Friday, 17 August 2012
MAUNDA ZORRO AIBUKIA KWENYE MOVIE
Baada ya Maunda Zorro kuwa nje ya game yake kwa muda wa takribani miaka minne now she's back but round hii kwenye movie scene.
Kwa mujibu wa Maunda Zoro ni kwamba ukimya wake ulitokana na kuwa bussy location akiigiza movie inayptarajiwa kutoka hivi sasa kwa jina la "
Room Number 13" chini ya kampuni ya ZG iliyopo Zanzibar ambayo ndani yake amecheza kama ghost.
Does that means anaacha mziki, "No siwezi kuacha mziki.Pamoja na kuwa kwangu kimya nilikuwa na-record ngoma ambazo management yake ilikuwa ikizizuia kuzitoa na hadi leo sijui inakuweje"-Maunda.
PUSH MOBILE WAKO TAYARI KUBORESHA MALIPO YA WASANII
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited, Freddie Manento
akizungumza na wanamuziki na wadau wake waliofika katika mkutano huo
wa kujadili masuala mbali mbali ya biashara ya muziki nchini.
Chart inayoonyesha malipo ya nyimbo za wasanii.
Wasanii wakifuatilia.
Producer Man Maji akifuatilia kwa makini.
Msanii
maarufu wa bongo fleva, Ferouz akiwa na meneja wake Petee wakifuatilia mkutano huo kwa makini.
Mkutano huo ulijadili masuala mbali mbali ya kuboresha malipo ya
wanamuziki hao ambapo Push Mobile Limited iliahidi kupigana kufa na
kupona na wadau wake (kampuni za mitandao ya simu za mkononi) ili
kuboresha malipo yao.
---
KAMPUNI
ya Push Mobile Limited imeahidi kuboresha kazi za wanamuziki pamoja
na asilimia ya malipo yanayotokana na milio na miito ya simu.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Freddie Manento
katika mkutano na wanamuziki na wadau wa muziki uliofanyika kwenye
hotel ya Serena.
Manento
alisema hayo baada ya kuweka bayana mchakato mzima wa mfumo wa
biashara ya muziki Tanzania katika mkutano uliohudhuria na wasanii
zaidi ya 80 wa muziki wa aina tofauti ikiwa kama injili, bongo fleva,
muziki wa dansi, taarab na reggae, hip hop na watayarishaji mbali
mbali (producers).
Alisema
kuwa kwa sasa Push Mobile inatoa wastani wa asilimia 20 mpaka 40 kwa
mwanamuziki pamoja na wadau wao . Alisema kuwa kiwango hicho hutolewa
baada ya wao kupokea kutoka kwa mitandao ya simu kati ya asilimia 35
mpaka 60.
“Lengo
letu ni kuona wanamuziki wanafaidika na kazi zao hasa kupitia milio
na miito ya simu, biashara ambayo kwa sasa imewaingizia kipato
kikubwa wanamuziki baada ya kuanguka kwa soko la mauzo ya albamu e na
kutopata kipato chochote kutoka kwenye redio na televisheni kama
ilivyoelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia
wakati anajibu hoja ya Mbunge wa Chadema, Zitto Kabwe,” alisema
Manento.
Alisema
kuwa asilimia ngapi wataongeza, itatokana na majadiliano na kampuni
za mitandao ya simu na hata kama kampuni hizo zitakataa kuongeza ili
kuwafaidisha wasanii, wao wataongeza tu.
Alifafanua
kuwa kampuni yao imekuwa ikiingia gharama kubwa za kiuendeshaji
katika kupromoti nyimbo za wasanii ili kuweza kupata soko.
“Tunatumia
si chini ya milioni 25 kwa mwezi kwa ajili ya kuandaa matangazo na
kudhamini vipindi katika redio na televisheni kwa ajili ya kupromoti
nyimbo za wasanii ili kuweza kupata masoko, pia tunatumia zaidi ya
million 7 kwa kazi ya kutengeneza nyimbo ili ziwezwe kuingizwa katika
mifumo mbali mbali ya simu za mikononi,” alisema.
Kuhusiana
na kuchelewa kwa malipo ya wanamuziki, Manento alisema kuwa tatizo
hilo linatokana na ucheleweshwaji wa wadau husika kufanya malipo kwa
wakati.
“Push
imejitahidi kuondoa tatizo hilo kwa kuwalipa wanamuziki kwa fedha
zake huku ikiendelea kudai kutoka kwa wadau husika ambao mara
nyingine ukaa miezi sita bila kutulipa, ni changamoto kwetu, lakini
tumejitahidi kufikia malengo na kutatua matatizo kwa wasanii, japo
changamoto ni kubwa, nawaomba wanamuziki kuelewa tatizo hilo, ”
alisema.
Akizungumza
katika mkutano huo mtayarishaji maarufu wa muziki nchini, John Water
Sharizo au Man Water aliipongeza Push Mobile kwa jitihada zake za
kuinua kipato kwa wanamuziki kwani zamani walikuwa wananyonywa sana
katika mauzo ya albamu.
Man
Water alisema kuwa ni jukumu la Push Mobile ambayo inafanya kazi na
wanamuziki wengi hapa nchini kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata
faida na kazi zao kwani wao ndiyo wameingia mikataba na wanamuziki na
wala siyo makampuni ya simu.
Alisema
kuwa wanashukuru kwa kipato kilichopo kwani hapo awali walikuwa
wanachapisha CD au kaseti 200 na kuuzwa mwaka mzima bila kupata
mrahaba kinyume na sasa.
PAH ONE NA CAMP MULLA WANAUFANANO
Japo si haki kuyalinganisha makundi haya kwa kuzingatia
mafanikio na umaarufu kutokana na ukweli kwamba Camp Mulla wapo mbali zaidi na
wanajulikana kimataifa kuliko Pah One, kuna mengi yakufanana katika makundi
haya mawili. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa yote ni coincidence tu na hakuna lililoiga
kundi jingine. Pah One wanawakilisha Tanzania na Camp Mulla wanawakilisha
Kenya.
10. Wote wana akaunti maarufu ya mtandao wa muziki wa
Reverbnation
Haya ni mambo kumi wanayofanana:
1. Makundi yote yaliundwa miaka miwili ama mitatu iliyopita
2.Makundi yao yanaundwa na waimbaji/marapper wanne
PahOne – Aika, Ola, Nah Reel na Igwe
Camp Mulla - Taio Tripper, Shappa Man, Miss Karun, K'Cous
, Japo yupo pia
Mykie Tuch ambaye ni CEO
Camp Mulla |
3.Kila kundi lina wavulana watatu na msichana mmoja
PahOne – Aika
CampMulla - Miss
Karun
4. Kila kundi lina producer ambaye ni member pia na
nyimbo zao hutengeneza wenyewe
PahOne – Nah Reel
Camp Mulla - K'Cous na Shappa Man
5. Wengi wana miaka chini ya 25
6. Wengi bado wanasoma
7. Karibu wote wanatokea kwenye familia bora
Pah One – Ola na Igwe wamesomea Afrika Kusini , Aika na
Nah Reel wamesomea India
Camp Mulla – Mtandao mmoja uliwahi kuwaponda kuwa
wanapendelewa kwakuwa wanatoka kwenye familia bora
Pah One |
8. Muziki wanaofanya ni wa aina moja (Hip hop, dance na
aina zingine za muziki wa kisasa)
9. Uvaaji wao unafanana sana
KEKO KUKINUKISHA JIJINI MWANZA WEEKEND HII
Rapper wa kike toka nchini Uganda, Keko anatarajiwa kupiga show
weekend hii jijini Mwanza.
Taarifa hiyo ameitoa mwenyewe kupitia Twitter account yake.
“TANZANIA ARE YOU READY!!! #KEKONIANS IN MWANZA
#MAKEYOUDANCE COMING TO YOU THIS WEEKEND tell every & anyone KEKO Coming!!”
KOFFI OLOMIDE ATUPWA JELA MIAKA MITATU
Stori kutoka Kinshasa Congo DRC zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki maarufu ambae jina lake lina uzito ndani na nje ya Afrika, Koffi Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu au kulipa faini.
Kilichomfanya star huyu wa rhumba mwenye miaka 56 apigwe nyundo hizo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake kwa jina la Diego Lubaki.
Nimemsikia mwandishi wa DW kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi ya mawakili 15 ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani kusikiliza kitatokea nini kwenye kesi yake August 16, 2012.Kabla ya kufikishwa Mahakamani Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni muda mfupi tu baada ya kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya mahakama ndogo Kinshasa kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni pamoja na kumpiga meneja wake ambae amekua akiishi Ulaya.
Mwandishi wa DW amesema ugomvi huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro elfu sita ambapo mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi alimpiga ngumi meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.
Hata hivyo meneja huyo aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka yake dhidi ya Koffi na kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao lakini majaji walilipiga chini hilo ombi lake.
Baadhi ya wananchi waliotoa maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono adhabu hiyo na kusema amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye, mwingine amesema ni safi kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye kutenda kosa.
Kutokana na adhabu hiyo kiongozi wa mawakili wanaomtetea Koffi amesema wamepanga kukata rufaa lakini wanasubiri maoni ya Koffi mwenyewe.…
Subscribe to:
Posts (Atom)