MWANAMITINDO  maarufu nchini, Ally Rehmtullah pichani juu atazindua onyesho rasmi la kazi zake mpya  za
 mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanawake na wanaume ‘Ally Rehmtullah 
2013 Collection’lililopangwa kufanyika Hoteli ya Serena,  jijini Dar es Salaam, Septemba 8 2012.
  Rehmtullah
 alisema dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha 
aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati za 
kuinua kiwango cha kazi za mitindo kwa Tanzania.
“Nimepania kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini,  ili
 kazi za wanamtindo na wabunifu ziweze kupenya kwenye soko la ndani na 
la Afrika Mashariki na ya kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika 
jumuiya ya Afrika mashariki,’ alisema.
Pia
 aliongeza kuwa, kwenye uzinduzi huo mavazi na onyesho litapambwa kwa 
rangi nyeupe, ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi 
yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa 
mwafrika.
Aidha,
 Rehmtullah alisema licha ya kuonesha mavazi pia kutakua na burudani 
mbalimbali kutoka kwa wasanii nyota, ambapo pia aliwataja wadhamini 
wakuu wa onyesho hilo kuwa, Mercedez Benz, Mo Blog, Belvedere Vodka, 
Dulux, Raha, Hugo Domingo,The Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm 
Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia 
Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Missie Popular Blog, Quality 
Furniture na Mx Carter.
Katika onesho hilo, linatarajia kudhuriwa na watu 400, wakiwemo viongozi wa serikali, wafanyabiashara na wageni mbalimbali  ambapo watashuhudia wanamitindo wengine mahili na chipukizi watakaoonesha mitindo siku hiyo.
 

 
No comments:
Post a Comment