Gwiji la muziki nchini Tanzania hususan taarab asilia, Fatuma Binti
Baraka "Bi Kidude" hatunaye tena. Taarifa kutoka katika familia yake
zinasema Bi Kidude alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal
amefariki leo. Bi Kidude atakumbukwa kama mwanamuziki mkongwe zaidi nchini
ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 10 tu na aliwahi kupokea tuzo
mbalimbali kutokana na mchango wake katika muziki wa mahadhi ya mwambao. Hakika
sanaa nchini imepoteza moja ya nguzo kubwa.
Pumzika kwa amani Fatuma Binti Baraka.
No comments:
Post a Comment