Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday, 25 April 2013

NDANI YA MJENGO WA PETER P-SQUARE!

Muda mfupi uliopita Peter Okoye ametupia picha zifuatazo kwenye page yake ya Instagram na kuandika, "home sweet home".






 

 


T-PAIN ANYOA DREADS!

Msanii wa Hip-hop na RnB pande za USA, T-Pain, ameamua kunyoa dreads zake. T-Pain pia aliandia hivi kupitia instagram, "We must all learn to adjust with our surroundings. Those who get stuck doing the same things for too long are bound to get left behind the strong who press on and reinvent themselves. Also. Good news. Hair grows back,"

T-Pain wa zamani
T-Pain pia alichukua nafasi kutangaza ujio wake mpya wa albam, 'Stoicville' bila kutaja lini itakuwa tayari but just tay tuned!
T-Pain mpya

Tuesday, 23 April 2013

MKESHA WA UBINGWA WA 20 MACHESTER UNITED!

Baada ya kuchukua ubingwa kwa mara ya 20, mkesha wa shamrashamra hizo ulifanyika Cafe Rouge. Wayne Rooney, Robin van Persie na Rio Ferdinand waliongoza sherehe hizo zilizoishia leo asubuhi ya saa 12!

Bata lilianzia chumba cha kubadilioshia nguo!



Usiku wake sasa.....







Asubuhi ya leo wakijirudisha taratibu....
 


JAY Z & KANYE WEST: HATUNA TATIZO!

Baada ya Kanye West kumchana Jay Z live on stage katika concert yake huko Uingereza back in February, juzi walikutana mitaa ya New York City na ku-hug kama vile hakuna kitu kilichotokea. Hii inaonyesha ni ,kisasi gani Jay Z anajiheshimu na haendekezi vi-bifu vya kijinga.

West alipokuwa on-stage miezi miwili iliyopita alisema, "I got love for Hov, but I ain't f***ing with that 'Suit & Tie." Akimaanisha anamuhudu Hov (yaani Jay Z) lakini sio shabiki wala haikubali 'Suit & Tie'. 'Suit & Tie' ni ngoma ya Justine Timberlake featuring Jay Z.



VITA YA LADY JAY DEE NA CLOUDS FM YAHAMIA KWA SALEH ALI WA GPL.

Mwandishi wa habari wa Global Publishers Limited, Saleh Alli ameingilia kati vita ya Lady Jay Dee 'Anaconda' na Clouds Fm 'Superbrand', kwa kuandika makala ndefu. Chukua time kusoma kile alichokiandika Saleh na majibu aliyotoa Jay Dee!

MGOGORO wa kimuziki kati ya msanii Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na kituo kimoja cha redio umezidi kuchukua kasi huku makundi mawili, kila moja likitengeneza ngome yake na kuamini linachoamini.
 
Kundi ambalo linamuunga mkono Jaydee na kumuona ni mkombozi, anazungumza kwa niaba yake na wasanii wengine, la pili ni lile linalobaki upande unaoshambuliwa, linatetea ngome yake.
 
Jaydee anashutumu kubaniwa nyimbo zake na kituo hicho ambacho kupitia mitandao kadhaa ya kijamii ameeleza wazi kuwa wanambania, wanaziponda lakini hata watangazaji wake wamekuwa wakionyesha chuki binafsi dhidi yake.
 
Jaydee pia aliwaponda wasanii Ben Pol na Linah anayetokea THT kwamba walishindwa kutokea kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wake wa Joto Hasira, kwa madai walizuiwa na bosi wao.
Ujasiri huu wa Jaydee ndiyo kitu bora ambacho kimekuwa kikitakiwa kufanyika kutoka kwa wasanii, yaani wapigane kutetea muziki wa Tanzania hasa kama kuna watu au kundi la watu limejikita katika kuuangamiza.
 
Lakini ni tofauti kidogo, kwani wasanii wengi wamekuwa imara na kuwa tayari kujitetea wenyewe tu na si vingine. Nasisitiza mara nyingi, wao ndiyo wahusika wa kwanza na wanapaswa kuanzisha mapinduzi kuanzia kwao, mfano kusema naonewa si kitu kibaya lakini je, umewahi kupigania wanaoonewa?
 
Kujitetea pekee unaweza kufanya, lakini vipi utafanikiwa kama asilimia kubwa ya kundi la wanamuziki linaendelea kuonewa. Ukibaki hauonewi pekee na asilimia kubwa ya wasanii au wanamuziki inaonewa, kunaweza kuwa na mapinduzi sahihi?
 
Ndiyo maana nashangazwa kusikia Jaydee leo anaona ubovu wa kituo hicho, anathubutu kusema hadharani akionyesha wazi ameumia. Lakini miaka 10 au zaidi iliyopita, Jaydee alikuwa kimya na hakuwaza kusema kwamba kituo hicho kinawabania wasanii wengine na‘kumtukuza’ yeye hata kama muziki wake haukuwa wa kiwango kilichokuwa kinazungumzwa.
Siwezi kusema muziki wa Jaydee ni mbaya, nimekuwa kati ya mashabiki wake. Lakini yoyote atanichekesha akisema nyimbo albamu zake zote alizotoa zilikuwa katika kiwango cha juu sana na ndiyo maana leo ni maarufu.
 
Hakuna asiyejua kwamba miaka nenda rudi, wasanii wamekuwa wanaongoza kwa unafiki, kutopendana wenyewe, kugeukana na hata kujenga makundi lukuki, ndiyo maana kila kukicha wamekuwa wakishambuliwa maana katika maisha yao hawana umoja.
 
Jaydee alianza kuwa mtangazaji katika kituo hicho baada ya kuacha kurap, akaamua kuachana na kurap na mwisho kuwa msanii wa nyimbo za kubembeleza, mara ya kwanza akianza kutikisa na albamu ya Machozi, Solo Thang anaweza kuhadithia vizuri kuhusu hili.
 
Kuanzia albamu ya Machozi, kituo hicho ndicho kilisimama kuhakikisha anakuwa bora hata kama muziki wake haukuwa ukimzidi kila mwanadada wakati huo.
Angalia, kulikuwa wasanii kama Stara Thomas, Carola Kinasha ambao kiuwezo walikuwa juu kuliko Jaydee, lakini hawakupewa nafasi ya kutosha, badala yake Jaydee ambaye hakuthubutu kuwatetea hata kidogo akaendelea‘kubebwa’ na watu wakaamini ni bora kuliko yoyote kwa upande wa akina dada au kina mama katika kuimba, haikuwa hivyo.
 
Angalia albamu ya Binti, karibu nyimbo zote zilikuwa na ujumbe mmoja, ulikuwa ukimshambulia mwaname mmoja ambaye alikuwa amemuumiza Jaydee. Takribani ujumbe wa nyimbo karibu zote ulikuwa ni mmoja, lakini ilibebwa na kuonekana ni moja ya albamu bora kabisa kuwahi kuwepo katika muziki wa Tanzania, kitu ambacho hakikuwa sahihi.
 
Wakati huo wasanii lukuki walilia kubaniwa, mmoja wao alikuwa ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ndiye alimtambulisha mwanadada huyo alipomshirikisha katika wimbo wa Mambo ya Fedha, kabla ya hapo hakuwa na jina. Jaydee hakuwahi kuungana naye hata kidogo hata kwa mstari mmoja wa kumtetea au kuunga mkono kutetea muziki wa Tanzania, kuonyesha anapinga mwenendo wa wanaolazimisha kuwabagua wasanii au kufanya mambo kwa mabavu kwa kuwa wameshika mpini.
 
Hakuna aliyesikia kilio cha Sugu, wasanii wanaochipukia bila ya kujua wasemacho, kisa nyimbo zao zinapigwa redioni, ili kuonyesha shukrani za dhati wakaanza kutangaza Sugu anatapatapa na amekwisha kimuziki!
 
Ajabu, asilimia kubwa ya maneno yake ndiyo yanayozungumzwa leo, ndiyo yanatumiwa na kila msanii anayebanwa au kuhisi kaonewa. Angalia, hata Jaydee naye ameingia huko! Swali langu hapa je, Jaydee na wengine wanaolalamika, wamekwisha kisanii?
 
Ndiyo maana nasema, tasnia ya muziki hasa muziki wa kizazi kipya umejaza watu wavivu kufikiri, wenye mioyo ya ‘Kichina’, wasio na uwezo wa kuthubutu hata kidogo ambao wanasubiri wayumbe au kuumizwa wao ili wamtafute wa kumuangushia lawama.
 
Jiulize, kama Jaydee alibebwa kwa miaka 10, halafu leo analalamika atakuwa sahihi? Sitaki kumpinga kwa kuwa kuna kitu anakiona lakini ninaamini alikiona tokea mapema, akauchuna.
 
Bado nasisitiza, yeye na wengine wote wanaolia baada ya kuguswa wao nawaita wanafiki, wanapigana kwa ajili yao na si kwa muziki wanaoutumikia. Iwapo wangekuwa tayari kupambana kwa ajili ya muziki huo, msanii kama Jaydee asingeanza vita leo.
 
NARUDI KWA JAYDEE
Sijawahi kuingia naye katika malumbano zaidi ya miaka 10 tokea alipokuwa mwanahabari mwenzangu na sasa msanii. Lakini nathubutu kumueleza kuwa ni kati ya wasanii wasiojali muziki wa Tanzania na wanajiangalia wao zaidi.
 
Picha ya unafiki na kujiangalia mwenyewe inaonekana sasa ingawa takribani miaka mitano iliyopita nilianza kuinusa. Leo analia, anabaniwa na anauona moto unaounguza muziki wa Tanzania ulivyo mkali.
 
Naamini aliuona miaka kibao nyuma, lakini kwa kuwa alikuwa akitetewa hakuweza kuangalia kwamba rafiki zake, wasanii waliombeba kabla walikuwa wakiungua. Akaendelea kuwapita kwa raha zake mustarehe.
 
Tungeweza kumuita Jaydee ni mpambanaji kama angewakosoa hao anawakosoa sasa katika kipindi walichokuwa wamempa mbeleko yeye, basi kweli ingeonekana anapigania muziki wa Tanzania. Sasa anapigania chake tu!
 
Jaydee amefika mbali kimuziki, alikuwa bora jukwaani na nyimbo kadhaa na nyingi zikapewa ‘over promotion’ lakini bado ninaweza kumuita mkongwe. Ajabu alibaki chipukizi hadi leo katika suala la kutetea haki za wasanii na muziki wenyewe.
 
Sitaki kumkatisha tamaa kwa mapambano aliyoyaanza, ninaamini ana nafasi ya kuanza kuusaidia muziki ambao umemsaidia. Lakini ndiyo kipindi ambacho anaweza kupata machungu waliyopata wasanii wenzake kunyeshewa mvua na kuunguzwa na jua wakati akiwa kivulini kwa ‘msaada’.
 
Anachokifanya leo Jaydee ni nyongeza tu ya walichokifanya Sugu au Afande Sele au wasanii wachache walioamua kuwa wakweli au wale walioamua kuwa wabunifu kama Ambwene Yessaya‘AY’, aliyekimbia vita ya redio na kuingia katika kurekodi video bora zilizoendelea kumng’arisha.
 
Simzuii, Jaydee kuendelea kupambana, lakini namuasa anachokifanya kama ni kwa ajili ya muziki akipozwa tena, asirudi nyuma.
 
Ninachomkumbusha, hata yeye amekuwa kundi moja na analowalaumu ambao angeweza kuwashauri mapema ‘ndani ya mjengo’ kama angekuwa na nia nzuri na muziki wa kizazi kipya. Msisitizo ‘Joto Hasira’ liwe la kweli.
 
Jay Dee alikuwa na haya ya kujibu:
 
Huyo Saleh si alimsema Shigongo mbona alirudi nyuma na kufanya kazi kwake!? Nafahamu pia ni mtu wa (Jina nalihifadhi) hivyo hanisumbui kichwa. Then anajiita mwandishi huku akiandika habari ambazo hana uhakika nazo. Bullshit.

Hajui tulichopitia na tulichovumilia anadhani tulikuwa tunaogelea mfereji wa maziwa na asali, km ni kuzuri mbona tumetoka.

 
 

Friday, 19 April 2013

VIDEO MPYAA: POMBE YA MADEE


BINTI YA GENEVEIVE NNAJI AFAHAMIKA!

Unaambiwa hajawahi kutokea msanii mwenye kutunza siri huko Naija kama Geneveive Nnaji. Geneveive ameweza kumficha binti yake kwa kipindi kirefu sana bila media yoyote kushtukia. Kwasasa binti yake anatimiza miaka 18 ndio kama media wanasanuka hivi.

Geneveive alipata ujauzito akiwa na miaka 15 tu. Mpaka sasa hajafahamika baba wa mtoto huyo ni nani lakini mchizi mmoja anayeitwa Acura amejitokeza na kudai yeye ndio mshua wa binti huyo!

The exclusive pictures unazoziona ni huyo binti yake Geneveive, Chimebuka a.k.a Lily akiwa zake huko Ughaibuni akimalizia high school na inasemekana modelling ndio ndoto yake!
Just beautiful like her mother.......

MSANII WA UGANDA AWAACHIA MASHABIKI WAZISHIKE NYETI ZAKE STEJINI!

Huyu ni msanii wa nchini Uganda. Akiwa on stage bila hiana wala kubana aliwaachia mashabiki wake wafanye chochote watakacho pale aliwasogelea na kuwaachia sehemu zake za siri. Baadhi ya mashabiki waliingiza mikono yao kunako nyeti za msanii huyo bila hata yeye kushtuka wala kujinasua toka kwa mashabiki hao waliokuwa wana uchu!


 

 

Wednesday, 17 April 2013

MR. NICE AZALIWA UPYA!

Alikuwa moto kwelikweli at his times, Afrika Mashariki na Kati. Mr. Nice, mwimbaji wa ngoma kama ‘Kikulacho’ iliyomfanya avute mkwanja mrefu pengine kuliko msanii mwingine yeyote kwa wakati wote hapa Tanzania. Baada ya kupiga shows lukuki nje na ndani ya Tanzania Mr. Nice alianza kudrop taratibu na katika press conference yake leo hii alisema sababu yeye kushuka ilikuwa ni management yake.


Mr. Nice pia alikanusha kuwahi kuwa na bifu na Jose Chameleone wa Uganda. Zaidi ya hapo Mr. Nice alizungumzia kuhusu wimbo wa “Mac Muga” wa Ali Kiba kuwa haukuwa ukimuhusu yeye na maisha yake ya kimuziki, yaani kupanda na kuporomoka kwake! Mr. Nice alikana kuwa alikwenda Afrika Kusini, hali ya kimisha ikawa mbaya mpaka kurudishwa nyumbani Tanzania. Mr. Nice alikana kwenda Afrika Kusini na kusema kuwa Ali kIba hajawahi hata siku moja kusema kuwa ngoma hiyo inamuhusu yeye Mr. Nice!


The King is back. Mr. Nice amerudi upya katika game na this time amemshirikisha DNA toka Kenya, ngoma inaitwa ‘Tafuta’. Mr. Nice ame-sign label deal na Grandpa production ya Kenya na tarehe 26 April ataanza mfululizo wa kugonga shows hukohuko KE. 

Angalia video ya Mr. Nice feat. DNA:

BI. KIDUDE AFARIKI DUNIA!

Gwiji la muziki nchini Tanzania hususan taarab asilia, Fatuma Binti Baraka "Bi Kidude" hatunaye tena. Taarifa kutoka katika familia yake zinasema Bi Kidude alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal amefariki leo. Bi Kidude atakumbukwa kama mwanamuziki mkongwe zaidi nchini ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 10 tu na aliwahi kupokea tuzo mbalimbali kutokana na mchango wake katika muziki wa mahadhi ya mwambao. Hakika sanaa nchini imepoteza moja ya nguzo kubwa.

Pumzika kwa amani Fatuma Binti Baraka.
 

Tuesday, 16 April 2013

MRS. CARTER TOUR YAANZA!

Kama kuhitaji ku-make headlines tu, basi the wife of Mr. Carter, Jay Z anao uwezo huo na katika show yake ya kwanza kabisa amefanya hivyo. Tour imeanza rasmi huko Belgrade, Serbia  Jumatatu usiku na Beyonce, 31, alipanda on stage ni kivazi cha rangi ya gold, transparent kilichoonyesha maungo yake yote ya ndani kama nipples!

Beyoncé ana shows 64 na atazunguka mabara ya Europe, North America mpaka South America.
 




Monday, 15 April 2013

2013 MTV MOVIE AWARDS RED CARPET FASHION

The 2013 MTV Movie awards ilifanyika usiku wa kuamkia leo huko Los Angeles, California. Na hii ndio red carpet fashion ya A-list stars waliohudhuria utoaji wa tuzo hizi.

Serena Gomes

Hana Mae Lee

Jamie Foxx na binti yake Corrine Bishop

Kerry Washington

Kim Kardashin

RuPaul

Snoop Dogg Lion

Zoe Saldana

Saturday, 13 April 2013

PAUL WA P-SQUARE APATA MTOTO!

Baada ya pacha wake Peter kupata mtoto wa pili wa kike sasa ni zamu ya Paul. Jana Paul Okoye na mchumba wake wa muda mrefu Anita, walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume. Mtoto huyo aliyepewa jina la Andre alizaliwa Atlanta, USA.

Peter tayari ana watoto wawili, toka kwa demu wake wa muda mrefu Lola Omotayo. Welcome to the world Andre Okoye.




SIZE 8: KUKAA UCHI BASI!

Baada ya msanii wa kike Size 8 kutangaza jana kuokoka, sababu ya haraka haikujulikana mapaka alipofanya interview na kutoa yale yaliokuwa yanamsibu. Size 8 ambae kuna wakati nchini Kenya alitangazwa kama msanii mwenye mkwanja mrefu kuliko wote alisema kuwa moja kati ya sababu za yeye kuokoka na kuacha mziki wa kidunia ni pale alipokuwa akitoka kupiga shows za usiku huwa analia usiku mzima na moyoni hakuwa akijisikia amani.


Pia Size 8 alisema kuwa kufuatia hali hiyo ya kutosikia amani moyoni mwake aliamua hata kuipiga chini show ambayo ilikuwa imuingizie milioni 2 za Kenya. Alipoulizwa kama ataendelea kuvaa vimini-vichupi na vinguo vifupi alivyokuwa akitupia hapo awali, Size 8 alisema, "hizo sasa zimekuwa mbaya. No more! No more skimpy clothing! Unajua hizo mavazi zinatisha watu. Sasa nitakuwa nikivaa mavazi za heshima. Mavazi zenye Jehovah pia anafurahia akiniona nazo. Si lazima ikuwe dress refu. Nguo tu ya heshima."


Size 8 tayari ameshatoa ngoma ya gospel iitwayo 'Mateke', icheki hapa:-



P-SQUARE WATOA ONYO!

Kupitia internet biashara kwa wasanii huko Naija imekuwa ngumu sana baada ya kujitokeza makundi ya watu kadhaa wakifanya wao ni mapromota hivyo kuchukua advance za wasanii mbalimbali huku wasanii wenyewe wakiwa hawajui lolote! Mwaka jana kuna mtu alilamba dola 100,000/= kupitia twitter na facebook kwa kudai kuwa yeye ni promota wa kundi la P-Square nchini Ufaransa.

P-Square wametoa onyo kwa wale watakaotaka kuingia nao mikataba ya show kwa kuwa makini na watu hawa katika mitandao hii ya kijamii! Kupitia akaunti yake ya twitter, Peter Okoye alitoa onyo kwa kuandika:
  

Kwa sasa P-Square ndio wasanii wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi nchini Nigeria kwa kuchaji dola 150,000/= kwa shows za kimataifa na Naila milioni 10 kwa shows za nyumbani kwao Nigeria!


Friday, 12 April 2013

AKON AMPONGEZA KENYATTA, AKOSOLEWA!

Baada ya kuapishwa na kuwa raisi kamili, pongezi mbalimbali zimekuwa zikitolewa na mmoja wa watu maarufu ambao hawakuwa nyuma kusifia jinsi mchakato mzima wa uchaguzi ulivyokwenda kwa amani na utulivu mpaka kupatikana kwa raisi Uhuru Kenyatta ni Akon. Baada ya hapo sasa zikatoka comments mbalimbali katika fanpage yake ambazo Akon alizipotezea lakini hii hakuiacha iende hivihivi.


Mmoja wa commenters aliandika hivi, "Huyu (Kenyatta) ni mwizi kama baba yake. Aliiba ardhi na kabila lake tu ndilo lililompigia kura. Kwa sasa ana kesi katika mahakama ya kimataifa na naamini watamtia hatiani. Kwanini (Akon) umpongeze?????"

Ndipo Akon akajibu, "Ndio maana Africa haiwezi kusonga mbele. Tunapoteza muda mwingi katika vitu visivyo na maana. Nimempongeza kwa kufanya uchaguzi kwa njia ya amani! Hii ni hatua kubwa kwa Afrika. Kama kuna lolote baya alilolifanya hapo nyuma ni yeye (Kenyatta) ataenda kujibu kwa Mungu. Sasa kwa kwanini ujiumize kichwa? Sisi sio watu wa kumjaji!"




REEBOK WAMTEMA RICK ROSS BAADA YA KUBAKA!

Hatimaye kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo Reebok imemtema rasmi Rick Ross. Hii ni baada ya the Maybach Music rapper The Boss kutema lines zenye utata tena zenye kumzalilisha mwanamke na kuonekana kama alibaka mwanamke kwa mistari yake katika ngoma ya "U.O.E.N.O".

Mistari ya Rossay inasomeka, ‘Put molly all in her champagne, she ain’t even know it/I took her home and I enjoyed that, she ain’t even know it’. Akimaanisha anamuwekea molly (kilevi) kwenye kinywaji/shampeni ya demu bila yeye kujua. Anampeleka nyumbani kwake na kum-do bila yeye (demu) kujua.
Wanaharakati waliowahi kubakwa juzi kati waliandamana mpaka ofisi za Reebok kuwaomba waache kumdhamini Rossay na Reebok leo hii wametoa tamko kuachana rasmi na rapper huyo na kusikitishwa kwa kile Rossay alichokifanya katikam ngoma hiyo ya Rocko.

Wednesday, 10 April 2013

5 RICHEST HIP-HOP ARTISTES MWAKA 2013.

Jana Gazeti la Forbes la USA limetoa list ya wanamuziki matajiri zaidi duniani katika mziki wa Hip-Hop kwa mwaka 2013 na majina kama Jay-Z, 50 Cent, Diddy na wengine wali-top the list.




1. Sean”Diddy“Combs
Utajiri: $580 million.

 
2. Sean”Jay-Z“Carter
Utajiri: $475 million.


3. Andre”Dr.Dre“Young
Utajiri: $270 million.

4. Bryan”Birdman“Williams
Utajiri: $270 million.


5. Curtis”50 Cent“Jackson
Utajiri: $125 million.