Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday, 18 July 2012

FINA MANGO ATUA MAGIC FM


Baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kusikika redioni mashabiki wa Fina Mango wana uhakika wa kuanza kuisikia tena sauti yake tamu.

Mtangazaji huyo wa zamani wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, hatimaye  amehamia Magic FM.

Akiwa Magic FM, Fina Mango atakuwa akiendesha kipindi cha 'Mkutano' ambacho kitakuwa kikisikika kila  Jumamosi kuanzia saa 9.00 alasiri – 12 jioni.

Kipindi hicho kiitwacho ‘Makutano’ kitaruka kwa mara ya kwanza tarehe 4 mwezi ujao (August).
“My first radio crush is making a comeback…all the best @Fina_Mango cant wait to hear you again on air,” aliandika shabiki wake wa zamani aitwaye Lijocha.
Apparently, Fina Mango atafanya kipindi hicho kwa makubaliano maalum na sio kuajiriwa kwakuwa tayari ana kampuni yake iitwayo 1Plus Communications.

Tuesday, 17 July 2012

J-LO NA STEVEN TYLER BYE BYE AMERICAN IDOL



Kwa masikitiko makubwa, Steven Tyler and Jennifer Lopez wametangaza kuondoka kwenye American Idol.
Siku ya alhamisi Steven Tyler alitangaza kujitoa kwenye  American Idol kwa kusema, "hataruduia tena kuwa judge wa American Idol".
Kwenye statement hiyo ya Steven aliandika hivi, "After some long… hard… thoughts… I've decided it's time for me to let go of my mistress American Idol before she boils my rabbit."
Steven mwenye miaka 64 kwa sasa, aliongeza kuwa anarudi yaliko Aerosmith yaliko mapenzi yake zaidi  "with two fists in the air and I'm kicking the door open with my band".

Jennifer Lopez nae alitangaza kujiondoa kwake kupitia kwa mwakilishi wake, Mark Young, hapo jana.
Jana asubuhi Jennifer alipiga simu kwenye radio show ya Ryan Searets  na kutangaza kwamba anaondoka American Idol alikokuwa kama judge.
"I honestly feel like the time has come that I have to get back to doing the other things that I do."-Jennifer.
Kuondoka kwao kwenye Amrican Idol kunawabakisha  Randy Jackson na Ryan Seacret lakini rumours za chini chini ni kuwa Randy anatarajiwa kuondoka muda wowote kwanzia sasa.
Kama Randy ataondoka, macho yote yataelekezwa kwa  Ryan Seacrest ili kujua ni hatua gani atakazozichukua.
Sababu za kuondoka kwa majaji hao bado hazijajulikana lakini inawezekana ni kutikana na rating ya show hiyo ilivyoshuka kwa kiwango kikubwa toka mwaka jana.

MARIO VAN PEEBLES KUZINDUA MUVI YAKE MLIMANI CITY


Wakazi wa Dar es Salaam watanufaika na ujio wa muigizaji na muongozaji wa filamu wa Hollywood Mario Van Peebles aliyealikwa mwaka huu kama mgeni wa heshima kwenye tamasha la filamu la kimataifa Zanzibar, ZIFF.

Van Peebles ataizindua filamu yake ya mwaka huu iitwayo ‘We The Party’ ambayo ameiongoza na kuigiza pia.

Kwa ushirikiano na ZIFF, kutafanyika ‘red carpet premier’ ya filamu ya ‘We the Party’ kwenye ukumbi wa Century Cinemax wa Mlimani City.

Tukio hilo litahudhuriwa na yeye mwenyewe Mario Van Peebles na mwanaewa kiume Mandela Van Peebles aliyeigiza kama mhusika mkuu kwenye filamuhiyo.

Filamu hiyo itaoneshwa kwa siku tano mfululizo ili kutoa muda zaidi kwa watu kuiona.

We The Party iliyoigizwa jijini Los Angeles inahusisha marafiki watanowanafunzi wa high school wanaozungukwa na mapenzi, pesa, kujirusha,chuo, sex, bullies, Facebook na mambo mengine.
Rapper Snoop Dogg anaye ameigiza kwenye filamu hiyo.

FIDSTYLE FRIDAY ON YOUR TV IJUMAA IJAYO



Hip Hop music from Tezee is about to hit the next level.

Some artist toka kwenye scene hiyo wamekuwa wakijaribu kukua kutokana na technologiainavyokua kwa kufanya online show na vingine vingi.

Baada ya kanzisha online TV yake ya Cheusi Dawa  ambayo ilikubalika kwa kiasi kikubwa hapa nchini, now Fid Q anahamia kwenye TV.

Kwa mujibu wa Fareed Kubanda ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa "Sihitaji Marafiki" Ijumaa ya tarehe 20 ataonekana kwa mara ya kwanza at EATV aki-run show yake itakayoitwa  "FIDSTYLE FRIDAY".

Ndani ya kipindi hicho Fid atakuwa akizungumzia issue mabalimbali zinazohusu Hip Hop.

Fid Q atakuwa msanii wa pili wa mziki huo kufanya show ya TV baada ya Chid Beenz aliyekuwa aki-host show yake ya "Chid Beenz" ambayo kwa sasa imefia kusikojulikana.

HUSSEIN MACHOZI NA SIZE 8 WAPENZI


Sababu iliyopelekea msanii wa Bongo Flava Hussein Machozi kupageuza jijini Nairobi, Kenya kama uwanja wa nyumbani hatimaye imejulikana.
Hussein ameiambia TanzaniaTopModels kuwa he has found his love in Kenya. Na msichana mwenye bahati ya kuitwa shemeji/wifi na watanzania si mwingine bali ni mwanamuziki maarufu nchini humo Linet Masiro Munyali aka Size 8. Hapo ndipo tunaweza kupata majibu ya kwanini hivi karibuni alisema anafikiria kuhamia moja kwa moja nchini Kenya.Imetokea tu kama bahati mbaya ama nzuri mwandishi wa habari hii ni mtu wa karibu mno na Hussein na hivi ndivyo maongezi yalivyokuwa:
Hussein: Asee eti nasikia wabongo wanadai nimeolewa na size 8..umezipata hizo?
Tanzania Top Model: Sijapata mwanangu, kwani unamla huyo mtoto?
Hussein: haha! wacha nikwambie ukweli man, kitambo sana tumeanza kuwa pamoja ila sa sijui nani kazitoa hizo!
TZ Top Models: Dah kumbe! Hongera sana mwanangu, so mnakaa pamoja?
Hussein: hahaha! mara nyingi huwa tupo pamoja japo kila mtu anakaa kwake.
TZ Top Models: Kwani hutaki watu wajue?
Hussein: aah! wanaeza jua ila sio ka wanavyo sema eti nimeolewa asee!
TZ Top Models: Mlikutana wapi na Size 8? Katika mazingira gani yaani?
Hussein: Kawaida, kuanza kuchat na tukawa marafiki hatimaye imekuwa hivyo.
 
TZ Top Models: Ndio sababu hutaki kuhama Kenya nini?
Hussein: haha! kama unavyojua hakuna mtu anayetaka kukaa mbali na pumzi yake yeye ni sababu kubwa ya mimi kuwa Kenya.
TZ Top Models: Lini unampeleka Singida kwa mama?
Hussein: Coz mi nimekuja kwao naye soon ataenda SINGIDA, MANYONI kujitambulisha.
TZ Top Models: Mna mipango ya kuja kuwa mtu na mke wake kabisa?
Hussein: Yes mipango ni kuwa mke na mume maana hakuna anayetaka kucheza na roho ya mwenzake..
TZ Top Models: So,unazizungumziaje tetesi kuwa Size 8 amekuoa na ndo anakuweka mjini Nairobi?
Hussein: haha! ni uvumi tu mwana kwani mi kukaa kwa mpenzi wangu ndo kusema amenioa? Okay, sasa atakuja TZ KWANGU tusikie watasemaje. Mwisho nasisitiza man tunapendana ki uhakika.
There you have it! Congrats Hussein, nice choice!

DOGO JANJA BACK TO XUL


We all remember tha sagga that happened mwezi uliopita hadi kumfanya Dogo Janja achague kurudi home kwa wazazi wake Arusha.

Haikuchukua round, Ustaadhi Juma na Musoma aliamua kumfuata kijana kwao na hatimae Dogo Janja ali-ink kuwa chini ya Mtanashati Ent. kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake.
The good news kwa wapenzi wa Janjaro ni kuwa leo amerudi rasmi at Makongo High School anakosoma kidato cha pili.


"Namshukuru Mungu bado ananipenda mimi mwanae, yalitokea mengi yaliyonifanya niione Dar chungu kiasi cha hata kukataa kusoma hapa but kila kitu sometimes hutokea kwa sababu, narudi shule rasmi! i cant wait kuwaona wanafunzi wenzangu, walimu wangu! naahidi kusoma sana"- Dogo Janja.