makao makuu ya wilaya ya Bahi.
Katika mahojiano aliyofanya na Habel, Matonya enzi za uhai wake
alisema kuwa hana mali yoyote kama wengi walivyokuwa wanadhani.
“Watu wanasema kuwa nina mali, lakini ni ‘walambi’
(akimaanisha kwamba ni waongo). Mimi sina kabisa mali; hata mbuzi; hata kuku
sina na wala sina mpango wa kununua tena hata kama nina pesa kwa kuwa
walishazoea kuniibia, hivyo sitaki tena kuwa na mali.”
Nilikuwa na ng’ombe wengi sana. Kila wakati walikuwa
wakiwaiba wakati ninaishi Kilimatinde na ng’ombe hao nilinunua kwa pesa yangu
ya kuomba huko Dar es Salaam. Walikuwa wengi lakini waliibwa wote na ndugu
zangu.
Kuhusu kuacha kuomba
Jibu: Labla serikali inijengee nyumba nzuri hapa na inipe
mtu wa kunitunza au hata wakijenga nyumba nzuri kwa mtoto wangu halafu
wanisaidie na chakula pamoja na chai ya kila siku, mimi naweza kustaafu kazi
yangu lakini bila ya kufanya hivyo kazi yangu nitakufa nayo.
Katika mahojiano hayo Matonya alisema alikuwa akipata kati
ya Sh50,000 hadi 100,000 kwa mwezi na mara nyingi alikuwa akirudi kijijini kila
baada ya miezi miwili au mitatu tangu alipoanz`a kazi hiyo mwaka 1961.
Rest in Peace Matonya.
No comments:
Post a Comment