Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday, 20 February 2013

OSCAR PISTORIUS ASHIKWA PABAYA MAHAKAMANI!

Ile kesi ya Oscar Pistorius, mkimbiaji riadha kwa kutumia miguu ya bandia, kutuhumiwa kumuuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp siku ya Valentine imepata taswira mpya leo hii! Shahidi mmoja akitoa ushuhuda wake mahakamani jana alisema kuwa Oscar Pistorius alipomtungua  Reeva kwa bastola yake kwa maya ya kwanza, Reeva alisikika akilia, lakini Pistorius aliendelea kummiminia na kummiminia risasi!

Pistorius mahakamani

Oscar Pistorius na Reeva Steenkamp
Ikiwa bado masikilizano ya dhamani yakiendelea siku ya Jumatano shahidi mwingine alisema kuwa alisikia mlio wa risasi huku kukiwa na mwanga, mara akasikia mwanamke akilia kwa maumivu, na tena milio ya risasi iliendelea. Sasa hii ni tofauti na maelezo ya Pistorius aliyesema mahakamani kuwa alimpiga mtu (mpenzi wake) kukiwa na giza nene. Zaidi ya hapo bado upande mashtaka unasema kuwa upo ushahidi wa kuwepo kwa majibizano baina ya Pistoruis na Reeva kati ya saa nane na tisa usiku kabla ya mauaji.

Chooni ulipokutwa mwili wa marehemu Reeva Steenkamp
  
Ushahidi huu wote unamuweka Pistorius katika wakati mgumu zaidi hasa wa kupata dhamani kwa wakati huu.



SABABU YA KIFO CHA GOLDIE HIKI HAPA!

Ni muda sasa kukiwa na ukimya maradufu na sintofahamu kuhusiana na nini kilimuuwa msanii wa Nigeria Goldie. Sasa sababu ya umauti wake hadharani.

‘Stroke’ ama Kiharusi kilichosababishwa na kupanda kwa presha, High Blood Pressure au Hypertensive intracerebral hemorrhage kwa muda mrefu! Inasemekana Goldie aliathirika kwa muda mrefu. Hypertensive intracerebral hemorrhage ni aina ya Kiharusi inayosababisha kuvuja kwa damu kwenye ubongo!


NGULI WA FILAMU NIGERIA AFARIKI DUNIA!


Mwigizaji nguli wa maigizo ya filamu nchini Nigeria, Justus Esiri, 70, amefariki dunia. Jabali hili la filamu lilijizolea umaarufu mzito na kupewa jina la ‘headmaster’ kutokana na tamthiliya ya Village Headmaster mwaka 1980 ameiaga dunia jana usiku, February 19! 


Katika maisha yake ya uigizaji, Mzee Justus Esiri aliweza kujitwalia tunzo kadhaa zikiwemo THEMA Awards, NTA Honours Awards and AMAA Awards. Na baadhi ya filamu alizoigiza ni Wasted Years, Forever, The Prize, Six Demons, Corridors of Power, Last Knight, The Tyrant, The investigation, The Ghost

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na sababu ya kifo cha Mzee Justus Esiri.

RIP Justus Esiri