Friday, 17 August 2012
KOFFI OLOMIDE ATUPWA JELA MIAKA MITATU
Stori kutoka Kinshasa Congo DRC zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki maarufu ambae jina lake lina uzito ndani na nje ya Afrika, Koffi Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu au kulipa faini.
Kilichomfanya star huyu wa rhumba mwenye miaka 56 apigwe nyundo hizo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake kwa jina la Diego Lubaki.
Nimemsikia mwandishi wa DW kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi ya mawakili 15 ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani kusikiliza kitatokea nini kwenye kesi yake August 16, 2012.Kabla ya kufikishwa Mahakamani Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni muda mfupi tu baada ya kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya mahakama ndogo Kinshasa kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni pamoja na kumpiga meneja wake ambae amekua akiishi Ulaya.
Mwandishi wa DW amesema ugomvi huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro elfu sita ambapo mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi alimpiga ngumi meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.
Hata hivyo meneja huyo aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka yake dhidi ya Koffi na kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao lakini majaji walilipiga chini hilo ombi lake.
Baadhi ya wananchi waliotoa maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono adhabu hiyo na kusema amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye, mwingine amesema ni safi kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye kutenda kosa.
Kutokana na adhabu hiyo kiongozi wa mawakili wanaomtetea Koffi amesema wamepanga kukata rufaa lakini wanasubiri maoni ya Koffi mwenyewe.…
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment