Baada ya msanii wa kike Size 8 kutangaza jana kuokoka, sababu ya haraka haikujulikana mapaka alipofanya interview na kutoa yale yaliokuwa yanamsibu. Size 8 ambae kuna wakati nchini Kenya alitangazwa kama msanii mwenye mkwanja mrefu kuliko wote alisema kuwa moja kati ya sababu za yeye kuokoka na kuacha mziki wa kidunia ni pale alipokuwa akitoka kupiga shows za usiku huwa analia usiku mzima na moyoni hakuwa akijisikia amani.
Pia Size 8 alisema kuwa kufuatia hali hiyo ya kutosikia amani moyoni mwake aliamua hata kuipiga chini show ambayo ilikuwa imuingizie milioni 2 za Kenya. Alipoulizwa kama ataendelea kuvaa vimini-vichupi na vinguo vifupi alivyokuwa akitupia hapo awali, Size 8 alisema, "hizo sasa zimekuwa mbaya. No more! No more  skimpy clothing! Unajua hizo mavazi zinatisha watu. Sasa nitakuwa  nikivaa mavazi za heshima. Mavazi zenye Jehovah pia anafurahia akiniona  nazo. Si lazima ikuwe dress refu. Nguo tu ya heshima."
Size 8 tayari ameshatoa ngoma ya gospel iitwayo 'Mateke', icheki hapa:-
 


 
No comments:
Post a Comment