Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited, Freddie Manento
akizungumza na wanamuziki na wadau wake waliofika katika mkutano huo
wa kujadili masuala mbali mbali ya biashara ya muziki nchini.
Chart inayoonyesha malipo ya nyimbo za wasanii.
Wasanii wakifuatilia.
Producer Man Maji akifuatilia kwa makini.
Msanii
maarufu wa bongo fleva, Ferouz akiwa na meneja wake Petee wakifuatilia mkutano huo kwa makini.
Mkutano huo ulijadili masuala mbali mbali ya kuboresha malipo ya
wanamuziki hao ambapo Push Mobile Limited iliahidi kupigana kufa na
kupona na wadau wake (kampuni za mitandao ya simu za mkononi) ili
kuboresha malipo yao.
---
KAMPUNI
ya Push Mobile Limited imeahidi kuboresha kazi za wanamuziki pamoja
na asilimia ya malipo yanayotokana na milio na miito ya simu.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Freddie Manento
katika mkutano na wanamuziki na wadau wa muziki uliofanyika kwenye
hotel ya Serena.
Manento
alisema hayo baada ya kuweka bayana mchakato mzima wa mfumo wa
biashara ya muziki Tanzania katika mkutano uliohudhuria na wasanii
zaidi ya 80 wa muziki wa aina tofauti ikiwa kama injili, bongo fleva,
muziki wa dansi, taarab na reggae, hip hop na watayarishaji mbali
mbali (producers).
Alisema
kuwa kwa sasa Push Mobile inatoa wastani wa asilimia 20 mpaka 40 kwa
mwanamuziki pamoja na wadau wao . Alisema kuwa kiwango hicho hutolewa
baada ya wao kupokea kutoka kwa mitandao ya simu kati ya asilimia 35
mpaka 60.
“Lengo
letu ni kuona wanamuziki wanafaidika na kazi zao hasa kupitia milio
na miito ya simu, biashara ambayo kwa sasa imewaingizia kipato
kikubwa wanamuziki baada ya kuanguka kwa soko la mauzo ya albamu e na
kutopata kipato chochote kutoka kwenye redio na televisheni kama
ilivyoelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia
wakati anajibu hoja ya Mbunge wa Chadema, Zitto Kabwe,” alisema
Manento.
Alisema
kuwa asilimia ngapi wataongeza, itatokana na majadiliano na kampuni
za mitandao ya simu na hata kama kampuni hizo zitakataa kuongeza ili
kuwafaidisha wasanii, wao wataongeza tu.
Alifafanua
kuwa kampuni yao imekuwa ikiingia gharama kubwa za kiuendeshaji
katika kupromoti nyimbo za wasanii ili kuweza kupata soko.
“Tunatumia
si chini ya milioni 25 kwa mwezi kwa ajili ya kuandaa matangazo na
kudhamini vipindi katika redio na televisheni kwa ajili ya kupromoti
nyimbo za wasanii ili kuweza kupata masoko, pia tunatumia zaidi ya
million 7 kwa kazi ya kutengeneza nyimbo ili ziwezwe kuingizwa katika
mifumo mbali mbali ya simu za mikononi,” alisema.
Kuhusiana
na kuchelewa kwa malipo ya wanamuziki, Manento alisema kuwa tatizo
hilo linatokana na ucheleweshwaji wa wadau husika kufanya malipo kwa
wakati.
“Push
imejitahidi kuondoa tatizo hilo kwa kuwalipa wanamuziki kwa fedha
zake huku ikiendelea kudai kutoka kwa wadau husika ambao mara
nyingine ukaa miezi sita bila kutulipa, ni changamoto kwetu, lakini
tumejitahidi kufikia malengo na kutatua matatizo kwa wasanii, japo
changamoto ni kubwa, nawaomba wanamuziki kuelewa tatizo hilo, ”
alisema.
Akizungumza
katika mkutano huo mtayarishaji maarufu wa muziki nchini, John Water
Sharizo au Man Water aliipongeza Push Mobile kwa jitihada zake za
kuinua kipato kwa wanamuziki kwani zamani walikuwa wananyonywa sana
katika mauzo ya albamu.
Man
Water alisema kuwa ni jukumu la Push Mobile ambayo inafanya kazi na
wanamuziki wengi hapa nchini kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata
faida na kazi zao kwani wao ndiyo wameingia mikataba na wanamuziki na
wala siyo makampuni ya simu.
Alisema
kuwa wanashukuru kwa kipato kilichopo kwani hapo awali walikuwa
wanachapisha CD au kaseti 200 na kuuzwa mwaka mzima bila kupata
mrahaba kinyume na sasa.
No comments:
Post a Comment