Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedict wa XVI
ametangaza kustaafu nafasi hiyo February
28. Papa huyo aliyechukua wadhifa huo toka mwaka 2005 alikutana na makardinali
huko Vatican leo hii na kutangaza uamuzi huo. Katika taarifu yake Papa alisema
kuwa hali ya afya yake ndio inayomfanya afikie uamuzi huo. Papa Ben XVI alionekana Ijumaa
iliyopita kushindwa kutembea japo alipata usaidizi wa fimbo.
Taarifa ya Papa Ben XVI umepokelewa kwa mshtuko kwani ameutoa bila hata
kushirikisha watu wake wa karibu. Na hii ni tofauti na Papa aliyemrithi, Papa John
Paulo II ambaye hakuachia nafasi hiyo mpaka pale alipofariki licha ya kusumbuliwa
na ugonjwa kwa kipindi kirefu.
No comments:
Post a Comment