Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday, 28 January 2013

NI WAKATI WA LULU KUTENGENEZA PESA?

Alifariki tarehe 7 April, 2012 na kuzikwa tarehe 10 April,2012. Ni miezi 9 imepita baada ya kifo cha mwigizaji maarufu Steven Charles Kanumba, The Great. Sababu au chanzo cha kifo chake kimekuwa bado kitendawili mpaka sasa huku kila mtu akijaribu kukisia sababu halisi. Baadhi ya media na hata polisi wamekuja na ripoti kuwa pengine unywaji uliopindukia wa kilevi cha whiskey, Jacky Daniels ndio sababu. Kuna waliosema eti Kanumba alikuwa mfuasi wa Freemasons ila alikiuka baadhi ya maagizo ndio ikapelekea kifo chake. Wengine wakasema kusukumwa na mwigizaji mwenzake Elizabeth Michael Kimemeta au Lulu ndio chanzo kufuatia majibizano kati yake na Kanumba wanaosemekana walikuwa wapenzi. Hii ikasababisha Lulu kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ‘kuua’ na baadae ‘kuua bila ya kukusudia’. Lulu akatupwa rumande, tarehe 11 April, 2012.


Dhamana inayofikia milioni 40 imepitishwa na taratibu za kimahakama zimefuatwa hivyo Lulu  ametoka! Kifuatacho ni Lulu kugeuka kuwa lulu mbele ya media kwani vyombo vyote vya habari, ndani na nje vitamtafuta kwa ajili ya interviews. Sababu ni kuwa inaaminika Lulu pekee ndiye anayejua ukweli wa nini kilitokea usiku ule kabla ya umauti wa The Great!

Ni ukweli kuwa Lulu atakuwa bize sana kipindi hiki wakati kila media ikitaka story hiyo ya ndani ‘Exclusive’ ya kifo cha Kanumba. Je, Lulu ataweza kuendana na presha za media hizi? Je, ni wakati wa Lulu kupumzika kiakili na kimwili baada ya sekeseke hili, japo bado halijaisha!
Lulu ni lulu sasa! Ana mpango gani? Ameshafikiria tukio lake kuligeuza na kuwa bidhaa? Au yeye ataishia kulia na kupangusa machozi atakapokuwa anahojiwa na huku wengine wakiingiza pesa? Wakili wake pia ana mchango gani katika hili? Wazazi je?


Wapo waliojigeuza lulu kuendana na matukio na usupastaa wao mbele ya jamii. Mfano harusi ya Jay Dee na Gadner. Bang magazine pekee walipewa haki juu ya picha hizo. Huko South Africa kuna media ambayo tayari imeshanunua haki za kurusha kifo cha Mzee Nelson Mandela. Hayo ni baadhi tu ya matukio ambayo yaligeuzwa na mengine yataweza kugeuzwa kuwa bidhaa na kuingiza hela nyingi!


No comments:

Post a Comment